Kumekuwa na minong'ono mingi kwamba uongozi wa serikari ya Magufuli unauwa upinzani.
Kwa maoni yangu upinzani wa nchi yetu uko katika makundi mawili makuu:
1.Wabishi (opposers).
-Hawa ni watu wanaokataa kila kitu hata kama ni cha ukweli ili mradi kulinda masilahi yao.
2.Wanaharakati (Protestants)'
-Hawa ni wale wanaokataa mambo wanayoyaona yanawanyima haki zao au za wenzi wao.
Mimi naona upinzani ulioko kwenye kundi la kwanza haupungui kutokana na uongozi wa serikali ya Magufuli.
Ikumbukwe kuwa kundi hili la upinzani haliko tu kwenye vyama vya upinzani bali liko pia kwenye chama tawala.
Kundi la pili la wapinzani ndilo linalopungua .
Hii nadhani ndo maana watu wanasema upinzani unakufa.
kama upinzani ni wa aina hii,inawezekana ukawa unakufa kweli kwani watu wengi wanaopinga kudhulumiwa haki zao watazidi kupungua kadri serikari itakavyokuwa inarejesha haki kwa watanzania.
Ila sidhani kama kundi la kwanza litaathirika maana lenyewe kazi yake ni kubisha tu ili mradi kulinda maslahi yake.
usiposifia mwaka huu utanuniwa na kila mtu. kwa mabaya au mazuri we sifia tu ila wakumbuke kuna mtu hapa alisfiwa mpaka akaitwa kijana uku akiwa na umri usiopungua 50 na mwingne mr clean lakin matokeo tumeyaona.
hili ndio tatizo la watanzania wavivu wa kufikiri kwa mapana
Upinzani hauwezi kufa wakati mfumo wetu wa kisiasa ni wa KIDEMOKRASIA. Uelewa wa Watanzania walio wengi mfano mzuri ni wewe mleta mada,ndo unazidi kufa.Elimu,Elimu,Elimu ni tatizo kubwa TZ that's all we need kwanza mengine baadae