Ni Muda huu nasikiliza Mchungaji anakeme Bawasili, na kumwagiza muumini aende uani akajitazame amepona

Bush Dokta

JF-Expert Member
Apr 11, 2023
18,124
32,196
Ni kweli ukiwa na matatizo unakuwa na hali ya kitanga tanga sana ili upate msaada.

Bawasili ni uvimbe unaotokea ktk njia za haja kubwa kutokana na kuvimba kwa mirija ya damu inaopeleka damu sehemu hizo.

Mishipa hii ni matawi ya mirija mikubwa kutoka tumboni. Mishipa hiyo ni Superior Mesentary Vein na Inferior Messentary Vein. Hivyo unapokuwa na ukinzani( presha) ktk maungo ya tumboni au kiunoni hupelekea damu kujaa na kwa muda mrefu mishipa hiyo huwa dhaifu na kufura( bawasili- vinyama).

Sababu kuu za kuvimbisha mishipa hiyo ni ulaji usiofaa kunywa maji kidogo, kukosa Roughages yaani mboga mboga na matunda, kuzaa na mazoezi ya squarting kama kichura na Gym za Abdominal Workouts.

Sasa Huyu Mchungaji amewaombea wawili Mwanamke na Mwanaume.
Mwanaume amekiri amepona ila mwanamke akasema bado...akaombewa tena huyo Mwanamke akasema bado.

Ndipo mchungaji akamwambia Yesu wangu sio wa mashaka. Bawasili itaondoka tu. Akakemea tena kwa Jina la Yesu.

Akamuuliza tena dada bawasili zimeondoka? Dada akajibu bado. Mchungaji kamuuliza unamwamini Mungu? Akasema ndio. mchungaji kampotezea.

Mimi nimewahi kuhudhuria ibada za Mchungaji Mwingira, Mzee wa Upako, Kiboko ya Wachawi.

Sijawahi kushuhudia miujiza zaidi ya kusikiliza Shuhuda kwenye Redio na TV.

Sasa nawaza je tunapigwa?
 
Huyo mwanamke hawakumpanga vizuri na ujira wake hatapata,huyo mwanaume amecheza vyema at least mchungaji mtume pasta au yeyote awaye ataokota mamburula wawili watatu wakumchangia manunuzi ya Range Rover Sport yake
 
Kabla ya kuombewa alivua mkaona hizo bawasili ?
Aah aah hii huwa ni kwa njia ya simu kupitia radio au tv.

Yaani hao wanaoitwa wamepona hupiga simu na kueleza shida zinazowasumbua so pasta huwashushia maombi kwenye simu huku hao wagonjwa kila mmoja kwa wakati wake akikiri hapo hapo hewani on the spot kwamba amepona,kuna wajinga wajinga huamini hizi drama ndiyo maana huu ujinga hauishi.
 
Back
Top Bottom