Nikifuatilia yanayoendelea Tanga kwenye kesi ya Kombo najiuliza kwanini tulitumia pesa nyingi kuunda tume ya haki jinai? Inaisaidia nini nchi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,037
4,752
Leo RCO amenyima dhamana na mahakama ipo imetulia tu. Wakati haya yanafanyika kuna watu wamelipwa mabilioni kuandaa ripoti ya haki jinai.

Unajiuliza tafsiri ya haki jinai ni nini? Je RCO anaweza kuwakatalia mahakama? Jaji Mkuu anaposhuhudia haya yakiripotiwa kwenye vyombo vya habari akakaa kimya anategemea nn?

Je, Mhe. Rais akianza kuwatumbu waliopo nyuma ya haya mtasema anawaonea? Kombo anaondoka na mtu

PIA SOMA
- Sasisho: Kombo Mbwana wa Tanga akosa dhamana licha ya kutimiza masharti ya dhamani kama ilivyopangwa
 
Kuna mambo ukiyasikia ya kidhalimu yanaumiza mpaka basi.

Unajiuliza wewe mtu baki iwapo uko mbali yanakuumiza hivyo je mhusika Mkuu na wazazi wake , mkewe , watoto na nduguze wanaumia kiasi gani?
 
Yaani huyo Hakimu wa Tanga ,amenajisi mhimili wa Mahakama..Vitendo kama hivi vya huyu HAKIMU vinafanya jamii kupunguza IMANI kwa Mahakama..ni AIBU!
 
Kwani anatuhumiwa kwa kosa gani hasa?

Mbona tuhuma zake hazitajwi umma tukajua ?
Itakuwa ni kesi ya uchochezi tu na ambao mara zote washitakiwa huishinda Jamhuri kabla na hata baada ya hukumu kutoka! Au Hakimu atoe hukumu ya kukengeuka, na mwisho wa siku na yeye apate uteuzi.
 
Back
Top Bottom