Doncy monco
Member
- Jul 26, 2019
- 38
- 104
Kutokana na changamoto za kimazingira, kiuchumi na kijamii, watu wengi wamejikuta wakikosa furaha. Ni wazi kuwa kukosa furaha kuna madhara makubwa kwenye afya ya mwili, akili na hata katika utendaji wako wa kazi.
Watu wengi hutamani kuwa na furaha lakini bado hawapati furaha; wengi hudhani kuwa na vitu kama vile pesa ndiyo chanzo cha furaha, lakini mambo hayawi kama walivyotarajia pindi wapatapo vitu hivyo.
Je unahitaji kuwa na furaha ili uboreshe afya na ufanisi wa utendaji kazi wako? Karibu nikushirikishe njia 10 za kukufanya kuwa na furaha.
1. Samehe
Watu wengi hukosa furaha kutokana na kubeba uchungu na maumivu yaliyotokana na watu waliowakosea. Ikiwa unataka kuwa na furaha ni muhimu kumsamehe aliyekukosea hata kama hajaomba msamaha.Kumsamehe aliyekukosea kuna manufaa kwako zaidi kuliko kwa yule aliyekukosea. Mara nyingi aliyekosea huendelea na maisha yake ya kawaida huku aliyekosewa akizidi kuumia.
2. Fanya unachokipenda
“Mafanikio siyo ufunguo wa furaha. Furaha ni ufunguo wa mafanikio. Kama unapenda unachokifanya, utafanikiwa.”Moja kati ya siri kubwa ya kufanikiwa na kuwa na furaha katika kile unachokifanya, ni kwa kupenda kile unachokifanya. Unapopenda kile unachokifanya, utakuwa na amani na furaha mara ukutanapo na changamoto au vikwazo.
3. Kuwa na shukrani
Mara nyingi tunatazama mambo mengi kiasi cha kushindwa kuwa na shukrani kwa Mungu kwa kua ndiye anayetujalia yotee pia kuwashukuru waliotusaidia kwa namna moja au nyingine.
4.Saidia wengine
Kumsaidia mtu mwingine siyo kumpa pesa au vitu; hata kumpa mtu ushauri au kumtia moyo kunaweza kuwa na maana kubwa kwa mtu huyoUnapomsaidia mtu mwingine unajisikia kuwa na thamani na furaha kwani umeweza kufanya kitu chenye manufaa kwenye maisha ya mtu mwingine.Nakumbuka niliwahi kumshauri mtu mmoja aliyekuwa amekata tamaa kutokana na kukosa pesa; baada ya muda kupita nikakutana naye, akashukuru sana kwa ushauri wangu. Alinieleza kuwa kama siyo yale maneno niliyomweleza angekuwa ameshajiua. Ni wazi kuwa nilijihisi mwenye furaha na amani kutokana na kuweza kumsaidia mtu mwingine.
5. Shirikisha wengine
Inawezekana jambo linalokukosesha furaha kuna mtu mwingine anafahamu utatuzi wake. Hivyo kwa njia ya kumshirikisha mwingine utapata ushauri au hata utatuzi wa tatizo lako. Jambo la kuzingatia ni kuhakikisha unamshirikisha mtu sahihi.
6. Ondoa mawazo hasi
“Akili ni kila kitu. Unavyofikiri ndivyo unavyokuwa.
Mawazo gani uliyonayo kwenye fikra zako? Je unawaza tu huwezi au kushindwa? Mawazo hasi au ya kushindwa ni chanzo kikuu cha kukukosesha furaha.Amini unaweza hatakama unaona giza; leo ni giza, kesho ni mvua lakini keshokutwa jua litawaka.Usikate tamaa, ondoa mawazo mabaya yanayokufanya ukose furaha na mani sasa
7. Usitafute ukamilifu
Mara nyingi watu hukosa furaha kwa sababu wanatafuta ukamilifu. Kwa hakika hakuna binadamu aliyekamilika; wote tuna madhaifu na mapungufu hivo jitahidi uishi na watu vizuri ili uwe na fraha.