Ni ipi safari usiyoisahau?

kakah

New Member
Dec 27, 2022
4
5
Habari,

Miaka kadhaa iliyopita nilifanya safari amabayo nitaikumbuka kwa muda wote nitakao ishi hapa duniani,
Nimeamua kushare hii story kama ifuatavyo.

Miaka kadhaa nyuma nilikwenda mkoani Kigoma kufanya biashara ya kuuza vipuri vya magari, huu uamuzi nilifanya baada ya kufika mwaka mmoja kabla ya kuamua kuwekeza katika mkoa huo, ni baada ya kwenda kufanya matembezi ya mwisho wa mwaka na nilivutika hasa na mandhari mazuri ya mji huo, kuanzia hali ya hewa, na ufukwe mzuri wa ziwa tanganyika.

Nikatokea kupapenda hasa huo mji,
Na baada ya kufanya survey nikaja kuvutika na biashara ya vipuri na vilainishi.

Niliona kuna fursa katika nyanja hiyo,
Na baada ya kurejea mjini nikabahatika kupata connection ya mfanyabiashara amabae alikubali kunipa mzigo kwa mali kauli, na kwa wakati huo sikuwa na msingi wa kutosha,kiasi pekee nilichokuwa nacho ni hela ya frame na pesa ya kusafirisha mzigo kuuufikisha kigoma.

Kweli mwaka uliofuata nikaamua kwenda kujaribu bahati katika biashara hiyo, na baada ya kupewa mzigo wa kuanzia ambao ulikuwa na thamani ya milioni sita.

Kwakua sikua na msingi mkubwa nikaamua kufikia kwa jamaa ambaye alinikaribisha kwa mara ya kwanza nilipofika, mungu saidia biashara nikawa nafanya biashara ya kusambaza vilainishi(lubricants) katika maduka ya spare za pikipiki na magari, na baada ya wiki napitia mauzo, biashara hii nilifanya kwa miezi kadhaa bila kupata faida kwa sababu nilikuwa mgeni katika soko na pia sikuwa na ofisi zaidi ya chumba nilichopewa na mwenyeji wangu alikokuwa anakaa ikitumika kama stoo ya mzigo inapofika, na kwakua mzigo ilikuwa ni ya mali kauli ilitakiwa nirejeshe kwa wakati, ili nizidi kuaminiwa, yote hayo kupelekea kuuza bidhaa hizo kwa bei ya chini mno ili vitoke kwa haraka hapo profit margin ikiwa ndogo sana, basi katika heka heka za mjini hapo nikaja kujuana na mfanyabiashara mmoja wa kongo amabaye alikuwa na uraia wa marekani, alikuwa nikijana wa rika langu japo alikuwa ni raia wa us lakini tulikuwa na asili moja. Na baada ya kuonana mara kadhaa kwenye mgahawa mmoja hapo town, tukaja kuwa marafiki na kuwekana wazi mipango ya kila mmoja,
Akaniambia yeye amekuja kufanya survey ya biashara ya dagaa, baada ya kuona bidhaa hiyo inatembea sana katika mkoa aliyotokea, basi nikawa nampa ushirikiona na usaidizi katika survey huku tukitembelea baadi ya vijiji vya mwambao kujua AtoZ ya upatikanaji wa hizo dagaa.
Lakini kwa bahati mbaya msimu wa uvuaji kwa wakati huo ukiwa umedorora kwa sabau ya masika, na baada ya kufanya tafiti zaidi tukagundua hata dagaa za mwanza zitafaa baada ya kutuma sample ya magunia baadhi huko kongo na mrejesho kuwa mzuri tukaamua twende mwanza kufunga mzigo, na mimi nikaona huku kwenye udalali wa spare nitachelewa nikaona bora niingie katika fursa hii nione outcome yake, Nikampigia supplier wangu nikamueleza kuwa kipindi hichi ni cha masika na kama ilivyo ada biashara katika masika nchini inatoka kidogo kidogo kwa hivyo tuvumiliane na kweli kwa kipindi hicho muda mwingi nilikuwa natumia kwa katika kutemebea na boss wangu mpya nikawa sifatilia biashara ya vilainishi japo mambo hayakuwa vibaya kama nilivyodai.
Basi kufupisha stori tulienda mwanza mwaloni nakubahatika kununua dagaa mzigo wa kutosha tu lakini kwa kiwango tulichonunua hakikutosha kukodi semi ya pekee yetu tulilazimika kushare gari na wafanya biashara wengine, tukapata gari iliyokubali kupakia lkn kwa sharti ya kujaza nafasi yote iliyobakia, lkn kwa bahati mbaya mzigo tulionunua haukuweza kujaza nafasi iliyoachwa wazi na boss tayari pesa ishakata, akaniomba nimuazime pesa anunue mzigo wa kujazilia lile gari akiniahidi tutakapofika tunduma atanipa hela zangu, nikakubali kumuazima kwa sababu tulikuwa sote katika harakati na huko tunduma tunakwenda wote nikampa,
Na baada ya kukamilisha tukapanda basi mpka mbeya na kisha tunduma kusubiri mzigo, na baada ya siku tano gari ilikuwa bado halijafika tunduma, na ilitakiwa kufika siku mbili kabla, tukafanya mawasiliano na dereva akatuambia gari imepata hitilafu kwa hiyo mzigo utafaulisha kwenye gari nyingine tuvumilie, na kweli siku mbili baadae mzigo ukawa umefika tunduma, na baada ya kufika tukatafuta mahali pakuweka huku tukifanya maarifa ya kuvusha kwa njia za panya na baiskeli za hapo, baada ya kuhifadhi mzigo boss wangu akapata mzozo na uhamiaji wakidai passport yake haikugongwa exit alipotoka zambia, na baada ya mzozo mrefu na uhamiaji tukaenda mpk kwa incharge nakudai hapo custom si kuna cctv wa review recordings ya ile siku, watamuona, yeye alipita hapo nakumpa passport officer agonge ili aliamua kufanya uhuni kutokugonga, baada ya hoja hiyo wakamuacha tuendelee na mambo yetu,
Baada ya delay hiyo tukaanza process ya kusafirisha mzigo kwa baiskeli kutoa tunduma kuvusha kwenda nakonde upande wa zambia, zoezi hilo nikiwa incharge kwa sababu visa yake haikuwa ya biashara kazi zote hizo mimi nikiwa ndo main man katika process zote.
Mungu saidia tukafikisha whare house kubwa hapo upande wa zambia amabako mizigo inafikia na kusafirishwa hapo mpk kongo, na baada ya kufika kwenye warehouses hiyo tukaamriwa mzigo yote ipakiwe upya ili kuhakiki kilichomo ndani ndo chenyewe aiseeeeeee hiyo siku sintakuja kusahau, ili magunia yanakatwa na mzigo kumwagwa kwnye turubai ni mixer moja ya kishetani wametufanyia mzigo umechanganywa mafuru, dagaa za ukerewe na kidogo sana za dagaa za bukoba, wakati sisi tulinunua super ya bukoba grade 0ne, basi bwana weee tukapigwa na butwa kwa kile tulichokiona na ikapita masaa mawili hatusemezani tunaangaliana tu, na mzigo ukiwa chini, nilitamani ardhi ipasuke siku hiyo na jamaa alifura sana na walahakutaka kusema na mtu na baada ya kimya kingi akarudi tunduma hotelini, mimi nikaa hapo nakufanya uamuzi wa kiume nikanunua magunia mapya na kuyapeki na baada ya kuandikisha nikarudi tunduma, nikawa nawaza hii biashara si yangu na mimi japo ni mwenyeji hii biashara sikuwa na ujuzi nayo lkn mbona tulihakikisha mzigo tulinunua na mzuri tofauti na huo tuliouona,
Nikawaza tulipopigwa nikaona ni kazi bure maji yalishamwagika,
Na baada ya kimya kingi nikarudi gesti tuliyofikia nikamuita jamaa na kumueleza yaliyotikea yametokea.
Basi bwana nikauliza marejesho ya oesa nilizomuazima akasema atanipa kesho kutwa na kesho yake ataenda border congo kesho kutwa atarudi twende wote dar es salaam maana na yeye anasafari ya huko pia, kweli baada ya siku mbili nikapata whatsapp text inasoma,
Itaendelea

Wandugu,
Simunajua umeme wetu huu na mgao unaoendelea,

Basi bhana nimekaa zangu tundumu nakuta meseji ya whatsapp inasoma 'my friend go back where you came from)'
Nikamjibu 'what about my money' akanijibu 'becouse of you incompetent we have lost money, and as result you have to be accountable if i reccruit what i have invested i will send your money' nikamjibu 'thats not what we have agreed' akanijibu 'goodbye'
Nikasema hakuna haja ya kubishana maana fimbo ya mbali haiui nyoka, ngoja nifanye mpango niondoke zangu nisije kuaibika miji ya watu, sasa nitarudije gest nadai hela ya siku mbili @30,000 hela pekee ninayo 8000, nikasema shughuli ipo mara, sasa kwa nature yamgu kuomba ni jambo gumu sana kwangu, kwa sababu si mtu wa kampani, nikaamua haraka haraka nitafute mteja nimuuzie simu yangu sony xperia z1 kipindi hicho katika simu latest nayo ilikuwamo, mungu saidia nikapata mteja nikamuuzia 115000 faster nikaenda gesti nikalipa deni lao nikaamua kwenda booking office ya basi nikate ticket, lakini kwanza niende mgahawani nile lunch,
Nimefika mgahawani nikafua koti langu nikaweka kwenye kiti kwa mtindo wa kufisha kama hanger, aloo nimemaliza kula naenda kujisaidia narudi koti halipo kwenye kiti, nilichanganyikiwaje!, maana pesa zilizobaki kwenye mauzo ya simu niliweka kwenye mfuko wa koti. Tafuta koti mpk jikoni wapi sijui ndo kuchanganyikiwa, na simu tayari nilishauza nitamtafuta nani wa kunitumia hela, basi nikawaza nikawazua nitaondokaje hapa,
Basi bhana nikasema liwalo naliwe bhana nikaamka asubuhi nikatafuta basi nikapata siti ya reserve ile ya mbele basi la princess muro, kilichonisaidia ni lile begi langu lilikuwa nikubwa na huwa na mazoea ya na begi kubwa ikiwa na taulo, blanket dogo plus na nguo so begi langu huwa ni kubwa, konda akanipokea akaniwekea kwenye buti, huku mimi nikizuga zuga nje mpka gari likawa tayari kwa safari, sasa kimbembe kwenye kudai hela, najisachi sachi namwambia konda 'ah boss nimesahau wallet kwenye begi kubwa' basi akasema tukifika mbeya mjini atanikumbusha, kwa bahati nzuri njiani nikawa nawaza itakuwaje, kwa ule woga na hogu tumbo likawa limevurugika mpk ikabidi tusimame njiani humo maporini nijisaidie, tulivofika mbeya gari lilivyogika stand nikakimbilia chooni ili nimalize haja vzr kwa sababu wakati wa porini sikuwa comfortable na hayo mazingira, wadau si munajua tumbo likiwa linaendesha, nikiwa bado namalizia malizia nasikia honi la basi letu likiwa linapiga mara nyingi nikajua naesubiriwa ni mimi, basi kurudi kwenye basi pole nyingi konda akawa hana muda tena wakufungua mabuti, nikasema ashukuriwe mungu na safari ikaendelea kituo kinachofuata Makambako hapa konda moja kwa moja kwenye butu huku akiniita tall njoo unitolea hela yangu, maana hapo gari ilisimama tupate chai nalile baridi nikasema leo umekwisha wahenga hawakukosea kusema mbio za sakafuni huishia ukingoni, bhana bhana nikajikuta nimeingiwa na ujasiri faster nikashuka nikasema huyo bwashe hawezi kunizidi maarifa ngoja nimchezee mapichapicha atafurahi yeye mwenyewe,
Nikafungua begi nikawa najifanya nasachi sachi nikamwaga vitu vyote chini nikajikuta naropoka 'Kmmq' inamaana nimesahau wallet yangu gesti' konda nae akawa anawaka hayo mambo ya kingese siyataki kusikiwa hela iko wapi, kukazuka mgogoro mkubwa pale chini ikabidi abiria wengine,
Akatokea mzee mmoja nakutuamulia maana konda na dereva walishaamua kunishusha palepale. Mzee akasema huo si uungwana maana kwa haiba na muonekano nilionekana mtu mwenye heshima yake kwa hiyo wasiniache mzee yule alikuwa msaada kwangu na akashauri niwatafute kwenye simu wanitumie hela, nikawajibu simu nilisahau siku tatu nyuma kwenye bajaji za tunduma, yule mzee akasema wewe mtu mzima bhana huwezi kukosa namba mbili tatu ulizohifadhi kichwani, nikasema mambo yasiwe mengi nikawajibu nina namba ya mke wangu nitampigia atanitumia hiyo nauli, konda akadai nimpe hiyo namba kwenye simu yake ampigie, nikamtajia namba yangu maana kwa wakati ule sikuwa na mke wala mtu niliyehifadhi namba yake kichwani, nikijua fika akipiga hiyo namba itakuwa haipatikani, safari ikaendelea huku konda akipiga piga kila mara ile namba, lkn ikawa haipatikani, yule bwana akawa anabwata sana mule kwenye gari abiria wakimpooza kuwa nijambo lakawaida simu kutopatikana maana inaweza kuwa imeisha charge, tukavuka iringa salama salimini lakini maneno ya shombo yakiwa mengi huku abiria wakiwa wanazozana na yule konda kwa jinsi alivyokuwa ana ni harass, tukafika mikumi gari ikasimama kwawauza mishikaki wa pale konda akiwa amechachamaa kweli, akatokea abiria mmoja akawaambia wale abiria wengine jamani huyu ni msafiri mwenzetu na hichi anachopitia kinaweza kumtokea yeyote kati yetu, kwanini tusichange mwenye buku mwenye buku mbili tumchangie aepukane na kejeli za huyo konda, basi yule bwana alikuwa mwokozi wangu ikapigwa michango mimi mwwnyewe nikiwa napita sitti moja baada ya nyingine huku nikiwa mnyoonge kabisa nakusanya michango, kwa jinsi nilivyokuwa nimefadhaika mtu mwenye imani usingeshindwa kunisaidia nikapata nauli na ziada ya elfu 12,000 nikawwaambia abiria kile kilichobaki wakasema hiyo nyinge nitafanya nauli nikifika ubungo, basi hiyo ikawa salama yangu.

Kuhusu yule boss wetu wa kongo alinitafuta baada ya wiki mbili nakunitumia robo tatu ya pesa niliyomuazima na nyingine akaahidi atanitumia,
Na baada ya muda alinipigia tena akaniambia anarudi kwao mambo yamemuia ngumu, akinihadithia jinsi alivyokuja kongo alifungua machimbo madogo ya shaba lakini hakufua dafu na baada ya kuona amefilisika akaona ajitupe kwenye biashara ya uchuuzi wa samaki labda ataibuka kwenye hiyo biashara mpk nako tulipopigwa na kitu kizitoooooo mno.
Nikampa pole nakumtia moyo asikate tamaa aendelee kupambana, na baada ya hapo nikamuambia kiasi kilichobaki nimemsamehe na yeye akaniambia anarudi us maana pesa imekata, nakuahidi atanatafuta akishafika,
Na upande wangu ile biashara ya spare na vilainishi ikawa imekufa baada ya supplier wangu kuona nimechelewesha marejesho,

Huyo jamaa yetu alikuwa ni mwafrika mwenzeto wa ukanda huu ila alipata urai wa marekani, maana wabomgo hatuchelewi kusema mzungu na dagaa wapi na wapi, mukanitupia vikombe vingi
 
Habari,

Miaka kadhaa iliyopita nilifanya safari amabayo nitaikumbuka kwa muda wote nitakao ishi hapa duniani,
Nimeamua kushare hii story kama ifuatavyo.

Miaka kadhaa nyuma nilikwenda mkoani Kigoma kufanya biashara ya kuuza vipuri vya magari, huu uamuzi nilifanya baada ya kufika mwaka mmoja kabla ya kuamua kuwekeza katika mkoa huo, ni baada ya kwenda kufanya matembezi ya mwisho wa mwaka na nilivutika hasa na mandhari mazuri ya mji huo, kuanzia hali ya hewa, na ufukwe mzuri wa ziwa tanganyika,.
Nikatokea kupapenda hasa huo mji,
Na baada ya kufanya survey nikaja kuvutika na biashara ya vipuri na vilainishi,
Niliona kuna fursa katika nyanja hiyo,
Na baada ya kurejea mjini nikabahatika kupata connection ya mfanyabiashara amabae alikubali kunipa mzigo kwa mali kauli, na kwa wakati huo sikuwa na msingi wa kutosha,kiasi pekee nilichokuwa nacho ni hela ya frame na pesa ya kusafirisha mzigo kuuufikisha kigoma,

Kweli mwaka uliofuata nikaamua kwenda kujaribu bahati katika biashara hiyo, na baada ya kupewa mzigo wa kuanzia ambao ulikuwa na thamani ya milioni sita,
Nikafika s. I lama na baada ya mzigo..
eeeh, imeisha hiyoo
 
Safari ya kwenda Bukoba ukweni kwao na mamdg eeeh. Huko njian gari lilizama kweny tope kheeeeeh tulipita kijijini fulani huko njian njian.
 
Shinyanga kampala . Picha linaanza tukaweka lamination kwenye vile vibali vya kusafiria vya mwaka mmoja ( East and Central Africa).Yellowfever vacination pale jirani na makongoro pharmarcy nayo ikawa mtiti . Boda ya mitukula visanga vingi vinatokea .
Siku inayofuata tunaingia Champala na link basi ( wenyewe hupaita ivo).Tunapiga root za kutosha na boda boda jion tunaambiwa tulipe 40k ya M7, kwa msaada aliotupa Kijana junior ( Bodaboda).Tunampa 50k kabisa .
KIUFUPI NITAILETA KAMA STORY YANGU PIA .KOKOTE MLIKO HILDA KAMILE NA KUDRAT ( UBINI WA MZEE WAKO NIMEUSAHAU).NA GODFREY MUSHI TUWASILIANE JAMANI
 
Back
Top Bottom