Uchaguzi 2025 Ni Mpango wa CCM CHADEMA kisiwe chama cha kitaifa, Ndio maana Mbowe kwao ni Chaguo Sahihi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
27,205
65,599
Mpo salama!

Ninachowakubali CCM wanajua kusukuma Kete zao kwa AKILI Sana na pale inapohitajika nguvu kidogo wanatumia

CCM KAMWE haitaruhusu Chama chochote cha upinzani kiwe chama cha siasa cha kitaifa.

CCM hawaoni shida wala haiwashughulishi chama cha upinzani kutawala kanda Fulani au Mkoa Fulani, kwa CCM sio shida Zao.

Lakini CCM wataanza kupagawa pale na kuchukua hatua za haraka za akili na mabavu pale wanapoona chama cha upinzani kukipafa nguvu kitaifa yaani zaidi ya kanda mbili tatu chama cha upinzani kina nguvu.

Ndio maana uchaguzi huu wa CHADEMA hapana Shaka CCM ni lazima wawe upande wa Mbowe kwa Sababu ni kupitia Mbowe chama hakitaweza kuwa cha kitaifa kwani bado CCM wataendeleza Ile propaganda ya CHADEMA kuwa Chagadema na kuwa Sacco's ya Wachagga.

Kwa Sisi wenye macho ya rohoni, tunajua agenda kuu ya CHADEMA wanaotaka kumchagua Lisu ni kubadilisha mwelekeo WA chama kutoka kuwa chama cha kikanda Mpaka kuwa chama cha kitaifa kwa kuondoa ule uchagadema.

Kwa wanasaikolojia mtakubaliano na Mimi kuhusu Wanaomuunga Mkono Lisu wengi ukifuatilia Wana agenda ya Siri ambayo CCM wenyewe wanaijua na hawatakubali agenda hiyo ifanikiwe.

Haya
 
We dogo ni myopic sana

Chama cha kitaifa ni kikiongozwa na Tundu?

CUF inaongozwa na Mnyamwezi

ACT kinaongozwa na Mchagga.

Sura za kitaifa na ambazo sio za kitaifa ni kama zipi?

Hivyo vyama viwili vimefanikiwa kupata ushawish mkubwa kias gani?

Na hicho ambacho sio cha kitaifa kwanini kila uchaguzi nguvu kubwa ya dolla inatumia kukizima..

Think.
 
Kuhusu fam kuna tetesi 3
1. Wanasemaga ni ccm damdam.

2. Wanasemaga akipewa hela analegea,( tetesi toka Twitter kuwa kashalambishwa asali ya 12B+).

3. Wanasemaga ni ntu wa system
 
We dogo ni myopic sana

Chama cha kitaifa ni kikiongozwa na Tundu?

CUF inaongozwa na Mnyamwezi

ACT kinaongozwa na Mchagga.

Sura za kitaifa na ambazo sio za kitaifa ni kama zipi?

Hivyo vyama viwili vimefanikiwa kupata ushawish mkubwa kias gani?

Na hicho ambacho sio cha kitaifa kwanini kila uchaguzi nguvu kubwa ya dolla inatumia kukizima..

Think.

Ukisoma uwe umetulia Mkuu.

Kama huna Kazi rudia kusoma pengine utaelewa Walau kidogo
 
Back
Top Bottom