Habari wanajamvi,
Tukiwa tunatazama michezo ya Olimpic nchini Ufaransa ni wakati wa kujitafakali na kupitia kwayo tukaja na mikakati ya muda mrefu kwenye michezo. Tumewekeza sana kwenye majengo ya shule na kuishia kutengeneza wanaomaliza shule na vyuo wakikosa ajira kwani mfumo wa elimu yetu kwa asilimia kubwa inatengeneza kijana atafute ajira na si kujiajiri hivyo kutengeneza utegemezi mkubwa.
Ombi langu kwa Mh. Rais, Waziri wa elimu na wizara nzima, Waziri wa michezo na utamaduni, Waziri wa Tamisemi, Wakuu wa mikoa na wilaya na wadau wote wa michezo na jamii nzima kwa ujumla wake.
Iwekwe sheria na lazima kila mkoa uwe na shule ya vipaji kwenye michezo na kila mkoa na mkuu wake wa mkoa awe na shule ya umahiri itakayomuwezesha mwanafunzi kuwa katika viwango vya kimataifa anayeweza kushindana na hata kuleta ushindi.
Hii italitangaza taifa ikiwa na pamoja na utalii hivyo kuongeza mapato.
Kila mwanamichezo atakuwa amejiajiri na kuajiri watu si chini ya 10. Uchumi wa mtu mmojammoja utapanda na hata kuziwezesha familia kutoka kwenye lindi la umaskini.
Michezo huleta furaha na mshikamano, taifa litafurahi na kushikamana.
Ubingwa kwa wanamichezo huongeza taifa kujiamini.
Hayo ni kwa uchache. Tunaona wenzetu Kenya, Uganda, Botswana, Ethiopia, SA, nchi za Afrika Magharibi na Kaskazini.
Ni wakati wa kuonyesha mapenzi ya dhati kwa michezo mingine kwa vitendo na isiwe tu mpira wa miguu ambao wachezaji wengi ni wa nchi za nje ndio wanaowika huku wakiwaacha wachezaji wa ndani wakiwa na viwango duni. Hii imefanya ushindani wa timu ya taifa kuwa hafifu kimataifa.
Ni wakati wa taifa kuamka na kuendelea hasa kwenye wakati huu ambao Mh. Rais anapenda ubunifu na kutangaza taifa kimataifa.
Nawasilisha.