Ni upi mtazamo wako wa sasa hasa kufeli kwa kundi hili la vijana, je ni serikari ndo inayostahiki lawama ama ni uzembe tu wa vijana kubweteka?

Sasa serikali kipaumbele chake ni kufanya ziara za nje ya nchi na watu kama mwijaku, baba levo, steve nyerere, harmonize etc. Hao ndio aina ya vijana ambao serikali inaona wanahitaji kushikwa mkono, kwa hali kama hiyo vijana wasomi hawaoni tena thamani ya elimu yao na hata waliopo vyuoni wanaona kama wanapoteza muda tu matokeo yake ni kuwa na kundi kubwa la vijana wa hovyo wasio fit kwenye mfumo rasmi wa ajira.

Kuna mtu atauliza kwa nini wasijiajiri? Huyo usimjibu, mpuuze upumbavu wake uko viwango vya juu sana
 
Kuna mtu atauliza kwa nini wasijiajiri? Huyo mpuuze upumbavu wake uko viwango vya juu sana
Aisee umezungumza jambo moja zito mno, big up.
 
Wote wanastahili lawama, huwezi sema lawama zote kwa serikali au zote kwa vijana,

Kuna vijana wengi tu wanatoboa, kina Niffer na wenzake,
Je hao wana serikali yao ? M naona kikubwa vijana tupambane, iwe shambani, uwingani au vipi,

Mana kiukweli serikali haina uwezo tena wa kuajiri watu wote, huo ndio ukweli mchungu
 
10% ya fedha za kila Halmashauri zingewekezwa kwa vijana ingekuwa dili,tatizo fedha zenyewe zinapigwa na wajanja. Kuna vijana wamesoma vyuo vya kilimo,ufundi,teknolojia,uvuvi....hawa wote wanahitaji mikopo ili wajiajiri na kibaya zaidi Taasisi nyingi za mikopo hazitoi mikopo kwa anayeanza biashara ila anayeendeleza.Cha msingi tuache kuzaa hovyo tuzae kutegemeana na uchumi aliokuwa nao mtu,pia tuwafundishe vijana kazi za mikono za uzalishaji tangu wakiwa wadogo kama vile kufuga kuku,kulima bustani na matunda,kuoka na kutengeneza vitafunwa,kutengeneza mazulia n.k
 
Sasa serikali kipaumbele chake ni kufanya ziara za nje ya nchi na watu kama mwijaku, baba levo, steve nyerere, harmonize etc. Hao ndio aina ya vijana ambao serikali inaona wanahitaji kushikwa mkono, kwa hali kama hiyo vijana wasomi hawaoni tena thamani ya elimu yao na hata waliopo vyuoni wanaona kama wanapoteza muda tu matokeo yake ni kuwa na kundi kubwa la vijana wa hovyo wasio fit kwenye mfumo rasmi wa ajira.

Kuna mtu atauliza kwa nini wasijiajiri? Huyo usimjibu, mpuuze upumbavu wake uko viwango vya juu sana
Kweli kabisa

Ova
 
Na hizo fedha zenyewe za halmashauri zikitengwa kwa ajili ya vijana, yatatokea ya kutokea. Aidha zitakuwa zinatolewa kwa undugu au wanaojiita na kujifanya wajanja watazipiga humohumo juu kwa juu.

Tanzania inasikitisha sana!
 
pia tuwafundishe vijana kazi za mikono za uzalishaji tangu wakiwa wadogo kama vile kufuga kuku,kulima bustani na matunda,kuoka na kutengeneza vitafunwa,kutengeneza mazulia n.k
Dunia imeondoka kwenye manual labour sisi ndio tunataka tukomae huko?? Vipaumbele vyetu vinasikitisha sana, ndio maana hata ulimwengu huwa unatudharau sana, ukiwa na taifa la watu wenye 'akili' na 'maarifa' ni lazima watu hao watatafuta njia nyepesi zaidi za kukabiliana na changamoto zao na hapo ndio inazaliwa dhana ya uvumbuzi chanya. Ila ni ngumu sana kuyafikia hayo kwa sababu dira ya taifa imeishaonyesha muelekeo wake ni 'uchawa'.

Taifa linaongozwa na serikali, serikali inaundwa na 'chama', chama kinapokea hoja za wananchi kupitia wawakilishi, wawakilishi wenyewe ndio hawa kina babu tale na msukuma ambao wao wana pesa na hawana elimu, maarifa yao yamejikita kwenye u 'mission town' na wala hawaoni thamani ya kuwa na wasomi maana hata wasomi walioko humo bungeni akili zao ni za ki hoe hae mwisho wa siku wanabaki kualika kina Liquid Konki Master na kutambua michango yao kwenye jamii kama mawakala wa kupumbaza watanzania, mwisho wa siku tunabaki kwenye circle ile ile. Garbage in Garbage out. Life goes on
 
Vijana wengi wa kitanzania wasomi na wasio wasomi wengi wao wamekuwa wakilalamika aina ya maisha ya sasa yalivyo magumu kwako.

je sababu ni serikali kutowawekea mazingira wezeshi au ni kubweteka kwako?
NANI ANASTAHIKI LAWAMA?
Naipa serikali maana wameshindwa kubadilisha mfumo wa elimu maana vijana ambao hawajasoma wana vipaji vizuri 2 vya kuwainua lakini ndo hivyo
 
Sasa serikali kipaumbele chake ni kufanya ziara za nje ya nchi na watu kama mwijaku, baba levo, steve nyerere, harmonize etc. Hao ndio aina ya vijana ambao serikali inaona wanahitaji kushikwa mkono, kwa hali kama hiyo vijana wasomi hawaoni tena thamani ya elimu yao na hata waliopo vyuoni wanaona kama wanapoteza muda tu matokeo yake ni kuwa na kundi kubwa la vijana wa hovyo wasio fit kwenye mfumo rasmi wa ajira.

Kuna mtu atauliza kwa nini wasijiajiri? Huyo usimjibu, mpuuze upumbavu wake uko viwango vya juu sana
Paragraph ya mwisho umetishaa sanaa!!
 
Wote wanastahili lawama, huwezi sema lawama zote kwa serikali au zote kwa vijana,

Kuna vijana wengi tu wanatoboa, kina Niffer na wenzake,
Je hao wana serikali yao ? M naona kikubwa vijana tupambane, iwe shambani, uwingani au vipi,

Mana kiukweli serikali haina uwezo tena wa kuajiri watu wote, huo ndio ukweli mchungu
Kwahiyo Niffer ndo katoboa? Je unajua njia aliyotumia kutoboa? Na hao wenzake ni wepii? Em wataje kwan.
 
Sasa serikali kipaumbele chake ni kufanya ziara za nje ya nchi na watu kama mwijaku, baba levo, steve nyerere, harmonize etc. Hao ndio aina ya vijana ambao serikali inaona wanahitaji kushikwa mkono, kwa hali kama hiyo vijana wasomi hawaoni tena thamani ya elimu yao na hata waliopo vyuoni wanaona kama wanapoteza muda tu matokeo yake ni kuwa na kundi kubwa la vijana wa hovyo wasio fit kwenye mfumo rasmi wa ajira.

Kuna mtu atauliza kwa nini wasijiajiri? Huyo usimjibu, mpuuze upumbavu wake uko viwango vya juu sana
Mimi naweza kuwa na double standard juu ya kufell maisha kwa vijana wetu! Hii trend ya kufell imeishapigiwa kelele miaka 30 hadi sasa tangu "cost sharing" ya vyuo vikuu wanafunzi walipoondolewa kusomeshwa bure badala yake wakaanza kukopeshwa tangu 1994! Kilichopelekea hali ya kulazimisha kuondoa elimu bure ya vyuo ni kubweteka kwa wanavyuo badala ya kunoa brain zao kuleta maendeleo na tija kwa nchi na kwao binafsi wakawa wanajiingiza katika vurugu na siasa hata kupelekea kumtusi mkuu wa nchi "panch" kipindi cha Rais Mwinyi kupelekea kufukuza kwa kukifunga UDSM. Baada ya hapo ilitakiwa vijana washtuke kuwa kuna "consequences" kama utapata fursa ya kusoma alafu usizingatie masomo itakula kwako! Naona hadi sasa vijana hawajajitambua maana wakienda vyuo wakaanza kushika hela za "boom" wanaanza kuweka kwa vitendo "pata hela tujue tabia yako" kwa kujiingiza kwenye ngono na ulevi na tabia za tamaa za mali za kumiliki simu kali za iPhone na mambo kama hayo. Mwisho wa siku wengi wanamaliza bila maarifa na kujazana mitaani wakilia "tuajiri". Tukiwaambia watuonyeshe walichokipata vyuoni hawana zaidi ya suruali mlegezo kwa vijana na vibinti kupost picha kwenye mitandao ya kijamii! ACHA WAVUNE WALICHOKIPANDA!
 
Kilichopelekea hali ya kulazimisha kuondoa elimu bure ya vyuo ni kubweteka kwa wanavyuo badala ya kunoa brain zao kuleta maendeleo na tija kwa nchi na kwao binafsi wakawa wanajiingiza katika vurugu na siasa hata kupelekea kumtusi mkuu wa nchi "panch" kipindi cha Rais Mwinyi kupelekea kufukuza kwa kukifunga UDSM.
Kumtukana Rais maana yake ni nini?? au kuwa na mtizamo tofauti na alio nao rais ni dhambi?? Hapo Cuba tu Elimu ya chuo kikuu ni bure je inamaanisha wanafunzi wote wanakubaliana na Sera za Rais wa Cuba?? Huko nchini marekani Elimu ya Chuo ni ya kulipia na ni gharama sana Je hali hiyo imepelekea wasomi wa vyuo wa marekani kuwa 'YES-MAN'?? Afrika ni lini tutaacha kuua Mende kwa nyundo?? Kwa nini tunaona hawa viongozi mfano Rais ni kama miungu isiyo stahili kuhojiwa wala kukosolewa??
Baada ya hapo ilitakiwa vijana washtuke kuwa kuna "consequences" kama utapata fursa ya kusoma alafu usizingatie masomo itakula kwako! Naona hadi sasa vijana hawajajitambua maana wakienda vyuo wakaanza kushika hela za "boom" wanaanza kuweka kwa vitendo "pata hela tujue tabia yako" kwa kujiingiza kwenye ngono na ulevi
Ngono na ulevi kwa wana vyuo haijaanza leo wala jana, hii ni tangu enzi za kina nyerere huko, kumbuka umri wa chuo ndio vijana wengi wana balehe, mimi binafsi ni chapombe mzuri tu tangu nikiwa kidato cha tano lakini masomo yalikuwa na nafasi yake na pombe (viroba + banana) zilikuwa na nafasi yake.
na tabia za tamaa za mali za kumiliki simu kali za iPhone na mambo kama hayo. Mwisho wa siku wengi wanamaliza bila maarifa na kujazana mitaani wakilia "tuajiri". Tukiwaambia watuonyeshe walichokipata vyuoni hawana zaidi ya suruali mlegezo kwa vijana na vibinti kupost picha kwenye mitandao ya kijamii! ACHA WAVUNE WALICHOKIPANDA!
Tamaa ya mali ni tabia ya mtu binafsi. Wengi wanazuga zuga huko vyuoni kwa sababu muelekeo wa nchi pamoja na wahamasishaji wanao onekana kuungwa mkono na serikali ni wale wanaosema elimu haina manufaa yoyote katika kufikia ndoto zako. mfano mzuri ni mwijaku.
 
Tusubiri mitaji
 
Attachments

  • 20231031_184651.jpg
    20231031_184651.jpg
    380.4 KB · Views: 2
Tatizo linaanza na serikali kuwafanya vijana kuwa ni watu wa kuwaza Mpira 25/7

Kuwapa elimu mbovu

Kuhusu vijana -vijana hawafundishiki wao ni mitungi mineli na milupo.

Kuhusu vijana -wapo vijana smart na wachache wanajitambua na wamefanikiwa vizuri.
 
Wote wanastahili lawama, huwezi sema lawama zote kwa serikali au zote kwa vijana,

Kuna vijana wengi tu wanatoboa, kina Niffer na wenzake,
Je hao wana serikali yao ? M naona kikubwa vijana tupambane, iwe shambani, uwingani au vipi,

Mana kiukweli serikali haina uwezo tena wa kuajiri watu wote, huo ndio ukweli mchungu
Wewe huna akili kichwani, unawezaje kumtolea sample mwanamke mwenye biashara mbili?

Yani kama vijana wenyewe ndio wana skili kama hizi ni bure kabisa.
 
Back
Top Bottom