Ni muda wa kujirekebisha kabla hamjameza ndoano

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
12,473
50,827
Ndugu watawala wa jamhuri ya muungano wa Tanzania bado muna muda wa kujirekebisha.

Msipuuzie kelele za umma mtakuja kulia kilio Cha kusaga meno

Walinda nchi uchoka kulinda tawala zisizoeleweka.

Watu hawalali wakiwalinda watu wasio na maadili

Kwa jinsi mtawala unavyofanya mambo ya hatari ndio unahatarisha usalama wa Taifa kwahiyo walinzi uchoka!!

Wakeshaji kwenye lindo ulipwa ujira kidogo mwisho uishia kupora au kutengeneza mipango ya majambazi.

Uvumilivu una mwisho hizi siasa zenu za serikali za mitaa, watu kutekwa na kuuwawa, watu kupotea mpaka watoto kufumuliwa mioyo .

CCM niwaambie ukweli lazima mlaumiwe nyie

Mnazipa kazi idara za usalama ambazo uwa hazilali pia mnawapa kazi maafisa usalama ambao ufanya kazi kwa uhadilifu!!

Niwaambie tu ukweli mwaka mmoja huu ni mfupi Sana kuelekea 2025 lakini vile vile ni mrefu Sana .

Watawala tendeni haki kwenye uchaguzi serikali za mitaa mwezi huu msije kulia 2025 .

Hakuna kitu kisichowezekana mnajidanganya historia uwa ina tabia ya kujirudia

Tendeni haki narudia tendeni haki jikoni Moto unawaka maji yamechemuka mno!!

Siasa ya nchi hii mwelekeo wake ni pale alipoiacha Kikwete mwaka 2015 haitarudi Tena nyuma kila atakayejaribu kuirudisha nyuma atarudi yeye!!.

I love Tanzania
 
Wakeshaji kwenye lindo ulipwa ujira kidogo mwisho uishia kupora au kutengeneza mipango ya majambazi.
Hahaha kuna jamaa yangu aliambiwa alinde jengo ambalo halijamalizika kuna mbao kibao zingine mpya zingine zimetumika kwenye ujenzi wakawa wamezikusanya nyingi sana, sasa hawamlipi hata hela ya chai wanamlipa mshahara tu, jamaa unakuta anaingia kazini lindoni hana hata 100 halafu analinda utajiri wa zaidi ya million 500 akasema huu ufala akaanza kutangaza tenda kwa wamama na wababa wanaouza samaki kwamba ana kuni waje wachukue, kweli wakamuitikia akawaambia waje kwenye ule mjengo usiku waje wachukue kuni alikua anauza mbao 3 efu 5 maana akiuza mbao 30 anakunja zaidi ya mshahara anaolipwa aliuza zile mbao vibaya sana sababu zilikua nyingi mno, hapo nahisi mwenye akili atakua amenielewa
 
Back
Top Bottom