Ni vigumu sana kumng'oa Mkoloni Mweusi kuliko ilivyokuwa kwa Mkoloni Mweupe

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
2,217
3,820
Asalaam aleykum,

Ama baada ya salamu hizo, rejea kichwa cha habari, chahusika.

Uhuru ni kitu muhimu ambacho kila mmoja anakitamani. Lakini kwa bahati mbaya sana katika historia ya binadamu, imekuwa ni hulka ya baadhi ya watu furaha yao kukamilishwa kwa kuwanyonya/kuwakandamiza wenzao.

Hili linadhihirishwa na mifumo ya kinyonyaji ambayo imekuwepo hadi kufikia kipindi cha ukoloni. Ukoloni ni ile hali ya Taifa moja kulikalia Taifa jingine kimabavu.

Tumeona katika historia kwamba asilimia kubwa ya nchi duniani (hasa hasa zile za Afrika, Asia, Amerika Kusini na Kasikazini) zilipitia Kadhia hii ya ukoloni.

Asilimia kubwa ya nchi hizo tayari zilishapata uhuru wao toka kwa mkoloni mweupe lakini kwa bahati mbaya, matarajio makubwa ambayo tulikuwa nayo kabla ya kupata uhuru, yanazidi kufifia kwa sababu kinachoonekana ni kama kilichofanyika ni kubadilisha tu rangi ya wakoloni, yaani badala ya kutawaliwa na wazungu, kwa sasa tunatawaliwa na weusi wenzetu ambao kwa maoni yangu ni aina mbaya zaidi ya ukoloni kuliko ile iliyokuwepo kabla.

Kwa bahati mbaya sana nchi nyingi za Kiafrika, zina matatizo na changamoto zinazofanana.

Mungu atusaidie ili tuweze kuondokana na aina hii ya ukoloni pamoja na ugumu wake lakini nina amini iko siku itawezekana.

Tunahitaji rasilimali za nchi, ziwanufaishe wananchi wote kwa ujumla katika kuwaboreshea miundombinu na huduma zote za kijamii.

Tunahitaji nafasi za kazi serikalini zitolewe kwa uwiano sawa na siyo kuhodhiwa na familia/koo chache tu.

Tunahitaji wafanyabiashara wadogo kwa wakubwa wafanye biashara zao pasipo bughudha.

Tunahitaji uwazi na uadilifu katika kuwachagua viongozi wetu kuanzia ngazi za chini kabisa hadi ngazi ya Rais (Uchaguzi huru na wa haki).

Tunahitaji uhuru katika kutoa maoni pasipo hofu yoyote.

Tunahitaji viongozi wafanye kile ambacho raia wanakitaka kwa sababu hata hivyo wapo pale kwa ajili ya kutuwakilisha na kwa maslahi yetu.

Tunahitaji uonevu na dhuluma za kila aina ziondolewe katika jamii zetu.

Tunahitaji wala rushwa na wabadhilifu wote wawajibishwe pasipo kuonewa haya.

N.k
 
Kama huyu mkoloni wetu CCM, sijui atatoka madarakani kwa njia gani!! Maana amejiwekea mizizi yake kila sehemu.
 
Back
Top Bottom