Ni pombe gani haina alcohol kubwa nataka nianze kuutwika maisha yamenishinda

Nguva Jike

JF-Expert Member
Jan 22, 2018
1,141
1,599
Habari zenu.

Maisha ni yamenizonga sana nataka kuanza kunywa pombe angalau nipoteze kuwaza sana. Ni kinywaji gani hakina alcohol kubwa lakini kinatuliza mawazo?

Nawaza sana maisha mpaka nakonda na ninakula. Nimeambiwa nikinywa nitapata ahueni ya kuwaza sana.

Nielekezeni.
 
Vinywaji vyenye alcohol ndogo ni bia. Ambazo ni gharama sana. Maana mpaka ulewe unakunywa nyingi.

Vinywaji ambavyo havina gharama ni jamii ya kisungura, smart gin ama double kick ambavyo ndio vina alcohol nyingi ila vinakuzeesha fasta
 
Vinywaji vyenye alcohol ndogo ni bia. Ambazo ni gharama sana.

Vinywaji ambavyo havina gharama ni jamii ya kisungura, smart gin ama double kick ambebavyo ndio vina alcohol nyingi
kwa afya ya figo zake nashauri asinywe hizo! zitamuumiza zitamfanye aonekane kama mzee!!.
huyu hatakiwi kabisa kunywa kilevi chochote maana anakunywa kama kujipunguza mawazo!,hata punguza ataongeza! pombe inataka pesa so akianza kutumia ikamkolea ataanza kutoka kwenye bajeti ndo atayakora oga !.

pombe inataka heshima,pombe hunywi kupunguza mawazo pombe unakunywa kama sababu ya afya na si nje na hapo!,inafaa sana kunywa pombe kama sehemu ya unywaji wenye faida unakunywa glass zako mbili za wine baada ya kula inaimarisha mmeng'enyo wa chakula,hata ukienda kulala huoti unakimbizwa kimbizwa!.
zipo pombe nyingi nzuri ambazo mtu akinywa kwa ustaarabu hazitamletea shida zipo liqueur ni nzuri,zipo aperitif kwaajili ya appetite... sasa nyie endeleeni kunywa kwa kupunguza mawazo muone mnavyoyaongeza...😂
 
Back
Top Bottom