Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 46,375
- 66,435
Maneno aliyozungumza Lissu leo wakati anarudisha fomu ni mazito sana, anasema mtu aliyemleta Abdul kwake ampe pesa na akamwambia hata wengine wameshapewa pesa ndiye anagombea kuwa makamu mwenyekiti wa CHADEMA na anamuunga mkono Mbowe kuwa mwenyekiti!
Katika hili jambo kama ni kweli ni baya sana kwa CHADEMA kwa maana chama kinapoteza imani mbele ya umma. Kwa upande mwingine kama Lissu ni muongo basi hawezi kuaminiwa kuwa kiongozi tena na wenzake ndani ya CHADEMA maana ni dhahiri atakuwa ana nia mbaya sana dhidi ya chama na hii inamaanisha safari yake ya kugombea urais kupitia CHADEMA mwaka 2025 inaweza kuwa imefika mwisho.
Pia amekejeli mtindo wa mwenyekiti Mbowe ambao huwa anaombwa na wapambe kila uchaguzi kugombea.
Lissu asipokuwa mwenyekiti wa CHADEMA atajaribu kuanzisha chama kingine, ataelekea ACT au ataachana na siasa kabisa.