Nife au niende gerezani?

Intelligent businessman

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
26,758
54,386
SIMULIZI; NIFE AU NIENDE GEREZANi
MTUNZI:Alli H
MWANDISHI: Intelligent businessman

SEHEMU YA 01

Ubaridi ulikuwa ukiingia mwilini utadhani nilikuwa nimeingia kwenye Jokofu lakini wala sikujali, nilichokuwa nawaza ni jinsi gani naweza kuwapoteza wanaonikimbiza, kilichonitisha zaidi wale watu walionekana nia yao ni kunidhuru mana kama ingelikuwa kuna usalama basi wasingelikuwa wananifukuza na silaha. Sikuwa mjinga kusimama wala kujisalimisha nilichoamua ni kukimbia, baada ya kukimbia sana nilijikuta nikipiga mweleka na kuanguka chini, wakati huo pumzi zangu zilikuwa zikiiingia na kutoka kwa kasi ya ajabu. Nilijikokota na kujichomeka kwenye kichaka kilichokuwa karibu. Jasho lilianza kunivuja kila kona ya mwili wangu utadhani nilikuwa nimemwagiwa maji, nilijaribu kuangaza macho yangu katika msitu mnene niliokuwamo, kulikuwa kuna miti mirefu iliyofungamana lakini chini ya miti ile kulijaa vichaka vidogo vidogo.

Sikuelewa namna ya kutoka ndani ya msitu ule, mbaya zaidi ilikuwa ni nyakati za usiku. Licha ya kuwepo kwa anga hafifu iliyotokana na mbalamwezi lakini msitu ulikuwa unatisha kuliko neno kutisha. Kilichonishangaza zaidi ni watu waliokuwa wananikimbiza, sikujua lengo lao lilikuwa ni nini kwangu lakini nilihisi sio watu wema kwani walikuwa wamebeba mapanga yalioleta mng’ao ndani ya giza nene, sio mapanga tu! walikuwa na silaha nyengine kama mikuki na mishale, idadi yao sikuwa na uhakika nayo lakini nilihisi watakuwa ni zaidi ya watano. Kipindi nipo kwenye kile kichaka kidogo, nilianza kusikia majani yakitikisika na kutoa sauti kuashiria kuna watu wanakuja upande niliokuwa nimejificha.

La! Haula..!
Sikutaka kuamini ulinipitia mshale karibu na shavu la kulia, ilikuwa bado kidogo tu unipate usoni. Nilistuka huku nikijiuliza wamenionaje pale nilipojificha, akili ya kuendelea kubaki kwenye kichaka iliisha, nilikurupuka kama mtu aliyefumaniwa na kuanza kukimbia kama mwendawazimu.

Katika kukimbia sikuwa na uelekeo maalumu nilijikuta nikikimbia ovyo ovyo lengo langu likiwa ni kujiokoa na umauti uliokuwa unaninyemelea, akili yangu iliniambia wale watu sio watu wazuri na endapo watafanikiwa kuninishika tu basi nimeuwawa. Hata sijui walikuwa na uwezo gani, licha ya kukimbia kwa kasi lakini nilipogeuka nyuma niliwaona wakinikaribia wakiwa na mapanga mkononi. ‘Ohhh! Shit! Wanataka nini hawa’, nilijisemea huku nikizidi kuongeza mwendo. Ghafla niliuvaa mkongwashale, huu ni mti wenye tabia ya kuzagaa chini kama kamba tena kamba zake huwa na miba inayochomoza kwa mbali, mti ule ulininasa kwenye miguu na kunifanya nianguke kama mzigo, nilipotaka kunyanyuka nikimbie nilihisi mguu wangu wa kushoto ukiniuma sana kuashiria umepata hitilafu maeneo ya kwenye goti.

'Ama kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni' lakini nafsi yangu ilizidi kuniasa nisijilegeze na kutiwa mbaroni na wale watu wabaya. Kiukweli nilikuwa nipo hoi bin taabani, dalili za kushikwa na wale mabaradhuli zilianza kujionesha waziwazi huku harufu ya kifo ndo ilikuwa ikinukia kama manukato ya bei ghali. Nikaona isiwe tabu, ndipo nilipoanza kujizoazoa ili nianze kukimbia kwa mara nyengine lakini nilikuwa nimechelewa, tayari walikuwa wameshanizunguka kila eneo, mtu mmoja alieyekuwa mrefu zaidi ya wote mwenye minywele mingi alinisogelea na Panga lililong’aa, hakuwa na mahojiano na mimi, aliponifikia alinyanyua Panga lake juu na kuelekeza usawa wa tumbo langu huku akiyatoa meno yake mabaya yenye kutisha, Panga lilikuja kwa kasi lakini kabla halijatua tumboni kwangu, nilipiga kelele kwa nguvu.
"Aaaaaaahhhhhhhhh aaaaahhhh!!".

Nilistuka kitandani nilipokuwa nimelala, ilikuwa ni ndoto ya ajabu sana, mwili wangu ulikuwa umelowa jasho.
'Ndoto gani hii ya ajabu.!?', nilijiuliza lakini sikuweza kujijibu hilo swali.

Akili yangu bado ilikuwa haijakaa sawa kabisa, maisha yangu niliyaona kama yameshaingia doa, nilikaa kwa unyonge sana katika kitanda chenye hadhi ya kuitwa tano kwa sita. Machozi yalianza kunilenga nilipoanza kumkumbuka Sharifa, ni mwanamke niliyetokea kumpenda kwa dhati lakini mpaka muda huo sikujua kama wameshamuua au yupo wapi, hata njia ya kumpata niliikosa kutokana na mazingira aliyopotea, yote haya yalichangiwa na tuhuma za mauaji zilizonilazimu nikimbie nyumbani na laiti ningejua basi nisingekimbia na Sharifa.
'Sharifa kwanini usingenisubiri tu nyumbani, ona sasa sina uhakika na maisha yako, sijui upo wapi, sijui kama upo hai au wameshakuua'. Nilijisemea ndani ya nafsi yangu.

Chozi lilianza kunitoka nikiwa sielewi maisha yangu yanaelekea wapi.

"Amriiiii..!!, Amriii..!!". Sauti ya kaka akiniita ilinistua kutoka katika ulimwengu wa mawazo.

" Naam! kaka". Niliitikia sauti ile ya kaka ambayo ilitokea upande wa nje wa chumba nilichokuwemo.

"Uje mara moja.".

"Sawa nakuja.". Mida hiyo giza tayari lilishaingia, nilikurupuka kutoka kitandani na kwenda kuwasha taa na kuivuta suruali yangu ya Jeans iliyokuwa inaning'inia kwenye kamba, kisha nikajitupia na fulana, nikaisogelea saa yangu ya mkononi iliyopo mezani, ilikuwa inaniambia ni saa 1 na dakika 47 usiku. Hapo nikagundua nimelala muda usio mrefu sana. Ilibidi nitoke sebleni ili nikamsikilize kaka Hamisi alikuwa anasemaje.

Nilipowasili sebuleni nilijipunzisha kwenye Kochi huku macho yangu nikiyaelekeza kwenye Tv. Muda huo kaka alikuwa Chumbani kwake. Nyumba ya kaka yangu huyo haikuwa nyumba yenye hadhi kubwa, ilikuwa ni nyumba yenye thamani ya kawaida sana, wakati huo mkewe ambae ni Shemeji yangu alikuwa amesafiri kwenda kuwaona wazazi wake.

Kaka Hamisi alikuwa ni kaka yangu ambae tumezaliwa tumbo moja na yeye akiwa ni wakwanza nikifuatia mimi halafu hakuna mwengine tena. Nyumbani kwetu ni Mafia lakini yeye aliamua kuvuka bahari na kuhamia Bungu lakini ikiwa ni ndani ya Mkoa wa Pwani, baada ya majanga yaliyonitokea nikaamua kukimbilia kwake na si hivo tu bado nilihitaji kukimbilia mbali zaidi.

Muda mfupi baadae kaka alikuja Sebleni kisha akaketi kwenye Kochi nililokuwepo.

"Vipi hivi sasa unajisikiaje ndugu.!".

" Nipo fresh bro!". Nilijikaza kiume .

"Kwanza pole sana ndugu yangu kwa yaliyotokea.". Kaka alinipa pole lakini hakuishia hapo akaendelea.

" Hivi Amri mdogo wangu, ni sahihi umeua.!?". Nilistuka kutoka kwenye mawazo baada ya kaka kuniuliza swali hilo.

"Kaka mimi sijaua, hata huo uwezo wa kumwaga damu ya mtu mimi sina lakini kama nisingekimbia unafikiri ile kesi ni ya nani.!?".

" Hata mimi naamini ndugu, enhe! nambie sasa ilikuwaje kuwaje mana niliongea na wazee nyumbani walinihadithia lakini naona nahitaji uniambie wewe muhusika wa tukio, ilikuwaje kuwaje..?". Kaka alinigeukia huku akikaa mkao wa kusikiliza yaliyonikuta hadi nikakimbilia kwake.

Nilishusha pumzi ndeefu lakini hali ya kulengwa na machozi ilibaki pale pale, kukosa kujua alipo Sharifa ilikuwa ni kama nimefanyiwa dhuluma ya kiungo cha mwili wangu. Niligeuza macho yangu na kumgeukia kaka ili nimpe mkasa mzima....

NAAAM! HII NI SEHEMU YA KWANZA NAOMBA TUKUTANE KATIKA SEHEMU YA PILI.

MASWALI YA KUJIULIZA.
Je Amri ni nani na amepatwa na nini na vipi maisha ya hapo baadae yalikuwaje..!?
Aliyeuwawa ni nani na kifo chake kilikuwaje..!?
Je huyo Sharifa kimempata nini..!?
Nini kitakachoendelea..!?

Hayo maswali yote yatajibiwa kila tutakavyozidi kusonga mbele.

NAKUSIHI USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA.

FB_IMG_16860196830983857.jpg
 
SIMULIZI; NIFE AU NIENDE GEREZANi
MTUNZI:Alli H
MWANDISHI: Intelligent businessman

SEHEMU YA 01

Ubaridi ulikuwa ukiingia mwilini utadhani nilikuwa nimeingia kwenye Jokofu lakini wala sikujali, nilichokuwa nawaza ni jinsi gani naweza kuwapoteza wanaonikimbiza, kilichonitisha zaidi wale watu walionekana nia yao ni kunidhuru mana kama ingelikuwa kuna usalama basi wasingelikuwa wananifukuza na silaha. Sikuwa mjinga kusimama wala kujisalimisha nilichoamua ni kukimbia, baada ya kukimbia sana nilijikuta nikipiga mweleka na kuanguka chini, wakati huo pumzi zangu zilikuwa zikiiingia na kutoka kwa kasi ya ajabu. Nilijikokota na kujichomeka kwenye kichaka kilichokuwa karibu. Jasho lilianza kunivuja kila kona ya mwili wangu utadhani nilikuwa nimemwagiwa maji, nilijaribu kuangaza macho yangu katika msitu mnene niliokuwamo, kulikuwa kuna miti mirefu iliyofungamana lakini chini ya miti ile kulijaa vichaka vidogo vidogo.

Sikuelewa namna ya kutoka ndani ya msitu ule, mbaya zaidi ilikuwa ni nyakati za usiku. Licha ya kuwepo kwa anga hafifu iliyotokana na mbalamwezi lakini msitu ulikuwa unatisha kuliko neno kutisha. Kilichonishangaza zaidi ni watu waliokuwa wananikimbiza, sikujua lengo lao lilikuwa ni nini kwangu lakini nilihisi sio watu wema kwani walikuwa wamebeba mapanga yalioleta mng’ao ndani ya giza nene, sio mapanga tu! walikuwa na silaha nyengine kama mikuki na mishale, idadi yao sikuwa na uhakika nayo lakini nilihisi watakuwa ni zaidi ya watano. Kipindi nipo kwenye kile kichaka kidogo, nilianza kusikia majani yakitikisika na kutoa sauti kuashiria kuna watu wanakuja upande niliokuwa nimejificha.

La! Haula..!
Sikutaka kuamini ulinipitia mshale karibu na shavu la kulia, ilikuwa bado kidogo tu unipate usoni. Nilistuka huku nikijiuliza wamenionaje pale nilipojificha, akili ya kuendelea kubaki kwenye kichaka iliisha, nilikurupuka kama mtu aliyefumaniwa na kuanza kukimbia kama mwendawazimu.

Katika kukimbia sikuwa na uelekeo maalumu nilijikuta nikikimbia ovyo ovyo lengo langu likiwa ni kujiokoa na umauti uliokuwa unaninyemelea, akili yangu iliniambia wale watu sio watu wazuri na endapo watafanikiwa kuninishika tu basi nimeuwawa. Hata sijui walikuwa na uwezo gani, licha ya kukimbia kwa kasi lakini nilipogeuka nyuma niliwaona wakinikaribia wakiwa na mapanga mkononi. ‘Ohhh! Shit! Wanataka nini hawa’, nilijisemea huku nikizidi kuongeza mwendo. Ghafla niliuvaa mkongwashale, huu ni mti wenye tabia ya kuzagaa chini kama kamba tena kamba zake huwa na miba inayochomoza kwa mbali, mti ule ulininasa kwenye miguu na kunifanya nianguke kama mzigo, nilipotaka kunyanyuka nikimbie nilihisi mguu wangu wa kushoto ukiniuma sana kuashiria umepata hitilafu maeneo ya kwenye goti.

'Ama kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni' lakini nafsi yangu ilizidi kuniasa nisijilegeze na kutiwa mbaroni na wale watu wabaya. Kiukweli nilikuwa nipo hoi bin taabani, dalili za kushikwa na wale mabaradhuli zilianza kujionesha waziwazi huku harufu ya kifo ndo ilikuwa ikinukia kama manukato ya bei ghali. Nikaona isiwe tabu, ndipo nilipoanza kujizoazoa ili nianze kukimbia kwa mara nyengine lakini nilikuwa nimechelewa, tayari walikuwa wameshanizunguka kila eneo, mtu mmoja alieyekuwa mrefu zaidi ya wote mwenye minywele mingi alinisogelea na Panga lililong’aa, hakuwa na mahojiano na mimi, aliponifikia alinyanyua Panga lake juu na kuelekeza usawa wa tumbo langu huku akiyatoa meno yake mabaya yenye kutisha, Panga lilikuja kwa kasi lakini kabla halijatua tumboni kwangu, nilipiga kelele kwa nguvu.
"Aaaaaaahhhhhhhhh aaaaahhhh!!".

Nilistuka kitandani nilipokuwa nimelala, ilikuwa ni ndoto ya ajabu sana, mwili wangu ulikuwa umelowa jasho.
'Ndoto gani hii ya ajabu.!?', nilijiuliza lakini sikuweza kujijibu hilo swali.

Akili yangu bado ilikuwa haijakaa sawa kabisa, maisha yangu niliyaona kama yameshaingia doa, nilikaa kwa unyonge sana katika kitanda chenye hadhi ya kuitwa tano kwa sita. Machozi yalianza kunilenga nilipoanza kumkumbuka Sharifa, ni mwanamke niliyetokea kumpenda kwa dhati lakini mpaka muda huo sikujua kama wameshamuua au yupo wapi, hata njia ya kumpata niliikosa kutokana na mazingira aliyopotea, yote haya yalichangiwa na tuhuma za mauaji zilizonilazimu nikimbie nyumbani na laiti ningejua basi nisingekimbia na Sharifa.
'Sharifa kwanini usingenisubiri tu nyumbani, ona sasa sina uhakika na maisha yako, sijui upo wapi, sijui kama upo hai au wameshakuua'. Nilijisemea ndani ya nafsi yangu.

Chozi lilianza kunitoka nikiwa sielewi maisha yangu yanaelekea wapi.

"Amriiiii..!!, Amriii..!!". Sauti ya kaka akiniita ilinistua kutoka katika ulimwengu wa mawazo.

" Naam! kaka". Niliitikia sauti ile ya kaka ambayo ilitokea upande wa nje wa chumba nilichokuwemo.

"Uje mara moja.".

"Sawa nakuja.". Mida hiyo giza tayari lilishaingia, nilikurupuka kutoka kitandani na kwenda kuwasha taa na kuivuta suruali yangu ya Jeans iliyokuwa inaning'inia kwenye kamba, kisha nikajitupia na fulana, nikaisogelea saa yangu ya mkononi iliyopo mezani, ilikuwa inaniambia ni saa 1 na dakika 47 usiku. Hapo nikagundua nimelala muda usio mrefu sana. Ilibidi nitoke sebleni ili nikamsikilize kaka Hamisi alikuwa anasemaje.

Nilipowasili sebuleni nilijipunzisha kwenye Kochi huku macho yangu nikiyaelekeza kwenye Tv. Muda huo kaka alikuwa Chumbani kwake. Nyumba ya kaka yangu huyo haikuwa nyumba yenye hadhi kubwa, ilikuwa ni nyumba yenye thamani ya kawaida sana, wakati huo mkewe ambae ni Shemeji yangu alikuwa amesafiri kwenda kuwaona wazazi wake. Kaka Hamisi alikuwa ni kaka yangu ambae tumezaliwa tumbo moja na yeye akiwa ni wakwanza nikifuatia mimi halafu hakuna mwengine tena. Nyumbani kwetu ni Mafia lakini yeye aliamua kuvuka bahari na kuhamia Bungu lakini ikiwa ni ndani ya Mkoa wa Pwani, baada ya majanga yaliyonitokea nikaamua kukimbilia kwake na si hivo tu bado nilihitaji kukimbilia mbali zaidi.

View attachment 2696344
Nenda kafie gerezani🤓🤓🤓🤓🤓🤓🤓
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom