Ni kawaida ya tajiri kuchukiwa, kama unataka utajiri jiandae kwanza kuchukiwa

Teslarati

JF-Expert Member
Nov 21, 2019
2,454
9,885
Niliwahi kumuuliza tajiri mmoja ambae najua hela zake sio za kukwepa kodi kwamba "Kwa nini unajihusisha kutoa sana misaada wakati wewe ni tofauti na wengine sababu wengine hutumia hio njia kutakatisha fedha zao" akanijibu kuwa anataka angalau amani ya moyo tu.

Akaendelea kusema kwamba wote wanaomfahamu wanamuongelea mabaya nyuma ya pazia, leo akimsaidia mtu lakini kesho asipomsaidia basi ni maneno, na hayo yanasambazwa kwa wengine pia. Kwa hiyo ni bora akasaidie wasiomjua ili ku-counteract negative feelings zinazotokana na maneno anayosikia kwamba yeye ana roho mbaya.

Kimya kimya nikajisemea huyu jamaa hakupaswa kuwa tajiri, he's just too innocent for this shit.

Kama unatafuta utajiri kwanza hakikisha haujali chochote kuhusu kuchukiwa au kuongelewa vibaya la sivyo utajiri wako ndio utakua chanzo cha stress zako wakati lengo la utajiri ni kuwa free from everything even stress.
 
uwe maskini uwe tajiri lazima utasemwa tu kwa ubaya kwa uzuri lazima usemwe tu reaction yako ndo kila kitu
 
Back
Top Bottom