1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,000
- 9,245
Siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi kubwa sana la watu kuuana kutokana na wivu wa kimapenzi. Jambo hili lilianza kusikika kidogo kidogo lakini kwa sasa limekua likitokea kila siku. Hali imekua ni mbaya sana kila kukicha stori kubwa mitaani na kwenye mitandao ni masuala ya vifo au migogoro ya kimapenzi.
Jamii katika suala hili imegawanyika mara mbili; kuna wanaounga mkono wale wanaojichukulia sheria mkononi na wengine wanawalaumu wale wanaochukua sheria mikononi. Yote kwa yote kila upande ukiusikiliza kwa makini utaona kuwa una sababu zenye mashiko.
Akiuawa mwanaume, wanawake na baadhi ya wanaume hasa wale ambao wamewahi kuguswa na kadhia inayotokana na usaliti, basi kwa nguvu kubwa wanashangilia na kusema wanaume wamezidi, wanaume hawajatulia, wanaume wameizidi umalaya na tamaa acha achomwe moto au amwagiwe maji ya moto.
Wakati huo huo wanaume wengi Wanabaki kulaani tukio la mwanaume mwenzao kuuawa kwa wivu wa kimapenzi. Lakini pia hali inakua hivyo hivyo pale anapouawa mwanamke kwa wivu wa mapenzi.
Hapo kwa kweli wanaolaani wanakuwa ni wengi zaidi, kwani wanawake wanaalaani kwa nguvu kubwa na wanaume pia na watoto pia wanapata madhara makubwa kwa kupoteza mama . Hapa pia kuna kundi dogo ambalo nalo linaunga mkono kuuawa kwa mwanamke anayefanya usaliti kwenye ndoa yake.
Sasa jamii imebaki njia panda, serikali nayo imekaa kimya na kulichukulia kama suala la kibinafsi tu na sasa wanasiasa na wasomi wetu wanalihusisha na wivu unaotokana mapenzi na magonjwa ya akili tu na msongo wa mawazo. Viongozi wa dini wanalihusisha na shetani. Jamii na mila zetu za Kiafrika inalihusisha na kupotea kwa maadili ya Mwafrika.
Sasa hebu tuangalie:
Je, hili suala la mauaji ya kila siku la wivu wa kimapenzi hasa kwa wanandoa linatokana na Ugonjwa wa akili, stress na wivu uliyopitiliza hivyo dawa yake ni kutafuta ushauri nasaha na matibabu ya kitaalamu? Je ,ni sawa Kwa serikali kuja na majibu mepesi kama hayo huku jamii ikiendelea kuona Kasina kubwa ya usaliti kwenye ndoa na watu kuuna na watoto kubaki yatima siku Hadi siku huku?
Hebu nitoe mfano kule Kenya Leo hii Kuna Rais mpya anaakili timamu na Hana msongo wa Mawazo Wala Hana wivu uliopitiliza; Je, anaweza au system inaweza kuruhusu Mtu yeyote kuanza kuchepuka na mke wake kisa eti wamekubaliana wenyewe na pia ni suala la madai TU na akiona Vipi Bora waachane TU Kwa wema?
Hali kadhali Tanzania kuna wakubwa wa Serikali wenye ndoa na wake zao au waume zao;
Je, Yule Bwana Mkubwa atakua mvumilivu au atakubali kuona mkewe anatembea na mfanyakazi wa ofisi yake au jirani yake na akapewa Taarifa na akafanikiwa kumjua mwizi wake na kuchukulia poa tu eti yeye sio mgonjwa wa akili na Hana stress hivyo atatoa TU Talaka na kumpa Sasa ruhusa kamili huyo mgoni wake au mchepuko wa mkewe wakajinafasi na kumwacha yeye kama Waziri mkubwa kubaki Hana mke na watoto wakose nyumba kamili ya kukaa na kuwaona wazazi wao? Hii haikubaliki Mbinguni na Duniani. Adhabu ya mzinifu ni lazima iwe Kali sana kuepusha haya yanayotokea.
Au mfano Jaji mkuu au kwanasharia mkuu wa Serikali ghafla apate Taarifa kuwa Kuna mtu anatembea na mke wake. Sidhani kuwa atapuuza na kujifanya kuwa yeye anaakili timamu na Hana stress Kwa vyovyote atafuatilia akijua ukweli na akamuonya mgoni waki kirafiki lakini akaendelea huku mkewe akiwa anaonyesha dharau kuwa kama Vipi tuachane nikale Bata na mchepuko wangu; Je,atakubali kutoa Talaka na kumwacha mkewe na furaha Kwa mwizi wake huku yeye akibaki peke yake na watoto wakiwa hawana uelekeo Maalumu wa kifamilia na malezi ya baba na mama kisa mama ameendekeza tamaa zake za kimwili na baba Mwingine ambaye naye ana mke wake na watoto ?
Au mkuu wa majeshi asikie mke awe anachepuka na mlinzi wa getini na afanye uchunguzi agundue ni kweli au awafumanie kabisa ? Je, atachukua karatasi na kuandika barua ya Talaka badala ya kuchukua bastola na kumchakaza mlinzi risasi ya kichwa.?
Au mfano Daktari wa magonjwa ya akili mwenye akili timamu kabisa asikie kuwa mkewe ambaye ni nesi kweye Hospitali hiyo kuwa anatembea/anachepuka na mtu ambaye hua anakuja kutibiwa kwake au kupata ushauri kwake? Je, huyo Daktari ataweza kumhudumia vizuri huyo mteja wake kisa TU Hana Ugonjwa wa akili au stress au wivu Kwa mkewe? Bila shaka hataweza kumhudumia?
Hapo nimetoa TU mifano Kwa watu walioko juu kwenye serikali na vyombo vyake lakini najua wazi kuwa walioko juu familia zao zinalindwa sana na haziwezi kufikiwa kirahisi na kila mwenye tamaa ya ngono . Na pia walioko juu wao Wana Mapesa Mengi wanasafari nyingi wakiwa hata na michepuko mitatu minne Kwa pamoja .
Hawawazi sana wake zao mana mara nyingine wameshawakinai. Lakini Kwa mtu wa kawaida mwenye kipato Cha chini na ambaye anapambana kumhudumia familia yake akiwemo mke wake na nimwaminifu Kwa mkewe au Mumewe halafu anamfumania mkewe au Mumewe ambaye ana ndoa na waliapa kuishi Kwa uaminifu inakua ni mtihani sana kumwacha mwizi wake salama.
Hukuna shujaa anayekimbia vita. Na siku zote mashujaa ni wale waliokufa wakipigania mataifa yao . Kuna wakati unakuta mchepuko unamfokea na kumtishia mwenye mke au mume halali wa ndoa na mwenza wake akiulizwa anasema wewe una wivu wa kijinga ? Kisa labda mchepuko unajiona una sura zaidi au pesa zaidi au cheo kikubwa. Hapo na majibu kama hayo jamii inategemea Nini zaidi ya mauaji kuongezeka!?
Siku hizi wengi wanajificha kwenye simu eti ooh simu ya mume wake anaiangalia ya Nini? Ukiona ameiangalia basi ujue Kuna mahali anaona mabadiliko ,hakuna mtu anayeweza kuficha hisia zake Moja Kwa Moja labda kama Mumewe au mkewe amelogwa ili awe taahira hafuatiilii chochote Cha mke wake.
Kwenye mauaji haya ya wanandoa wahanga zaidi ni wale watu wanyonge na sio wakubwa. Hawa wanyonge ambao Kwa Sasa kulingana na ugumu wa maisha ndoa zao zinaingilika kirahisi sana ; Je, ndao zao na watoto wao wanalindwaje dhidi ya wanaume na Wanawake Wazinzi wasiojali ndoa na hatima ya watoto wa wenzao? Ni kweli kuwa Kwa Sasa suala la kuchepuka Kwa Wanawake limekua kama mashindano Kati ya walioko kwenye ndoa na walioko nje ya Ndoa. Wanawake wanahujumiana wenyewe Kwa wenyewe.
Yani tamaa imeongezeka sana kutokana na mitandao mtu yupo Mwanza anamtongoza Mwanamke aliyeko Dar es salaam kirahisi sana . Hali hii ni janga kubwa sana siku zinavyoendelea Kwa sababu hakuna Tena heshima ya Ndoa . Ndoa inaonekana kama ndoano na Wazinzi wanafanya makusudi kuzini na waume na wake za watu ili kuzidi kuvuruga ndoa na kuwafanya wanaume na Wanawake wawe wa kila mtu bila utaratibu.
Ikitokea Ugonjwa wa kuambikiza kama ilivyokuwa AIDS miaka ya 1980 kuelekea 1990 mpaka 2020 Watanzania wataisha.
Sasa hivi hata biashara ya Kondom Haina soko Tena mana virusi vimshafubaa na hakuna wagonjwa Tena. Woga haupo Tena hasa Kwa wanandoa ndio Hali ni mbaya zaidi. Hata hivyo vifo vimegeukia vya kuuana badala ya magonjwa Sasa ni kuuna Kwa kukataa mapanga na kumwagiana maji ya moto na risasi.
Watawala walioko juu na wanasiasa waliangalie jambo hili la Wana ndoa kuuana Kwa jicho la tatu. Hali ni mbaya kwenye ndoa nyingi. Wanaume wengi Kwa Sasa wanaugulia ndani hasa wa kipato Cha chini na Vijana .
Siku hizi hakuna kijana asiye na pesa anayeweza kuwa na mchumba mrembo na wakafikia ndoa. Hata wakiona wanaishia kuuana. Yote ni Kwa sababu hakuna SHERIA Kali ya kulinda kizazi Cha kesho na maadili.
Hivi Hawa wa maisha ya chini hasa wa kiume Watakuja kuwa na familia yenye mama,baba na watoto kama serikali itaendelea kukaa kimya kwenye hili tatizo la wanandoa kuuana?
SHERIA ya Sasa ya Ndoa imebaki kuwalinda Wazinzi wenye pesa huku maskini wakiishia makaburini au gerezani au kuishi na stress na kufa kabla ya wakati. Mzinzi Mwenye pesa anaweza akamchukua mke wa mtu bila woga mana anajua hata akifumaniwa hakuna SHERIA Kali ya kumbana zaidi ya kesi ya madai ambayo maskini hawezi kuifungua. Lakini pia akipewa vitisho anatoa pesa nyingi na kitakatisha fumanizi lake.
Maskini mzinzi akifumaniwa anauawa au kulawitiwa mana Hana Cha kulipa. Hapa maskini ndiye anayeumizwa na SHERIA hii ya Ndoa ambayo inatoa fursa Kwa Wazinzi wenye fedha kujitwalia Wanawake mpaka kwenye ndoa za watu. Maskini anapoona anaporwa mpaka mke wake au mume wake ambaye kwenye kiapo Chao Cha ndoa aliapo kuwa faraja kwake basi anaamua kuua. Hapo hakuna namna mana Hana wa kumkimbilia ili apate msaada wa kulipiwa kisasi chake . Kazi ya serikali ni kulipa kisasi badala ya mdhulumiwa Vinginevyo mdhulumiwa analipa Mwenyewe.
Serikali inawatupia mzigo viongozi wa kidini kuwa watoe Elimu ya kiroho zaidi lakini ukweli ni kwamba nao pia ni ama ni wahanga au vikwazo kutokana na ukweli kuwa wapo pia viongozi wa dini Wazinzi wanaovuruga ndoa za watu.
Wanafanya makusudi mana hakuna SHERIA Kali ya kulinda ndoa za watu.
NINI CHA KUFANYA:-
Ni wakati Sasa wa kubadili SHERIA ya Ndoa ili Suala la Kuzini na Mke au mume wa mtu liwe ni jinai Moja Kwa Moja hasa inapotokea Kuna ushahidi wa kutosha. Yaani pawe na ufuatilliaji mpaka wa kimtandaoa mana mitandao inetumika sana kwenye kuvuruga ndoa za watu. Iwe suala la kushea simu Kwa wanandoa wenye ndoa ya mke mmoja liwe ni wazi au kukubaliana lakini iwe ni haki ya Mwana ndoa ya mke mmoja kuomba kufuatilia mienendo ya mwenza wake na kufungua kesi ya Jinai ili kumbaini anayevuruga ndoa yake na kufikshwa mahakamani na kupewa kifungo.
Lengo ni kulinda ndoa maana mtu anapoamua kuoa mke mmoja na mume mmoja basi amefanya hivyo Kwa taratibu za kisheria ili awe na familia yenye ustawi. Sasa tukiwaachia watu wakae bila kubanwa na SHERIA Hakika miaka ishirini ijayo ndoa za mashoga zitakua nyingi sana mana watoto wengi watakosa Bora. Lakini pia kuwaacha watu wenye stress na vinyongo kwenye jamii ni hatari Kwa amani ya nchi.
Mtu ambaye alikua anampenda mke wake au mume wake halafu ghafla akajikuta ameachana na mke wake au mume wake Kwa sababu TU Kuna Mzinzi mmoja mwenye pesa au anayejifanya yeye ni kidume au kipisi kali Cha kutembea na wake au waume za watu, rahisi Sana mtu kama huyo kufanya tukio baya au uhalifu mbaya .
Hata ugaidi hua mara nyingi unatokana na masuala ya Ndoa. Ukiangalia mfano suala la mahakama ya Kadhi nchini Tanzania lilikua hasa linalenga masuala ya Ndoa.
Waliponyimwa paliibuka chuki za chini Kwa chini na hata kuibuka Kwa vitendo vya kigaidi. Kijana mfano alikua na mchumba wake mzuri halafu anatokea Mzee wa miaka 60 mwenye pesa na mke wake na watoto na wajukuu anakuja anamrubuni mchumba wa huyo kijana na kusababisha kijana anashidwa kumuoa Tena. Bila shaka kijana huyo anakua na hasira na kinyongo na Hana pa kwenda ili kisasi chake kilipwe badala yake anaambiwa aende akafungue kesi madia mahakamani ili alipwe fidia. Fidia ya Nini wakati shida yake sio pesa ni mke? Kijana kama huyu ni rahisi kulipa kisasi au kuwa na roho mbaya na hata kujiunga na ugaidi.
Hata utendaji kwenye maofisi ya umma unashuka Kwa sababu ya migogoro ya Ndoa. Watu wanaingia kazini na stress wanashindwa kutoa huduma nzuri.
Watu wanafanya ufisadi ili wawe na fedha nyingi mana wanajua ndoa za watu maskini Kwa Sasa hazina Tena uaminifu na uvumilivu. Wamama wanakopa vikoba pesa wanahonga Vijana matokeo yake Wanabaki na madeni.
Kwa Wanasiasa wenye migogoro ya Ndoa wanaweza kuhamasisha maandamano yaliyojaa chuki na hata kuvuruga amani ya nchi.
Serikali ije na MUSWADA WA kurekebisha SHERIA ya Ndoa ili hata waislam wenye wake wanne wote watambulike kwenye haki zao Kwa watumishi wa umma.
Mtu yeyote mwenye ndoa ya mke mmoja akifumaniwa na au akivuriga ndoa ya mtu afungwe gerezani.
Mwenye ndoa ya wake wengi pia akifumaniwa afungwe gerezani na faini juu mana alikua na fursa ya kuoa mke Mwingine ili kukidhi tamaa zake. Ifikie mahali tujenge jamii iliyostarabika sio kuuana Kwa sababu ya kuishi kama nguruwe na mbwa na Kuku. Hii itarudisha heshima ya Ndoa na kulinda watoto na pia kupunguza mauaji. Na pia itahamasisha Vijana kuoa na kuolewa mana watakosa urahisi wanaoupata ngono kama ilivyo Sasa. Kijana au Binti atajua akitembea na mume au mke wa mtu kifungo kinamsubiri.
Lakini pia suala la kupima DNA Kwa wanandoa wapya liwe ni lazima mana watoto wengi wanaozaliwa sio wa baba wa kwenye ndoa na wamezaliwa sio Kwa sababu ya kukosa uzazi Bali kwa sababu ya kuchepuka na wengine kuapa kuwapa michepuko yao zawadi ya kumzalia mtoto. Hii ni hatari hasa mwanaume anapojua anawaza jinsi Nmanavyohangaika na maisha kumbe baadhi ya watoto sio wake.
Hapa kuzaa nje ya Ndoa libaki kama makubaliano au asiyeweza kukaa na mwenza asiyezaa basi aombe Talaka au wakapandikize mtoto Kwa kuridhiana sio kusalitiana.
Kwa upande wa Viongozi wa dini waache mahubiri ya kugemea upande mmoja na kusema kuwa wanaume ndio wanaochepuka , Hali inayowafanya Wanawake kuona kuwa wao hawaonekani na hivyo wanaendelea kuchepuka kwa kujificha na wakiona wanabainika wanajificha kwenye mgongo wa viongozi wa dini wakati ukweli ni kwamba Wana ndoa wa kike na kiume ndio wanaoongoza kuchepuka.
Lakini pia serikali iangalie zaidi SHERIA zinazoruhusu ndoa ya wake wengi ipewe kipao mbele mana inaonekana kuwa Wanawake wapenda kuchangia wanaume ndio maana wengi wanapenda waume za watu.
Na wanaume wengi HAWAWEZI kuwa na mke mmoja hivyo waoe wake wengi sio kuvuruga ndoa za watu.
Haiwezekani mwizi aibe Kuku wa Kienyeji anayeishi Kwa kula mchwa maporini na majalani na Hana gharama yoyote lakini akiibiwa basi mwizi anafungwa miaka sana lakini mtu anaingia na kuiba mke au mume wa mtu anayemgharamikia kuanzia mahari na matunzo na kulea watoto halafu eti iwe ni kesi ya madai TU au mtu avumilie TU. Lakini akimkuta maskini anaiba mbuzi wake anaweza kumpigia mshale au kumpeleka Polisi na akafungwa miaka sana. Kuku mmoja Tena kutokana na umaskini TU haiwezi kuwa ni kosa kubwa kuliko kutenganisha mtu na familia yake na kuacha watoto WAKITESEKA. Wote Hawa ni Wahalifu mana wanavunja ustawi wa jamii na kuleta chuki kwenye jamii.
Serikali na Bunge wasipochukua hatua Kwa sababu tu wao hawaguswi sana kadhia hii ya kuachiwa watoto yatima kutokana na mauaji ya wivu wa mapenzi wajue ipo siku Watajua kuwa walitunga SHERIA ya Ndoa ya mazingira ya Ulaya bila kuangalia mazingira ya kiafrika.