GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 6,822
- 9,656
Inafahamika kuwa unapokuwa umemuasili mtoto Kisheria, anakuwa na haki zote kama watoto wako wa damu. Kuanzia majina, urithi na haki zinginezo za watoto wa kwenye familia.
Kama jina lako ni Mapema Akili, na mtoto uliyemuasili anaitwa Sahihi, majina yake kamili yatasoma Sahihi Mapema Akili. Kisheria, ni mtoto wako halali!
Ninachotamani kufahamu, ni namna sahihi ya kumtambulisha pale unapokuwa kwenye hadhara na ukawa unawatambulisha watoto wako kwa kuzingatia miaka ya kuzaliwa kwao: mzaliwa wa kwanza, wa pili... na wa mwisho au mdogo.
Ikiwa mtoto uliyemuasili ni mkubwa kumzidi mwanao wa damu, itakuwa sahihi kumpa hadhi ya uzaliwa wa kwanza ilhali si mwanao wa damu?
Ikiwa hutafanya hivyo na huku yeye naye ni "mwanao", na anafahamu kuwa ndiye mtoto mkubwa kiumri katika watoto wako, hakutamfanya ajihisi kunyanyapaliwa?