Ni wakati wa CHADEMA na ACT kuungana kupambana na mkoloni

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
4,434
9,438
Habari ya wakati huu ndugu zangu, karibuni tena kwenye mawazo ya kibeberu na Beberu J

Katika mizahania ya siasa Tz kuna vyama viwili vya upinzani ambavyo navyo unaweza sema vinapigania kuwa chama kikuu cha upinzani, CHADEMA ya bwana Mbowe na ACT wazalendo ya kwake Zitto, mifarakano ya hawa wawili imekuwa ganda la ndizi kwa chama cha mapinduzi CCM kuendelea kutawala bila shida maana hakuna anaedeal nae, wapinzani wamekuwa wakiparuana wao kwa wao muda wote badala ya kudeal na adui mkuu ambae ni CCM.

Katika ulimwengu wa kibepari na hata wa kisiasa inashauriwa usiweke visasi na wala usitoe hukumu ya kudumu, kwa maana kesho na kesho kutwa unaweza muhitaji yule uliemuwekea kisasi ili kufanya mambo yako yaende mbele kwa urahisi ( kwenye ubepari mambo lazima yaende tu sema yatachelewa).

Ndugu zetu ACT wana nguvu kubwa sana ya kujenga hoja zinazo "sound" vyema sana masikioni kwa watu wenye akili na hata watu wa kawaida, ila tatizo hawana mtaji wa watu, ndugu zangu CHADEMA wana mtaji mkubwa wa watu ila toka kutoka kwa Zitto na Slaa CHADEMA hawawez tena kujenga hoja nzito (huu ni ukweli), CHADEMA sasa hawana hoja kama chama, wanapingana wao kwa wao, hawana sera mbadala, wamegeuka pinga pinga na wazee wa siasa za matukio, wanazidi kupoteza imani kwa watu kwa sababu watu hawaelewi hawa wanasema nin na hoja yao ni nini?

Watasema wanapigania katiba mpya, ila bado hawajaweka wazi vipengele vyao na wala kutoa mapendekezo yao ya msingi (kama rasimu hiv) ya ile wanayotaka, humo humo CHADEMA wapo wanaosema turudi kwa wananchi tukaanze moja kutafuta maoni, wengine wanadai tumalizie ile ya ndugu Warrioba, hawana msimamo kama chama, leo Heche anasema hiki kisha Lema kesho anapinga kile kile kwa kifupi kwa sasa uwezo wa CHADEMA kihoja upo katika lowest possible level.

Hivyo kwa kuona pengo lililopo mimi kama bepari naona ipo haja kubwa sana kwa vyama viwili hivi kurudi mezani na kuungana pamoja na kuzika tofauti zao ( watu wanacheat kwenye ndoa wanasameheana 😂sembuse issue za siasa bwana tena za Tz).
Warudi mezani, waungane kumtoa CCM madarakani, hapa watakuwa na options mbili

#1. Waungane na kila mmoja abaki na identity ya chama chake( hapa iwe CHADEMA + ACT wazalendo) , hapa waweke sharing ya power plan nzuri, eg nani atachukua wizara ngapi, nani atatoa waziri mkuu. Mgawanyo wa majimbo utakuwaje,etc, na ni vyema hili waliweke mapema kwa manufaa ya yao wenyewe wasije tofautiana huko mbele

#2. Waungane waje na chama kimoja chenye nguvu kitakachopambana na CCM directly, i.e wavunje vyama vyao walivyonavyo sasa waje na chama kingine kimoja chenye kutumia rasilimali za ACT na CHADEMA ili kumuondoa CCM madarakani.

Kuendelea kupambana na CCM as separate identities hakutaleta manufaa yeyote kwa vyama hivi viwili, and truth be told itakuwa hasara kwa CHADEMA, mana naona wakipoteza watu kwenda either ACT na CCM,

Faida itakayotokana na muunganiko huo
#1. CHADEMA itafaidika na uwezo mkubwa wa ujengaji hoja na sera mbadala toka kwa ACT wazalendo, na hivyo kuonekana chama sahihi mbadala wa CCM

#2. ACT wazalendo wanaenda kunufaika kwa kupata platform au wafuasi wengi wa CHADEMA wa kuwahutubia na kuwaeleza sera zao na hivyo kura nyingi zaidi

#3. Umoja dhabiti wa kuitoa CCM madarakani, au hata kama wasipoitoa ila CCM cha moto watakiona 2025

#4. Kupunguziana maadui, katika siasa na maisha inabidi uhakikishe una maadui wachache as possible, kwa kuungana kwao watakuwa wamebaki na adui mmoja tu nae ni CCM, Na hivyo kuelekeza nguvu na rasilimali zote katika mapigano dhidi ya CCM.

Ila kama wapinzani wakienda kwa mafungu katika uchaguzi wa mwaka 2025 bas CCM anaenda pata kura zaidi ya 70% kama kawaida kisha CHADEMA anapata 10%+ na ACT wazalendo nae atapata hizo hizo ambazo zitawasaidia tu kupata ruzuku ya kula, hata kutengeneza umoja wa kambi nzito ya wabunge wa upinzani bungeni hawataweza.
Ni imani ya Beburu J kwa manufaa makubwa ya nchi yetu tunahitaji upinzani thabiti wenye kujenga hoja nzito zenye data za kutosha ili kuwakumbusha na kuwaongezea speed chama kilicho madarakani katika kuwaletea wananchi wake maendeleo.

Nasema ahsante kwa kusoma mawazo yangu, na nikukaribishe katika mjadala huu kwa mawazo yako,
Mpaka wakati mwingine tena, Ulikuwa nami Beberu J
Bye bye 👏

Nb. Blender hio hapo inauzwa kwa bei rafiki sana, Hit my Dm uweze fanyiwa free delivery
 

Attachments

  • 83E736D6-67FE-4663-A299-6EEEDEAB120A.jpeg
    83E736D6-67FE-4663-A299-6EEEDEAB120A.jpeg
    88.5 KB · Views: 4
Back
Top Bottom