Ni kweli Watanzania wanahitaji Katiba Mpya?

Dec 26, 2021
33
23
Ni kweli watanzania wanahitaji katiba mpya?

Kabla ya kuanza kutekeleza hitaji la katiba mpya, ni lazima tujue watanzania wangapi ni wahanga wa katiba ya Sasa.

Tukishajua wako wangapi ni lazima pia tujue pia muamko wao pia.

Kupitia muamko huo, tutapata kujua uelewa wao wa katiba iliyopo madarakani.

Na uelewa wao utatusaidia kipi kifanyike aidha katiba ibadilishwe ama tutatue changamoto zinazokwamisha sheria za ndani ya katiba kwa Nini hazitekelezeki?

Changamoto zitazobainika zinakwamisha utekelezaji na usimamiaji wa sheria za katiba ya Sasa. Ndio zitatuambia Sasa ni kweli tunahitaji katiba mpya au maboresho ya baadhi ya sheria za katiba ya sasa n.k

Sasa tujiulize
1: Wewe mwenyewe ambae unaunga mkono mchakato wa kudai katiba mpya, katiba ya Sasa unai-ielewa? Kama unaielewa ni changamoto zipi zinazokwamisha Sheria za katiba ya sasa zisitekelezwe? Suluhisho ni kudai katiba mpya? Katika Jamii inayokuzunguka wangapi Wana uelewa wa katiba ya Sasa?

2: Hitaji la kudai katiba mpya, ni hitaji la Watanzania wote au ni hitaji la viongozi wa vyama pinzani?

Kiuhalisia ni hitaji la viongozi wa vyama pinzani, ambao wanaijua katiba vizuri na madhaifu yake na ndio ambao wanaoshawishi wafuasi wao.

Wafuasi wao nao si wote wana-uelewa wa katiba ya Sasa na wimbi kubwa la wafuata upepo.

Huwezi kudai mabadiliko ya kitu wakati hicho kitu unachokitaka kukibadilisha hukijui na hukielewi, athari yake ukibadilisha Kuna uwezekano wa kurudia makosa ya awali ya kile ulichokibadilisha.

Watanzania walio wengi hawaijui katiba ya Sasa na wengine mpaka wanazeeka hawajawahi kuisoma na hata kuiona.

Huenda ni kwa sababu haipatikani kwa urahisi au ujinga wa kutokujua umuhimu wa katiba katika maisha yao ya Kila siku wawapo nchini na huenda wizara husika ya Sheria na katiba imeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha na kuhakikisha Kila Mtanzania anakuwa na elimu ya Sheria za katiba na anakuwa nayo kwa urahisi.

Sababu na changamoto ni nyingi, lakini suluhu ni nini?

Suluhu ni kudai marekebisho ya katiba bila kuijua katiba ya Sasa faida zake na madhaifu yake?

Suluhisho si kudai katiba mpya, suluhu ni kuhakikisha watanzania zaidi ya asilimia 80 wanaijua katiba ya Sasa na kuielewa na waitumie ndani ya muda Fulani. Mtanzania azijue haki zake za kikatiba ya Sasa, na azitumie.

Vyama pinzani na watanzania kiujumla,waishurutishe wizara husika na wizara shirikishi kama wizara ya elimu, kuhakikisha katiba ya Sasa inapatikana kwa urahisi na elimu ya Sheria ya katiba inapatikana Kwa Kila mtanzania.

Mfano: Katiba ya Sasa Ina Sheria nzuri za mirathi, lakini bado unakuta mjane na watoto wake wanazurumika.

Ni kwa sababu mjane haijui Sheria inayomlinda na taasisi husika ngazi yake ya kata hazipo. Hivyo humpasa awe na fedha na muda wa kumsafiri kwenda kudai haki yake. Sasa ni wangapi Wana uwezo huo?

Swala la kudai katiba mpya kwa sasa ni swala la kisiasa na la kuwanufaisha wanasiasa.

Maana wahanga hawapewi elimu hiyo na pia vyama pinzani badala ya kudai kila kata ipate mahakama ya mwanzo. Maana unaweza ukawa na Sheria Bora na katiba Bora, lakini mahakama zipo mbali na wewe. Huna pesa huwezi kufuatilia haki zako za msingi kisheria.

Vyama pinzani kama kweli wanataka katiba mpya inabidi wahakikishe haya

1: Mahakama za mwanzo ziwepo katika Kila kata nchini.
2: Katiba mpya na elimu ya awali ya haki za kisheria kikatiba inapatikana kwa urahisi na ngazi zote za Mtanzania.
3: Watanzania wapatiwe uelewa wa Sheria za kikatiba.

Vugu vugu la kudai katiba mpya lipo kwa watanzania wanao ishi mjini, na lipo kinywani na mtandaoni, hao mjini tu kuna wimbi kubwa la wasioijua katiba vyema hao wanafuata upepo. Uamko vijijini ni mdogo na kule wana-mahitaji Yao makuu nje ya katiba mpya.

Chama chetu pendwa, ambacho ndio chama tawala lipo sahihi kusema watanzania Wana mahitaji ya msingi nje ya katiba mpya.

Ni kweli maana Tanzania ina vijiji vingi kuliko miji, na kwa maana hiyo watanzania wenye uhitaji wa mahitaji mengine nje ya katiba wapo wengi mno nchini.

Mh. Freeman Mbowe na viongozi wengine shiriki wa vyama pinzani, yapasa wahakikishe wanawafikia watanzania wengi wa vijijini ili kudai katiba mpya kwa kuanza kuwapa elimu na kuwapigania wanapata mahakama za mwanzo.

Wilson M. Mwalukasa
T. Civil Engineer
Smart Ujenzi

Tuna-Husika
1. Ramani za Nyumba na Majengo mbali mbali.
2. Ujenzi na Kuandaa tathmini za ujenzi.
Mawasiliano:
Simu na Whatsapp.
0762-704-031
0654-704-031.
 
Sio katiba mpya peke yake tunahitaji mahakama zenye uhuru,ofisi ya DPP yenye uhuru,tume ya uchaguzi yenye uhuru...ndio mana ccm kumejaa wajinga na majambazi kwa vile katiba walitengeneza wao
 
Sio katiba mpya peke yake tunahitaji mahakama zenye uhuru,ofisi ya DPP yenye uhuru,tume ya uchaguzi yenye uhuru...ndio mana ccm kumejaa wajinga na majambazi kwa vile katiba walitengeneza wao
Watanzania wangapi wenye uelewa wa Sheria za katiba ya Sasa?
Hitaji letu ni nini haswa?

Vyama pinzani mnadai Katiba mpya, wakati ngazi ya kata hamna mahakama

Watanzania walio wengi ambao wapo vijijini, hawana mahakama za mwanzo. Sasa tudai tupate mahakama katika Kila kata au tudai katiba mpya au tudai maboresho ya katiba ya Sasa?
 
Kama unajiona hutoshi, usichangie. Kama hujui hata katiba ni nini, siyo lazima uizungumzie. Kama hata hisitoria ya katiba iliyopo, na hali yake ya sasa na matatizo makubwa yakimsingi yanayotokana na mapungufu ya katiba hiyo, huwezi kujadili katiba ama iliyopo ijayo wala umuhimu wake.
Huwezi kuwa katika timu ya waamuzi wakati unahitaji elementary knowledge ya jambo linalotakiwa kuamuliwa na ndiyo sababu kuna wataalam katika kila nyanja.

Katiba inayolinda madhaifu kwa sababu yananufaisha kundi fulani la watu, katiba inayoshamirisha utwana na ubwana katika nchi ya kidemokrasia, katiba isiyojali kesho ya taifa, hiyo si katiba ya taifa.

Kwa ufupi, hakuna haja ya kuanza kujadili hapa kama tunahitaji ama hatuhitaji katiba mpya. Hili swali la kizamani sana. Ili ujiupdate, pitia mchakato wa tume ya jaji Warioba ili kupunguza muja wa mjadala.

Tunahitaji katiba ya nchi, si katiba ya vyama fulani vya siasa.
 
Kama unajiona hutoshi, usichangie. Kama hujui hata katiba ni nini, siyo lazima uizungumzie. Kama hata hisitoria ya katiba iliyopo, na hali yake ya sasa na matatizo makubwa yakimsingi yanayotokana na mapungufu ya katiba hiyo, huwezi kujadili katiba ama iliyopo ijayo wala umuhimu wake.
Huwezi kuwa katika timu ya waamuzi wakati unahitaji elementary knowledge ya jambo linalotakiwa kuamuliwa na ndiyo sababu kuna wataalam katika kila nyanja.

Katiba inayolinda madhaifu kwa sababu yananufaisha kundi fulani la watu, katiba inayoshamirisha utwana na ubwana katika nchi ya kidemokrasia, katiba isiyojali kesho ya taifa, hiyo si katiba ya taifa.

Kwa ufupi, hakuna haja ya kuanza kujadili hapa kama tunahitaji ama hatuhitaji katiba mpya. Hili swali la kizamani sana. Ili ujiupdate, pitia mchakato wa tume ya jaji Warioba ili kupunguza muja wa mjadala.

Tunahitaji katiba ya nchi, si katiba ya vyama fulani vya siasa.
Palipo nguvu kubwa ya wananchi, jambo lao au hitaji lao ni rahisi kutekelezwa.
Unakubaliana na Mimi mpaka hapo?

Wananchi wenyewe ni watanzania, je watanzania wangapi wanaielewa katiba ya Sasa na ni wangapi Wana muamko kama wako? Maana muamko huu upo mitandaoni na jamii za mjini, na watanzania wengi Kwa idadi ya taifa ipo vijijini na ndio wahanga wa uendeshwaji wa shughuli za kisheria.

Je hao wana muamko huo? au ndio wachache wapate kuamulia wengi, kwenye mchakato huu?

inahitajika muda, rasili Mali fedha na watu na elimu Pana sana, watanzania wapate kueleweshwa kuhusu katiba ya sasa halafu ndio tutadai katiba mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom