A
Anonymous
Guest
Jiuzi nilienda ofisi ya NIDA Kinondoni huko Kawe. Kisa mtandao wao kukata nilipoenda mara ya kwanza nilipaswa kuacha makaratasi yangu ofisini kwao. Niliporudi kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole yaani kuingizwa kwenye mfumo, maafisa wote wa chumba cha picha walikuwa bize na shughuli zao. Wakaniambia nipitie fomu zote zilizokaa mezani kwa kutafuta ya kwangu mwenyewe.
Kwa hiyo niliweza kuangalia na kupitia taarifa binafsi za watu kama mia kabla ya kupata fomu yangu. Hapo sikuwa na nia mbaya na sikuangalia sana fomu za watu wengine ila nilishangaa sana. Kumbe hivi ndivyo taarifa zetu zinavyolindwa na NIDA. Mtu anaweza kuingia chumbani kwao akijifanya kama aliacha fomu yake kule jana na ana access rahisi ya taarifa za watu, majina, namba za simu, makazi, nk.
Aidha kirasmi hairuhusiwi kutumia simu ndani ya chumba hicho lakini kanuni hiyo haitelezeki. Wengi waliosubiri kupata huduma kule walitumia simu zao bila kusitishwa. Hii inahatarisha taarifa zetu zaidi.
Hatua zichukuliwe kuhakikisha faragha yetu na ulinzi wa taarifa yetu binafsi. Maafisa hawa waelimishwe kuhusu hatari za vitendo hivi na umuhimu wa kufuatilia itifaki ya kulinda taarifa binafsi.