Mambo vipi wanaJF
Naombeni ushauri wenu kama unalo lolote la kunishauri!!
Nina mpenzi wangu ambae tuna muda wa miezi 7 sasa na nampenda sana tena sana tu!Jambo linalonifanya niombe ushauri ni hali ambayo kila mara inajitokeza kwake!
Kiufupi kabla ya kuanza mahusiano, alishawahi kuolewa na wakabahatika kupata mtoto mmoja lakini kwa bahati mbaya mume wake alipatwa na mauti mwaka 2014 Tunduma ilipotokea vurugu na akapigwa risasi, akakimbizwa hospital lakini kwa bahati mbaya akapoteza uhai!! Ameishi tangu kipindi hicho akiwa hayupo katika mahusiano hadi kipindi ambacho nilikutana nae!!
Nikampenda, nikamuomba atambue hisia zangu na ikafika kipindi akawa yupo tayari kuwa namimi!
Tatizo lililopo sasahivi, kila wakati amekuwa akilia tu mara tu anapokumbuka uwepo wa mumewe wa kwanza, istoshe hali hyo imekuwa ya kujirudia rudia na nilipofanya uchunguzi nikagundua alikubali kuwa namm kwakuwa alikuwa mpweke tu lkn hakuwa na mapenzi, bado anamkumbuka sana mumewe!
NIFANYAJE KUHUSU HILI?PLEASE NAOMBENI USHAURI,ASANTE!