Ni Jambo la hatari kugeuza taasisi zote za serikali "watoza ushuru"

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Serikali ni chombo kilichopewa dhamana na wananchi kutumia rasilimali zao kuwaletea maendeleo.

katika kutimiza hili kuna taasisi ndani ya serikali yenye wajibu wa kukusanya mapato yatokano na kodi na tozo mbalimbali na kuingiza katika mfuko wa pamoja wa wananchi ambao ni hazina na humo serikali hutoa fedha hizo kutekeleza bajeti ya mwaka husika.

lakini pia kuna taasisi zenye wajibu wa kutumia fedha hizi za wananchi kutoa huduma mbalimbali katika jamii.

Hapa kunaonekana kutokea utata kwa kila taasisi ya serikali kuonekana kujikita katika kutoza ushuru na sio majukumu yao ya msingi.

mifano.

1. hivi karibuni tumekuwa tukipewa takwimu za jeshi la polisi limekusanya shilingi ngapi katika mwezi husika. jambo hili ni la hatari sana kwani ukusanyaji wa mapato kwa jeshi la polisi kunakinzana na majukumu yao ya msingi. kazi ya jeshi la polisi ni kuhakikisha usalama barabarani hivyo kupungua kwa matukio ya uvunjaji wa sheria barabarani ndio utendaji wa hali juu kutoka jeshi la polisi kitengo husika.

lakini unapolisifia jeshi la polisi kwa kiasi kikubwa cha fedha walichokusanya kutokana na makosa ya barabarani maana yake unageuza makosa haya kuwa mtaji na kamwe hakuna atakayekuwa na nia ya kuyaondoa bali kufanya hata yale yasiyokuwa makosa yaonekane makosa ili ushuru huu uendele kuongezeka na jeshi hili lionekane linafanya kazi.

ni jambo zuri kupiga faini makosa ili kuwafanya watumiaji wa barabara wawe makini lakini jambo hilo lingefanyika kwa utaratibu ambao faini hizi zinakwenda kwa mtoza ushuru moja kwa moja na huyu mwenye wajibu wa kulinda usalama barabarani yeye tumtathmini kwa record za matukio tu. yakipungua na tukaona mwenendo wa watumiaji wa barabara unabadilika basi ndio tunasema hawa wanatenda kazi.

2. Wizara ya ardhi imetangaza mkakati wa kutoza kodi kila kipande cha ardhi. Siku zote wizara hii imejikita kutoza ushuru na sio maendeleo ya makazi na miji. wao wanachokifanya ni kutoa hati kwa makazi holela ili yalipe kodi kuondoa makazi holela wanaona si jukumu lao.

Ki msingi arrangement ya makazi ndio msingi wa maendeleo katika miji, kuweka sheria na kanuni za makazi ndio msingi wa maendeleo. na wizara hii ilitakiwa kujikita kutoa huduma na kuweka mazingira ya taasisi husika ya kutoza kodi iwatoze kodi husika wananchi kulingana na sheria na taratibu tulizojiwekea. hawafanyi lolote lililo jukumu lao bali wako bize kila mtu alipe kodi ya ardhi.

Chukulia mfano mdogo tu, ipo miradi inayotekelezwa hapa nchi na serikali kupitia sekita binafsi, huko wanaajiri wataalamu wa kufanya survey kwa kuwalipa mishahara tena midogo, kila siku mtu akifika anashinda akizunguka mijini wakifanya survey karibia miji yote kila sehemu. wizara hii wakambiwa kusurvey na kupanga miji wanakuambia gharama ni kubwa kwa kiwanja kimoja almost laki mbili kama hakuna compensation. hiyo ni gharama eti ya kupanga mji kwa pamoja maana ukitaka kuhalalisha squarter yako ili ulipe kodi wanakubambikiza kana kwamba wako after business na sio kuwa na shauku ya kupanga mji wote ili kuweka msingi huo wa maendeleo ya makazi na nyumba.

bila hata ya kuwa na watu wanaozunguka mijini kufanya survey, mtu akikaa kwenye kompyuta na programu inayopatika free bila gharama yoyote (google earth) mtu anaweza kuutazama mji wowote na anaweza kuchukua picha ya eneo kuonyesha nyumba za mtaa, miji au anaweza kufanya survey kuchukua coordinates anazozitaka. lakini hawa utawaona wananunua sijui vindege vya kupiga picha, kutumia gharama kibao but nothing katika output.

ki msingi taasisi hii imejigeuza tawi la TRA na jukumu lake la msingi hakuna kinachofanyika.

Wizara ya nyumba na makazi ipimwe kwa upangaji miji yetu na katika kufanya hivyo iweke mazingira ya taasisi nyingie kufanya kazi. kama ni TRA wawekewe mazingira, kama ni watoa huduma wawekewe mazingira lakini sio wao kuibuka na kutoza kodi kutoza kodi.

waulize tanesco wanavyopata shida kusambaza umeme makazi holela, waulize watoa huduma za maji wanavyopata shida, waulize shirika posta wanavyoshindwa kupeleka huduma mpaka majumbani, waulize Tanroad na halmashauri wanavyohangaika kutengeneza barabara makazi holela, waulize wizara ya elimu inavyokuwa na shule vichochoroni hazina viwanja wala nini. hivi haya yote mnadhani tatizo litaondoka kwa kuwatoza kodi watu wanaojenga ovyo? au haya ni kutambua kuna tatizo katika upangaji na sio upimaji wa miji yetu. Ukipanga mji ukakaa vizuri ndio haya mambo yanakaa vizuri na ndio vigezo vya maendeleo ya makazi.

lakini inavyoonekana kila taasisi inajigeuza mtoza ushuru na kutizama kukusanya fedha, mambo mengine tunaendelea kuyafanya kwa mazoea. Kwa mtizamo wangu "something is blind somewhere"
 
Tunahitaji serikali makini inayokumbusha wananchi kutimiza wajibu wao kwa kuchangia mfuko wa pamoja yaani hazina lakini na yenyewe ikitambua kila sehemu wajibu wake.
 
Kila anayevuta oxygen kutozwa kodi! Huu nao si ubunifu?
 
Juzi kati nilienda taasisi moja ya serikali inahusiana na kukusanaya data, kampuni ninayofanyia kazi ilikua inahitaji hizo data, tukaambiwa tulipie dola mia moja ili tupewe hizo data. Mkurugenzi alituambia he is ashamed of the thing, but they have no option because wamepangiwa kiwango cha pesa na auditor atakuja kukagua.. Aibu kubwa mno, data zinaoaswa kuwa free lakini zinauzwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…