Niliaibika sana, sitakaa nisahau

Kitombise

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
8,517
25,428
Nakumbuka nilipokuwa primary kipindi hiko nilikuwa na girlfriend wangu ambaye tulikuwa tunaishi jirani na tunasoma shule moja, darasa moja na dawati moja. Kila siku tulikuwa tunaenda shuleni pamoja na tunarudi pamoja nyumbani.

Ulikuwa ukinikosa nyumbani basi ujue nko kwao, na kila weekend tulikuwa tunashinda pamoja mpaka tunasahau kama kuna kula. Nakumbuka baba angu alikuwa akinigombeza kuwa nmezidisha michezo sana mpaka perfomance yangu class ikawa inashuka na kusahau hata muda wa kurudi kula kisa michezo.

Sasa siku moja jumapili niliangalia movie sana mpaka mida ya saa 9 za usiku ndo nkaenda kulala, sasa asubuhi yake niliamka mchovu na nikakumbuka ni siku ya shule ikanibdi niende japo nilikuwa nasinzia sana njani huku nikielekea school.

Baada ya kufanya usafi tukaingia class. NILIKUWA NIPO DARASA LA TATU KIPINDI HICHO.
Sasa tulipoingia tena class saa 13:00 baada ya kutoka lunch, tena lunch yenyewe ni makande na jinsi maharage yalivyokuwa na usingizi.

Nikawa NASINZIA mbayaa ukijumlisha tena na jana Kuchelewa kulala ndo ikawa balaa sana. ilikuwa ni somo la English hvyo teacher alivyoingia na kuanza kufundishwa nikawa nimepitiwa na usingizi baada ya ule uchovu mkali.

Punde kidogo nkashtushwa na yule girlfriend wangu kuwa teacher alikuwa amenipoint mm nijibu swali. aaaagrrh! hapo nkashtuka balaaa alafu na hata hili swali lenyewe nlikuwa sijui kaulizaje. basi nikawa nabababika tuu mara teacher akarudia tena kuuliza "what the meaning of TOGETHER?"

Basi nkawa nababaika bila kujua nijibu vipi ila nkasikia yule GF wangu akiniambia kwa mbali "jibu lake ni TUNAWAKILISHA"Heeeeh! basi na mimi ikavuta picha huku nikipambanua lile jibu nililolisikia nikalicombine na lile neno ka kwenye Chanel 5 kuwa wanaandikaga "TOGETHER, TUNAWAKILISHA" basi hapo nikaona Ewaaah! hili ndo jubu, nikajibu kwa sauti kubwa huku nikihiamini kuwa jibu lake ni TUNAWAKILISHA.

Heeh! mara nikasikia kila mtu kaduwaa baada ya hapo wanafunzi pamoja na mwalimu wakacheka mbayaaaa.Basi hyo siku nilichekwa sana karibia siku nzima mpaka nikawa sina raha. keaho yake pia nilipikuja shule wakawa tayari wameshanibatiza jina naitwa TUNAWAKILISHA. ikawa kila mahali nikipita naitwa tunawakilisha, tubawakilisha mpaka jina nikalizoea mpka namaliza darasa la 7 nikawa naitwa hivyo hvyo Tunawakilisha.Tunawakilisha.

YANI ILIKUWA NI AIBU AMBAYO MPAKA SASA HIVI NAONA IMEZIDI KULIKO AIBU ZOTE ZILIZOWAHI KUNIPATA.Je na wewe mdau unakumbuka ulipikuwa scul ni aibu gani ilishawahi kukupa/kukumba?
 
mmmmmmmmmmm,mie sikuizi sijui nikoje sijui majukumu na ulezi nakua sikumbuki vya zamani kabisaaaaaaaaaaaaaa...
 
PUMBA KABISA
 
asa mkuu mbona hiyo story umeianzia mbaaliii, ungeandika tu ulilala darasani ukaulizwa swali, ukajibu tuna wakilisha .............. sasa girl frend sijui unashinda kwao ya nn yote hayo.
 
Ha ha ha ha ! Umenikumbusha wakati niko darasa la 6! Kuna kajamaa kalikua kafupi halafu kakubwa kwa umri (Kijeba) swakati huo Waziri Mkuu alikua Frederic Sumaye nakumbuka teacher akauliza Waziri Mkuu wa Tanzania ni nani, lilikua somo la Maarifa ya Jamii! Yule bwana alikua amesinzia nadhani kipindi kile Yusuph Makamba ni Mkuu wa Mkoa wa DSM..alipokurupushwa akaulizwa swali ghafla akaropoka "Yusuph Makambaa" Mpaka kesho "Makamba" limekua jina lake na urefu ule! Hahah
 
Umetisha baab,imefanana na moja ilitokea mahakamani mshtaki katukanwa wakiwa kwenye chumba cha mahakamu hakimu akamuuliza mshtaki unaweza sema mshtakiwa alikutukanaje...Mshtaki akasema hapana hakimu siwezi taja alivyonitukana labda niandike halafu wazee wa mahakama wanisaidie kusoma hakimu akamkubalia, akandika kuwa mshtakiwa alimuambia "Twende tukadu" aliandika bila tafsida hapo nimepyunguza ukali wa maneno...Basi kikaratsi kile akapewa mzee wa mahakama mwanamke asome yule mzee akaona soo...Akampa mzee wa mahakama aliekuwa pembeni yake kumbe yule mzee wa pembeni alikuwa amelala...Yule mama mzee wa mahakama akamgusa kwa taratibu yule mzee alivyoamka akamsogezea hicho kikaratasi..kilichaondikwa ''TWENDE TUKADU" yule mzee bila kujua mahakam yote inamuangalia akamuuliza yule mama mzee wa mahakam aliempa hicho kikaratasi''EEH MAMA TWENDE SASA HIVI? Hakimu akaingilia kati kuwa we saidia mahakama kusoma maneno ya mshtaki si wewe umeulizwa...Mzee akaona soo mbaya.
 
Kuna uzi umeanzishwa special kw ajili ya hizi!! Ungeipeleka humo....
 
duuh! huyo pia alitisha sanaaa
 
kweli huyu aliaibika kuliko mimi
 
Hivi shule ya msingi kuna watu walikua na girlfriend?
 
mbona sijakuelewa kabisa darasa la tatu umeshaanza udanganyifu kwa hii jinsia pendwa au ulikuwa kijeba

kastori kanavutia kidogo
 
Mimi nakumbuka siku hiyo ambayo tulikuwa darasa la kwanza karibia watoto 84, na kati ya hao ni wanne tu wanajua kuongea kiswahili, wengine wote wanazungumza kinyumbani tu....! Halafu alikuwepo kaka mmoja mkubwa kahamia shuleni kwetu akitokea darasa la tatu, na ndio mmojawapo wanaoweza kuongea kiswahili...! Sisi ndio tulikuwa waanzilishi wa shule ile....! Ghafla mkaka yule aliingia kwa kuchelewa na kumkuta mwalimu akifundisha...! Wote tulisimama kumsalimia "shikamoo kaka", viniginevyo tungekoma mwalimu akitoka....! Kumbe mezani mwalimu alikuwa na soda yake imefunguliwa na andazi...! Halafu wakati tunaandika yaliyoandikwa ubaoni, mwalimu akatoka nje (nafikiri alienda uani)...! Then, jamaa akainuka na kwenda mezani, akaling'ata lile andazi na kumezea soda ile pia...! Akarudi kukaa kule nyuma ya darasa...!
Kidogo mwalimu akarudi na kukuta andazi lake limemegwa....! Aliongea hadi kimeru (kikwao)...! Wale watoto wanne wanaojua kuongea kiswahili; akiwemo jamaa, walijitetea na kupewa kazi maalum kila mmoja...! Jamaa alipewa kazi ya kuhakikisha kila atakayechapwa atarudi kuunga mstari tena na kusubiri kuchapwa tena, wengine walipewa kazi ya kukata fimbo....! Nakumbuka siku hiyo tulichapwa hadi saa ya kwenda nyumbani....! Hakuna hata mmoja aliyedhubutu kumnyooshea jamaa kidole, kisa ungepita njia gani baadaye....!
 
Mtoto wa darasa la tatu anakua na mpenzi?
sema sishangai sana kama mimi nilianza kuwafanya nikiwa na miaka kam miwili au mitatu ule msimu mzuri wa kimama mama nilikuwa nang'ania kila siku kuw baba na mtoto namtuma kila saa ili nibaki na mama yake
 
mbona sijakuelewa kabisa darasa la tatu umeshaanza udanganyifu kwa hii jinsia pendwa au ulikuwa kijeba

kastori kanavutia kidogo
kwani maana ya Girlfriend si rafiki wa kike, ila siyo kwamba alikuwa dem wangu. Hapana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…