Ni ruhusa msimamizi wa mirathi kuuza mali za marehemu bila ridhaa ya warithi

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
92
1,685
NI RUHUSA MSIMAMIZI WA MIRATHI KUUZA MALI ZA MAREHEMU BILA RIDHAA YA WARITHI.

Bashir Yakub,WAKILI
+255 714 047 241.

Sheria inampa mamlaka msimamizi wa mirathi kuuza mali za marehemu bila hata kuhitaji au kupata ridhaa ya warithi.

Jambo la msingi kwake ni kuhakikisha kuwa uamuzi ule wa kuuza bila ridhaa ya warithi ni wa busara katika hali iliyopo na kuwa ni kwa ajili ya maslahi ya warithi wenyewe.

Kwa mfano : Kuna familia hasa za mitala ambazo warithi hawaelewani na hawawezi kukaa meza moja na kuamua jambo.

Au kuna familia ambazo kuna watu wanaendelea kufaidika na mirathi kama kuchukua kodi nk. wakati wengine hawafaidiki na chochote.

Au kuna watoto wadogo ambao wanahitaji mahitaji ya msingi kama ada huku migogoro haiishi nk, nk.

Msimamizi wa mirathi katika mazingira kama haya au mengine yanayofanana na haya anaweza kuuza mali za marehemu bila kuhitaji ridhaa au kuwashirikisha warithi.

Suala la msingi sana kwake ni iwe amefanya uamuzi huo kwa ajili ya maslahi ya warithi.

Fedha husika zitazopatikana katika mauzo hayo atazigawa kwa warithi kama inavyostahili.

Na ridhaa au ushirikishwaji huu si katika kuuza tu, bali hata katika kuzitolea maamuzi mengine(administration) mali za marehemu haitakuwa lazima kwake kupata ridhaa ya warithi.

Ni hapa huwa tunakusisitizeni kuwa msimamizi wa mirathi ni mtu nyeti mno na hivyo yafaa kuwa makini mnapokuwa mnamteua.

Tarehe 6 / 10 / 2023 Mahakama ya Rufaa chini ya majaji watatu imesisitiza tena jambo hili kupitia Rufaa Na.430/2022 kati ya SAID MPAMBIJE KAMAGA na FUNGULIA SWETU FUNDIKIRA dhidi ya NYAMHENDE SWETU FUNDIKIRA na Wengine.

Mahakama imesisitiza kuwa hakuna sheria inayomtaka msimamzi wa mirathi kupata ruhusa, au ridhaa ya warithi kabla kuuza ya nyumba ya marehemu.

Na ikaenda mbele kubariki mauzo ya nyumba yaliyofanywa na msimamizi wa mirathi bila ridhaa ama kuwashirikisha warithi.

Mahakama ya rufaa pia katika rufaa kati ya MOHAMMED HASSANI vs MAYASA MZEE NA MWANAHAWA MZEE (1994) TLR 225. ilisema hivyohivyo kuwa sio takwa la kisheria msimamizi wa mirathi kupata ridhaa ya warithi kabla ya kuuza mali za marehemu.

Vivyo hivyo katika Rufaa Na. 30/1990 kati ya AZIZ DAUDI vs AMIN AHMED ALLY.

Huu ndio msimamo wa sheria na tuujue.
 
Kwa Nini asiwashirikishe na kuwapa sababu hao warithi kabla ya KUFANYA maamuzi?
 
Sasa kama Warithi hawana masikilizano,yeye msimamiz wa mirath atawalazimisha watu wazima waelewane!? Ni kuchukua maamuzi magumu tu kama administrator, kama kuna makosa Mahakama itasema!!
 
Mkuu nakumbuka uliwahi anzisha movement ya kupinga bundles kupandishwa gharama and so on ghafla ukaitelekeza hiyo ajenda!! Ulikwama wapi?
 
Mkuu tafsiri zipo nyingi tu, mahakama za Tanzania unazijua, na watanzania unawajua vizuri. Ninachoweza kukushauri nyumba au kiwanja kikishakuwa cha urithi tena wa watu wengi achana nacho. Vinginevyo uwe mtu wa kupenda migogoro. Mifano ni mingi ya msimamizi wa mirathi kuuza nyumba kwa tamaa zake na ndugu wengine kukimbilia mahakamani, hizo kesi zinachukuaga hata miaka 20. Mpaka kufikia muafaka mnunuzi ndo anakuwaga kashaumia ela inaelea tu. Wakati mwingine watu wanauana kabisa. Ngoja niishie hapa.
 
Back
Top Bottom