Ni kweli wanaume waliooa wanawake wasomi wanapata raha hizi?

roselina john

JF-Expert Member
Aug 17, 2017
758
943
RAHA YA KUWA NA MWANAMKE MSOMI na MWEREVU, MESEJI ZAKE

1. Ndio mpenz wangu, nimekumiss sana. Naenda pata lunch, tutaongea vizuri baadae. Love you!

2. Mume wangu kipenzi nazidi kumuomba Mwenyezi Mungu atupe amani na upendo katika familia yetu tarajiwa.

3. Sitaacha kukupenda, nitakuombea na nitaku-support pale ukinihitaji kwa chochote hata kwa ushauri nishirikishe, plz kuwa mwaminifu na mie.

4. Alafu kile kiwanja kimekaa pazuri cha kufanya tuweke fremu za biashara mme wangu, ila tukipime kiwanja.kwanza,

5.umekumbuka kumtumia shemeji yangu ada mme wangu? Hujui elimu ni ufunguo wa maisha?

6. Nimeyasikia matatizo ya wifi yangu lakin mme wangu msamehe hakuna aliyemkamilifu mme wangu

7. Mi nahisi jumapili ijayo nikawatembelee wakwe zangu, ila napaswa tupange niwapelekee zawadi gani,

Hizo ndo messeji utatumiwa na mwanamke msomi na mwelewa,

SASA UWE NA MWANAMKE MWENYE BIRTH CERTIFICATE TU

1. Morning babe, send me credo..plz bae

2. Bae plz dont 4get pizza, alaf kuna mtu anauza perfume nzuri kweli. Luv u xo xo

3. Bby time 4 swimming, naenda na my friends then i need some money plz

4. My handsome boy buy me data plz

5. Mpeenzi sijikii kuthoma 2chat bax , mi ntalia.. nshanuna hapa.

6.My hubby naomba hela ya dela la kuendea kwenye 40 ya mtoto wa Maimuna

7.Bebe nataka niende msibani plz plz naomba hela ya saluni tyuuu

8. Kwanini ulinioa kunitesa huwaoni wanaume wenzio ambao wamesoma wana vyeo,

9.wadogo zako wanajazana hapa na kuchafua sebule ,hawana kazi uko kijijini?

10. Mme wangu kwenu siendi tena kwanza mama yako ananitukana mlevi alafu nyumba za vile sijazizoea, kunguni jamani,

Wanaume Chukua hatua oa msomi na mwelevu angalau awe kamaliza kidato cha nne
 
Mimi naona sio suala la usomi au kutokusoma per se, ni suala la kizazi cha nyuma (wahenga) wenye majibu/msg nzuri na kizazi cha sasa a.k.a kizazi cha dot.com ambacho wengi wao wamejaa tamaa mbele na kuomba hela kila kukicha haijalishi kasoma au la.
 
Wasomi wengi mizigo huu ndo ukweli ambao ni mgumu kuusikia..wachache sana wamesoma na bado wana akili nzuri za kudumisha mahusiano we kama hutaki usumbufu,vurugu,kupandishiwa sauti mbele ya watoto wako ..oa mwenye elimu ya kawaida...ila kama unaa bahati unaweza kupata msomi anaejielewa na hapo ni bahati nasibu tu......sio kwa uwezo wako bali zali tu linakudondokea..
 
Back
Top Bottom