Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu hoja hii aliisema sana tena kisayansi sayansi ya siasa kuhusu uwakilishi wa watu:
Tundu Lissu asisitiza Mabonde, milima hayapigi kura bali ni watu na kuwa kura moja ya Dar es Salaam iwe sawa na kura moja Bukoba, Mbeya n.k na kurejea takwimu za Tume ya Uchaguzi :
bali watu Mtwara wapiga kura 930,000 majimba bunge 10, huku Dar es Salaam watu 3,000,000 majimbo 10, Mbeya 1,000,000 majimbo 7.
Majimbo-bunge lazima yawe na idadi sawa ya wapiga kura ili kura zote ziwe na uzito unaolingana. Mfawanyo wa maeneo / jimbo bunge lazima yawe na idadi sawa
Kutoka maktaba :
SENSA NA DEMOKRASIA
Taarifa za idadi ya watu husaidia katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimali;
Taarifa za msingi za hali ya kidemografia, kijamii na kiuchumi za idadi ya watu na makazi za mipango katika ngazi zote;
Kigawio katika kukokotoa viashiria vingine mfano Pato la mtu mmoja mmoja, Pato la Taifa, Ajira na ukosefu wa Ajira na kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi;
Taarifa itakayowezesha serikali kujua ongezeko la idadi ya watu, kwa mgawanyo na viashiria vingine, ambavyo ni muhimu kwa usimamizi wa mazingira; na
Msingi wa utawala bora na ujumuishaji wa demokrasia. Takwimu sahihi za Sensa zinahitajika kwa ajili ya ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa ufanisi, kurekebisha mipaka ya kiutawala katika serikali za mitaa.
Source :
Hii ndiyo tofauti ya Sensa ya 2022 na zilizopita