Ni kweli Waislam wamekataliwa kutumia Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya Eid fitr baada ya kukubaliwa?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,954
32,058



Wanamajlis,

Nimepokea taarifa hii leo asubuhi najaribu kupata ukweli:

[11:11am, 02/07/2016 Waislam wakataliwa kutumia uwanja wa uhuru kwenye sherehe za eid.

*Mwanzo walikubaliwa na wakaambiwa walipie tsh 10,000,000/=

*Baada ya kutekeleza maelekezo hayo , ikaja amri nyingine ya kunyimwa kibali cha matumizi ya uwanja huo.

*Waislam watilia shaka kuwa kuna agenda ya siri, kwani hakukuwa na sababu za msingi.

*Waislam waomba rais kuingilia kati.

* Yatangaazwa kupatikana kwa hasara ya zaidi tsh. 50,000,000/= kwajili maandalizi ya sherehe hizo.



Mashindano ya kuhifadhi Qur'an Uwanja wa Uhuru yaliyotayarishwa na
Sheikh Nurdin Kishki Mwezi wa Ramadhani 2016
Mashindano yakuhifadhi Qur'an yalijaza watu kushinda mpira katika uwanja ule...ujumbe ule ni mzito kwani dunia nzima picha za Waislam walioshonana kusikiza Qur'an zilionekana...wengi bila shaka walisema, "Ala Tanzania kumbe Waislam wengi vile!" Hii inawezekana imewatisha wenye mamlaka ya kutoa na kutotoa, wenye mamlaka ya kuwasha na kuzima...

Ukiitazama hiyo picha unaweza kudhania Simba na Yanga wako uwanjani wanawania kombe la ubingwa lakini siyo umma umekuja kusikiliza Qur'an siyo kuangalia mpira.

Hii haijapatapo kutokea nchini petu.
Alhamdulilah...


 

Ustaadhi Mohamed Said Waislam kukataliwa wala si hoja kwani uwanja wa Uhuru umejengwa na BAKWATA ?.Ule ni uwanja wa michezo si msikiti jengeni msikiti mkubwa mfanye sherehe zenu.Mbona CHADEMA wamekataliwa kwingi kufanya mikutano yao tena wakati mwingine mikutano ya ndani au nao ni waislam acha zako kupandikiza chuki za kidini wakati unajuwa wazi awamu hii uhuru wa kukutana umewekewa pingamizi nyingi.
 
Halafu sasa uwingi wao unamsaidia nini mmoja mmoja ktk kuitafuta pepo? Uwingi uende sambamba na kupungua maasi.
 
Ngongo,
Ahsante kwa majibu yako.
Hakuna neno.

Mimi naweka kumbukumbu.
Hii blog yangu ni ya kueneza habari za Waislam wa Tanzania.
 
Kweli mzee wangu, ingawaje hata ukizoom utaona wamekuja kusikililiza Qur'an na jezi zao za yanga... Badala ya kuvaa vazi la heshima hususan kanzu katika kipindi kama hiki... Naomba tu kujua hii picha haikuchukuliwa katika mechi na tp mazembe?
huoni picha ya chini vibaragashia vilivyojazana ?
ile ya juu ni kweli yaweza kua yanga vs tp mazembe lakini hiyo ya chini hata kama hujui kusoma picha pia huzioni
 


Sioni waislam hapa bali naona mashabiki wa Yanga sijui kwanini unapenda uchonganishi wa kidini hivi ilihali unajuwa wazi mikutano ya vyama vya upinzani pia imezuiliwa kwa kisingizio cha vurugu huyo ndio Magu baba wote mtaisoma namba.
Ngongo,
Hebu angalia na picha hizi hapo chini:







 
Hyo picha ni ya Yanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…