Ni sharti gani ambalo mganga alikupatia na ukashindwa au kukataa kuendelea nalo

Top Gun

Member
Dec 11, 2024
47
169
Karibu vijana wa jadi
203fb559049c00e423c94caf436e2add.jpg
 
Ati mimi na yeye pamoja na viajuza vyenzake sita tukakae uchi kwenye makutano ya barabara kuu hapa Misungwi tena mchana kweupe huku magari yanapita kwa kisingizio kwamba hakuna atakayetuona; na magari yatakuwa yanatupita tu bila kutukanyaga nikasema haloooo!

Msione watu wa huku machimboni wana hela wanasukuma Fortuner mpya zero kilometer mkafikiri mchezo. Watu wamepitia mengi sana japo hawasemi. Ndiyo maana hata kufilisika na kufa kwao ni kugusa tu hasa wakikosea masharti.

Tangu siku hiyo niliamua kujikita kwenye kilimo cha nyanya na dengu. Mambo ya kwenda kukalishana uchi njia panda tena barabara kuu huku malori yakipita full speed tena mchana kweupe hapana aisee! 😄
 
Back
Top Bottom