Ni mavazi gani unaweza vaa siku ya kwanza kukutana na mpenzi wako?

Villky_J

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
492
609

Habari wanajamiiforum.

Leo tushirikiane katika hili. Kumekuwa na utata mkubwa sana kwa pande zote mbili husasani siku ya kwanza kukutana na mpenzi wako, ambae labda kwa muda mrefu mlikuwa mkiwasiliana bila kuonana ana kwa ana.

Wengi wetu huwa tunazidisha madoido mpaka tunaboa kiasi kwamba badala ya kupendeza ndio tunaharibu hususani kwa dada zetu. Unakuta mwanadada kajipodoa mpaka sura imebadilika inafanana na mwanasesere.

Upande wa wanaume mtu kajipigilia mpaka dada hata kuongozana nae anaona aibu. Sio macheni, makoti, mara makofia humohumo mpaka hajulikani kwamba anataka kuwa gentleman au bishoo yaani haeleweki.

Karibuni wadau tupeane uzoefu.
 
Inategemea huyo mpenzi wako anapenda kukuona na mavazi gani.
 
Mi napenda avae t shirt na jeans na buti matata za kimayooo na sun glasses
 
Hakuna nguo maalum maaana kuna wanaoelewa hyo na wasioelewa,kuna wenye nacho na wasionacho so yyte tu
 
jeans nzuri ( isiwe ya special dukani iwe mtumba classic) t- shirt ya special ( isiwe mtumba), saa nzuri yenye mikanda ya leather ila hata aina nyingine sio mbaya, usivae ma- miwani ya kuchomelea mageti, vaa kiatu ukipendacho ila isiwe buti ndefu, be moderate piga unyunyu ( body spray) wa kawaida.
usivae ma- cheni kama minyororo ya kufungia mbwa, au yale ya 50cent, ingekusaidia zaidi ungekuwa tall maana wanawake/wasichana wanarubunika haraka sana na mameni tall,

#NB. kumbuka kuijaza wallet yako yale mshetani mekundu ( pesa isipungue 150,000),.....hii itakusaidia sana kama huyo m/mke atahitaji kinywaji au chakula cha ghalama ( ili usianze kusema kuku choma ni wabaya kiafya),...usiwe bwege jitahidi urudi na angalau 70...au 80..nyumbani

Jitahidi umgegede siku chache au siku hiyohiyo halafu mteme ( la sivyo atakuchuna sana)
USIAZIME GARI la Mtu..

by Saguda47...kutoka mkoani
 
Ww umenielewa mibashara maana kuna watu wanacomplicate mpk unawashangaa wanaenda kwenye event ama
Mtu ambaye hujawahi kuonana naye unakuwa hujui anapenda styl gani sasa ujikurupishe na msuti wako... Au ndio umevaa kama vijana wetu wa kitaaa jeans
imechanwa na zile t-shirt
unfinished...
 
Duuuu...
umetisha mkuu nimekusoma
 
Mtu ambaye hujawahi kuonana naye unakuwa hujui anapenda styl gani sasa ujikurupishe na msuti wako... Au ndio umevaa kama vijana wetu wa kitaaa jeans
imechanwa na zile t-shirt
unfinished...
hapo utakuwa umejipalia makaa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…