wastani kwa idadi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 340
- 882
To cut the story short watoto tupo sita rika ni 30 hadi 40, wengi tayari tunaishi mikoa mingine sababu tumeajiriwa serikalini
Mzee alifariki 2015, Bi Mkubwa 2023
Pale mjini kuna nyumba mbili, ya kwanza ni ya kitambo tuliyoikuta na kuishi nao wazazi, nyingine tuliijenga watoto miaka ya 2013 lakini mama aliendelea kubaki ile nyumba ya kwanza, baada ya hapo hio nyumba ilikuwa kama abandoned, ni mara chache sana tunaenda watoto.
Ila sasa cha kushangaza hio nyumba kuna mwanafamilia kwa mbinu anazojua yeye akaenda kukopea milioni 30 hivi, Na ajabu ni kwamba yeye tayari ana kazi mshahara almost milioni 4 kasoro na kajenga nyumba nzuri tu huko aliko.
Tunapewa taafifa na Mwenyekiti kwamba kuna Mwanafamilia kakopa pesa hizo kwa kuiweka dhamana nyumba
Taarifa ni kwamaba nyumba inakaribia kuwa mali ya taasisi hio ya kutoa mikopo, Ni kama vile lengo lilikuwa ni kuiuza nyumba bila nia ya kuresha mkopo.
Tulichoamua wanafamilia wengine
Tunaweza kumbana kwenye vyombo vya sheria lakini hatutaki kufika huko, hatutaki hadhara ijue haya matatizo ya kifamilia, hatutaki vyombo vya habari kuanza kututangaza, n.k.
A. Mwanafamilia mwenzetu aliekopa tumempa deadline ya kurudisha hizo fedha zote na riba sambamba na nyaraka za uthibitisho zisizo na shaka maana ni ndani ya uwezo wake na baada ya hapo kuna utaratibu maalum wa kuwajibika kwa alichofanya ikiwemo kwenda kuwaomba wazazi msamaha kaburini na kutuomba sisi msamaha,
B. Akikataa itabidi wanafamilia wengine tujichange tuikomboe nyumba lakini nasikitika kusema huyo mwengine hatakuwa sehemu ya familia tena, he will be an outsider atajijuaga mwenyewe na maisha yake, tutamzikaga tu.