Ni kama vile Vunjabei anaelekea kufilisika

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
8,734
16,480
Nilikuwa Mbeya huko nikapita mitaa ile ya SIDO ni kama vile duka la Vunjabei linapumulia mashine, halina mzunguko wa biashara kivile.

Jana nimepita Iringa napo naona lile duka alilolifungua kwa mbwembwe nalo lishajifia na kufungwa muda tu.
Hapo Dar duka lake la Sinza nalo linapumulia mashine.

Ni kama vile jamaa kaanza kufilisika mdogo mdogo.

Nimeambatanisha picha za duka lake la Iringa lililofungwa.

IMG-20240906-WA0012.jpg
 
Ni kawaida kama umeshafanya biashara ama kuwa karibu na watu walofanya biashara. Kupanda na kushuka, na kupanda tena ama kushuka moja kwa moja. Upepo ukikubali unaweza shika hela hadi ukatamani kupiga nazo picha. ukiwa kichwa chepesi hauishi kuwa mitandaoni kupost mafanikio na lifestyle. Na upepo ukigoma utatamani malaika washuke waiizime mitandao. hutatamani kuona hata picha za moet ama Hennessy
 
Nilikua mbeya huko nikapita mitaa ile ya sido ni kama vile duka la vunjabei linapumulia mashine,halina mzunguko wa biashara kivile.
Jana nimepita iringa napo naona lile duka alilolifungua kwa mbwembwe nalo lishajifia na kufungwa muda tu.
Hapo dar duka lake la sinza nalo linapumulia mashine.
Ni kama vile jamaa kaanza kufirisika mdogo mdogo.
Nimeambatanisha picha za duka lake la iringa lililofungwa.
Ivumayo ....
 
Hii sasa ndio roho halisi ya mtu mweusi
Mtu mweusi na mambo ya uchumi wapi na wapi. Wazungu na uchumi wao wanazungumzia kukua na kushuka kwa biashara, wanajadili kuhusu inflation, kufirisika, kufa kwa kampuni, bailout, mergers and acquisition.

Sasa mweusi mwenzako akiuliza kwa muelekeo uleule unasema roho ya mtu mweusi. Wahindi, Waarabu, Wachina huwa hawajadili biashara. Au unataka weusi wasifie tu ila wasihoji, sasa si ujiuzie mwenyewe chumbani kwako. Kufungua uite media, mwenendo usiulizwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom