Nicole amekosa dhamana karudishwa rumande baada ya kesi yake kusikilizwa

Wild Flower

JF-Expert Member
Jul 20, 2023
401
849
1741677030026.png

Mwigizaji Joyce Mbaga (32) maarufu kama 'Nicole Berry' leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Jijini Dar es salaam amesomewa mashtaka matatu ikiwemo kuendesha genge la uhalifu na kupokea shilingi za Kitanzania milioni 185.5 kutoka kwa umma bila kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo mbali ya Nicole, Mshtakiwa mwingine ametajwa kuwa ni Rehema Mahanhu (31).

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,2025 na Washtakiwa hao wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na Wadhamini wawili na kuwasilisha Mahakamani fedha taslimu shilingi milioni 46.3 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Nicole na mwenzake wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Rhoda Maingu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira wakidaiwa kuyatenda makosa hayo kati ya Julai 2024 na Machi 2025 ndani ya Mkoa wa Dar es salaam.

Wakili Maingu alidai kuwa katika shitaka la kwanza Washtakiwa wanatuhumiwa kuongoza genge la uhalifu ambapo wanatuhumiwa kwa miezi hiyo na miaka hiyo wakiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam waliendesha biashara ya kihalifu au jinai, kwa lengo la kujipatia faida kutoka kwa jamii na kupokea amana au miamala bila kupata leseni kutoka BoT.

Katika shitaka la pili Washtakiwa wote wanatuhumiwa kati ya Julai 2024 na Machi 2025 wakiwa eneo lisilofahamika ndani ya mkoa wa Dar es salaam walipokea amana ya shilingi milioni 185,515,000 kutoka kwa jamii bila kuwa na leseni na katika shtaka la tatu Washtakiwa waliendesha mfumo wa malipo bila kuwa na leseni ya malipo inayotolewa na BoT.​
 
Duuh Raha,karaha!
 
Kweli na hilo tako lote na nyonyo wameshindwa mdhamin mtoto mzuri kwelii??? Madanga yenye pesa yamepotelea wapi
Ungekuwa wew ungewez kuchoma 46m kwa mtu ambae ana jinasibu kwamba anatumia 6m kwa siku then anavimba na mambo ya kifahari tena kachukua pesa kafanyia matumiz yake wew ukamlipie wanaume sio wajinga kiasi icho maybe mwanaume mjinga ndo atafanya huo ujinga
 
Mwigizaji Joyce Mbaga (32) maarufu kama 'Nicole Berry' leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Jijini Dar es salaam amesomewa mashtaka matatu ikiwemo kuendesha genge la uhalifu na kupokea shilingi za Kitanzania milioni 185.5 kutoka kwa umma bila kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ambapo mbali ya Nicole, Mshtakiwa mwingine ametajwa kuwa ni Rehema Mahanhu (31).

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,2025 na Washtakiwa hao wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na Wadhamini wawili na kuwasilisha Mahakamani fedha taslimu shilingi milioni 46.3 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Nicole na mwenzake wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Rhoda Maingu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Ramadhani Rugemalira wakidaiwa kuyatenda makosa hayo kati ya Julai 2024 na Machi 2025 ndani ya Mkoa wa Dar es salaam.

Wakili Maingu alidai kuwa katika shitaka la kwanza Washtakiwa wanatuhumiwa kuongoza genge la uhalifu ambapo wanatuhumiwa kwa miezi hiyo na miaka hiyo wakiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam waliendesha biashara ya kihalifu au jinai, kwa lengo la kujipatia faida kutoka kwa jamii na kupokea amana au miamala bila kupata leseni kutoka BoT.

Katika shitaka la pili Washtakiwa wote wanatuhumiwa kati ya Julai 2024 na Machi 2025 wakiwa eneo lisilofahamika ndani ya mkoa wa Dar es salaam walipokea amana ya shilingi milioni 185,515,000 kutoka kwa jamii bila kuwa na leseni na katika shtaka la tatu Washtakiwa waliendesha mfumo wa malipo bila kuwa na leseni ya malipo inayotolewa na BoT.​
kafanya nini kwani ,mbona mafumbo mafumbo tu hapa
kuunda genge la uhalifu ndo kufanyaje
 
Back
Top Bottom