Nichukue pikipiki gani kati ya hizi tatu?

Jul 8, 2017
81
61
Wakuu, baada ya kufanya utafiti na kukusanya maoni toka kwa watumiaji wengine kabla ya kununua, nimepata pikipiki tatu ambazo zinashindana kwa vigezo ninavyovihitaji mimi. Vigezo hivyo ni:
1. Uwezo wa kutumia mafuta kidogo kwa safari za km 50 kila siku.
2. Ubora wa injini (sitegemei kumwona fundi kila wiki).
3. Uwezo wa kutembea njia rough na lami, maana naishi mjini ila nafanya kazi kijijini.

Baada ya upembuzi huo nimepata pikipiki hizi ambazo naomba mnichagulie moja ya kununua.

images (2).jpeg

Hii ni TVS HLX 150 yenye gia 5.

images (1).jpeg

Honda ACE150 hii.

images (3).jpeg

Boxer 150 X hii.

Nichukue ipi wakuu maana zote zinanichanganya kimaamuzi.
 
Boxer BM 150 ni nzuri kama wewe una kimo cha wastani. Ninayo tangu 2023 mwanzoni bado iko powa naitumia kwa matumizi yote off road na Rami maana naishi mjini ila shughuli zangu za kiuchumi zinategemea zaidi shambani.

-Ulaji mzuri wa mafuta
-Comfort ability hasa ukizingatia mie sio mrefu sanaa kwahyo inanipa hali ya utulivu ukilinganisha na Tvs kidogo ndefu sanaa
-Muonekano pia huwa sipendi ile show ya nyuma ya Tvs
 
Wakuu, baada ya kufanya utafiti na kukusanya maoni toka kwa watumiaji wengine kabla ya kununua, nimepata pikipiki tatu ambazo zinashindana kwa vigezo ninavyovihitaji mimi. Vigezo hivyo ni:
1. Uwezo wa kutumia mafuta kidogo kwa safari za km 50 kila siku.
2. Ubora wa injini (sitegemei kumwona fundi kila wiki).
3. Uwezo wa kutembea njia rough na lami, maana naishi mjini ila nafanya kazi kijijini.

Baada ya upembuzi huo nimepata pikipiki hizi ambazo naomba mnichagulie moja ya kununua.

View attachment 3308219
Hii ni TVS HLX 150 yenye gia 5.

View attachment 3308220
Honda ACE150 hii.

View attachment 3308223
Boxer 150 X hii.

Nichukue ipi wakuu maana zote zinanichanganya kimaamuzi.
Ningekuwa mimi ningechukua Boxer 125 nisave mafuta zaidi.
 
Back
Top Bottom