Ni lazima mama wa mume kuhudumiwa na mke wa mtoto wake?

happymsafi

Senior Member
Jul 4, 2016
100
84
Jamani ni lazima mama wa mume kulelewa na mke wa mwanae hata kama huyo mama ana watoto wake wa kike wakubwa wengine wana kazi zao na wanajitegemea wenyewe? Mi bmiinafsi naona si sawa kama mama ana watoto wake wakike ni bora kuenda kukaa kwa watoto wake wa kike wamhudumie kuliko kuenda kuhudumiwa na mke wa mwanae.

Tabia ya binadamu hawezi kuhudumia mtu ambae si wake kama atakavyo muhudumia mtu wake na endapo atamuhudumia basi lazima matatizo yatatokewa yule anayehudumiwa anaweza akahisi kama hapewi huduma inayostahili kupewa hata kama mhudumu anajitahidi kwa kiasi gani.

Jamani wadada ambao mna mama zenu baba zenu ambao wanahitaji huduma wachukueni wazazi wenu muwahudumie wenyewe msiwasukumie wifi zenu kwani wifi zenu pia wana mama zao baba zao wanahitaji kuwahudumia vilevile. acheni kuwatafutia watu matatizo ya lazima.

Mimi binafsi siwezi kumuacha mama'ngu aende kuhudumiwa na mke wa kaka yangu hali ya kuwa mie nipo. Huko ni kumpa mtu mzigo huku ukijuwa kabisa mama yako hawezi akapata huduma nzuri kama utakayompa mwenyewe.

Mwisho wa siku mnaona watu wabaya wakati wabaya ni nyie wenyewe uwezo wa kulea wazazi wenu mnao lakini mnawapeleka kulelewa na mtu aliekutana na kaka yako ukubwani hamfahamu amelelewa vipi halafu mnaleta lawama tu.

Kina dada chukueni wazazi wenu muwalee wenyewe kama pesa ya kumtunza kaka yako atakuletea huko kwako lakini si kuenda kumuachia wifi yako kama vile yeye ndo ana haki ya kukulelea wazazi wako hali ya kuwa yeye mwenyewe ana wazazi wake wanahitaji kulelewa?

Kwanini ushindwe kumlea mzazi wako uzeeni akiwa mgonjwa mpaka umsukumie mtu baki wakati yeye alikulea kwa hali zote raha na furaha ukiwa mdogo. Jamani leeni wazazi wenu wenyewe wifi zenu pia wana wazazi wao wa kuwalea.
 
Inategemeana na mila za kwenu, mila za Kilimanjaro wachaga mtoto wa kiume mkubwa analea mama, wapare mtoto wa kiume mdogo ndiye mwenye jukumu hilo, kwahiyo haiwezekani kuingia kwenye familia ya watu ukavuruge utaratibu kisa hujiamini kuwa mwema ama huoni tu kuwa ni sawa, mila na desturi za watu lazima ziheshimike, kama wewe ni mke wa familia ya hii taratibu ukitaka kuthaminiwa kubali na heshimu Mila za kwa kuondoa migongano na Laana zisizo za lazima.
 
mara nyingi hawa wazee wana tabia fulani inayopingana na mipango ya watoto wake. Mzee huangalia vitu vingi tu kwa anaemtaka amhudumie. Eidha huyo mtu si mlalamishi, msengenyaji, Mbahili, na sio mpenda usafi kupitiliza, sio mchoyo, anayejali na kusikiliza kwa ukaribu nk. Sasa inawezekana Wewe ndie aliekuchagua kuliko hata binti zake.
 
Inategemea jamani..
Siyo kila mtu anaweza kukubali mke ampeleke mama yake kwenda kuugulia kwake..
Wengine hata ndugu akija kwako kidogo atakuambia naomba umwambie huyo ndugu yako aondoke
Ila ndugu zake wakiwepo hamna shida kabisa...
 
Ila wachaga wabinafsi sana..
Na ni bora mchaga aoe mchaga mwenzie..hapo wataelewana sana
Asilimia kubwa ya Mama zenu wanapenda kushindana na wakwe especially kama cyo wa huko kwenu
 
Mie nitahudumia kwa uwezo wangu kama haridhiki mlango uko wazi arudi kwake

Sonia;
Ukiusoma uzi ulioandikwa na huyu mdada ni wazi kabisa kwamba hampendi mama mkwe wake. Ameogopa kusema tu. Swali; Hivi ka si huyu mama, huyo mume wako ungelimpata wapi?? Kwa nini ulikubali kuolewa badala ya kukaa na mamako ukamlea hadi afe ndio uolewe?
Hata angelikuwa na watoto 8 wa kike na wakiume 1 tu aliyekuoa. Wewe ndiye wa kumlea, kumtunza na kumuogesha. Ni heshima kuwa, kakuzalia mume. Mtunze kwa heshima kama unamheshimu mumeo. Ila kama ni hao wanawake wa siku hizi mnaowadharau waume zenu, hata mamake utamdharau tuuu.
Hao mawifi nao kule waendako watawakuta mama mkwe. Wawatunze ka wa kwao anavyotunzwa.
 
Nimeona huu uzi inabidi umenikumbusha mbali sana, baba yangu akiwa kitenda mimba kwenye familia yao bibi mzaa baba aliishi na sisi siku za mwisho za maisha yake. Ilifika wakati hata hakuweza kukaa pekeyake na msaidizi tu. Alikuja akiwa na 80+ na tuliishi nae kwa kama miaka kumi na zaidi. Uzee unakuja na mambo mengi sana. Hakutaka nguo zake zifuliwe na mtu ambae si ndugu yake, house girl, wote hao walikuwa watu baki pamoja na mama pia. Ndugu zangu wakiwa shule ilibidi niwe mfua nguo, sasa ile umetoka kupaka nail polish unaingia chumbani uchukue novel mwenyewe ukasome, unapewa nguo za kufua.
 
Tatizo mabinti mnaoolewa...

Hebu mkawe baraka kwenye miji ya watu

Mama wa mumeo ni sawa na mama yako..... hata mama yako anaweza kulalamikia huduma. Utampeleka kwa nani?
Kwani ukitimiza wajibu wako na kumhudumia kwa upendo maneno na lawama zitakuchubua ngozi???

Kiafrika wazazi huenda kwa watoto wao wa kiume unless kuwe na sababu nzito... ndio wazazi huenda kuugulia kwa binti...kumbuka binti kaolewa. Yupo mji mwingine ndio maana wazazi wa kiafrika huona shida kwenda kwa binti....


Hivyo wakamwana jamani...muwe na upendo....muwe wavumilivu
....muwe na kiasi mkawe baraka ktk nyumba na miji muingiayo
 
AMEN mpendwa.
 
Busara zako naomba zıwafıkıe mabıntı wote wenye akılı za kuku
 
Huyo mtoto wa kike inawezekana ana kwake lakini ni kwa mumewe pia. Kwahiyo mimi kama mume usimuhudumie mama yangu lakini mama yako akae kwangu umuhudumie.
Ukishakuwa na fikra hizo tayari ushaweka roho mbaya kwenye nafsi yako na huyo mkweo hata akiwa mwema utamtafutia dosari maana tatizo lako si kulea mama wa mwenzio tatizo lako ni roho mbaya. Kumbuka utazaa watoto wa kiume na ipo siku utakuja kuwa mama mkwe wa mtu.
 
Inategemea jamani..
Siyo kila mtu anaweza kukubali mke ampeleke mama yake kwenda kuugulia kwake..
Wengine hata ndugu akija kwako kidogo atakuambia naomba umwambie huyo ndugu yako aondoke
Ila ndugu zake wakiwepo hamna shida kabisa...
Na hii ndo dosari ya wanawake wengi, kuthamini ndugu zake kuliko wa mume. Ukisaidia upande wake wewe ni mkarimu mno ila ukisaidia kwenu basi una matumizi mabaya ya pesa.
 
mwee kikwetu sie kumlea mama mkwe sio ombi ni lazima, na kwanini usimlee labda, huyo ndo mama mzaa chema kama unampenda mumeo lazima upende na familia yake, wala hutakiw kuuliza. yani wew ukae na mama yako kwa mumeo halaf mama yake asiwepo, hiyo haipo

ila inategemea na mila zenu na tamaduni zenu, lakin kwa ushaur kama mama mkwe yupo jivunie kuwa nae na umjali vyema, na mama yako nae atatendewa the same.
 
This is a real African woman. sio watu wanakuja na mambo yao ya kizungu wakati wanajua mila na desturi za kwetu.
ndugu zake ni wa kwetu ila ndugu zangu ni wangu.
kama unaweza kumlea mama yako ukiwa na mume wako, kwa nini mumeo ashindwe kumlea mama yake akiwa na wewe!???
kiafrica ukiolewa unakuwa ni mtoto wa kule ulikoolewa na unapaswa kuchukua kazi zote za watoto wa kike wa nyumba ile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…