SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Yapo Mambo mengi ukiyachunguza, utagundua tabia zilizomo ndani ya Mgombea wa CHADEMA na hapa ni wazi kuwa amekosa agenda.
Sehemu ya hotuba yake ya Jana imekuwa na mbwembwe nyingi huku akishangiliwa na watu wasio weza kuhoji chochote kutoka kwa mgombea huyo.
Anasema Raisi anatufanya wajinga kwa kusema amejenga Bwawa la Umeme, Reli kanunua ndege nk. Nimuombe Lisu na wanachadema wenzake wajisikilize halafu watujibu. Je nikweli wamefanywa wajinga? Au wao ndio wanajifanya Wajinga?.
Bunge La mama Anne Makinda. Tundu Lisu alisikika aikesema kwa kejeli ndani ya Bunge Nchi hii Sasa inaitwa Tanzagiza kwa sababu ya Tatizo La Umeme. Akipigiwa makofi kwa kusema Umeme unakatika na ni wa mgao. Akaenda mbali kuyalaumu makampuni Kama symbion, IPTL Dowans, na kwamba pamoja na uwekezaji wao Tanesco wanapata hasara.
Raisi Magufuri Akasikia Kilio hiki. Kawatimua makampuni hayo, kawapa Nguvu Tanesco Sasa Unajengwa mradi utakao kuwa mwarobaini wa umeme. Leo Lisu anasema tunafanywa wajinga! Hapa anayewafanya wenzie Wajinga ni Nani?
Katika Bunge hilohilo Lissu huyo huyo alisema katika Usafiri wa anga ni Aibu kwa Tanzania Nchi yenye Mali Asili za kutosha kukosa ndege. Akasema ndege za Rwanda, Kenya na Ethiopia ndio zinatumika hapa kwetu. Akawadharau viongozi wetu kwa kuamua kujenga terminal 3 wakati hata ndege ndogo hawana. Leo anasema zilikuwepo Tangu ukoloni! Hivi Nani anayetufanya wajinga?
Ni Lisu huyu alisema Madini Yetu yana porwa, makaburu wamepewa vitalu, majizi yako wizara ya Madini. Lakini pia Ni Yeye Kama wanavyosema wao Ni Yeye ambaye aliamua kupingana na Raisi hadharani akiwatetea makaburu. Akakanyaga Elimu za wasomi wetu akiziita roport zile kwa Lugha ya Kigeni "professorial Rubbish". Akaenda mbali zaidi akasema tutashitakiwa, Kama haitoshi wakati wanapitisha seria mpya ya Udhibiti wa madini Yetu wabunge wa chama chake wote walipinga. Swali hapa ni je Tulishitakiwa? Je Ni kweli report zile hazikuwa na Tija kwa Taifa? Na Sasa Nani anayejeribu kutufanya wajinga?
Ni Yeye Lisu alisikika akisema Reli ya Kati tangu tumerithi kwa mkoloni mpaka Leo Ni ileile, imechakaa, mbovu na kila aina ya kejeri reli Ile emekarabatiwa, kigoma watu wanakwenda na Delux Moshi Tanga Leli inapitika Kama hii haitoshi inajengwa Reli ya Kisasa na Watanzania tunaona. Mtu mwenye Akili unawezaje kusema tunafanywa wajinga?
Ni Yeye Lisu aliye komaa na Mafisadi, hapa hakuwa na mchezo, alipaza sauti kwelikweli. Akamkatalia Raisi Kikwete hadharani kwamba Fedha za Tegeta Escrow si Mali ya watu ni fedha za Uma. Ni Nani asiyejua Jinsi alivyomtukana Lowasa na issue ya Richmond?Ni Yeye huyo huyo alimnadi Lowasa kuwa ni mtu Safi 2015. Tena ni Yeye Leo Mafisadi wanaposhughurikiwa anasema wanabambikiziwa kesi na kuporwa fedha.
Ni Yeye Lisu alisikika akisema wakina mama wanajifungulia njiani, wanalala chini mahospitalini, hakuna dawa, Msd wakapewa kila aina ya kejeli. Leo wakina mama wanajifungulia kwenye vituo vya Afya, usafiri uhakika tunaambiwa Raisi asitufanye wajinga.
Kwa kifupi Lisu haaminiki. Ni mtu kigeugeu na kwakweli Ni Yeye anayejifanya mjinga wakati anaelewa wazi jinsi Nchi hii inavyojengwa.
Ukweli anaujua Dodoma alivyoikuta sivyo alivyoiacha hili tu limemshangaza. Pamoja na ukweli kuwa hata kuhamia Dodoma Lisu na wenzia Walipiga kelele hawakutaka Leo hawataki kuondoka Dodoma.
Uwanja wa ndege chato Ni dhambi kuwepo? Chato hakuna watanzania? watu wa chato hawana hadhi ya kupanda ndege? Je chato mapato yatokanayo na uwanja huo ni Mali ya Magufuri?
Utasema chato kunanini? Wapo watu, wapo wafanyabihashara wa madini, wapo watumishi na Wana haki ya kupanda ndege na kuwa na uwanja. Acheni wivu.
Hifadhi mpya ya Buligi Ni Mali ya Magufuri? Watalii wa ndani na wanje wakienda hapo pesa anapewa Magufuri? Je uwepo wa uwanja na biashara hii Mpya ya Utalii haviendi sambamba? Makampuni ya Utalii yatakayowekeza huko na hotel zitakazojengwa huko zote zitakuwa Mali ya Magufuri? Vitu hivi havita wasaidia watanzania?
Ikiwa mapato ya hifadhi na uwanja wa ndege sio Mali ya Magufuri Ni Mali ya watanzania nongwa ya Nini kwa watu wa chato?
Umesema nyerere hakufanya hivyo? Lisu
anajua uwanja wa ndege Musoma ulijengwa mwaka Gani? Je ule wa Mungumu Serengeti? Huko sio Mara? Au hapakuwa Asili ya Nyerere. Ajibu kwa hoja wakatio huo Dodoma kilikuwa na uwanja? Mtwara kulikuwa na uwanja? Mbeya je?
Asitufanye wajinga