Ni fedhea Viongozi wa CCM kuandaa zoom meeting kuwajadili machinga. Ni Machinga gani ana muda wakuingia zoom kushiriki mjadala?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,984
Nimeana Zungu na wengine wameitisha mkutano kupitia Zoom kujadili kadhia ya machinga kuondolewa baadhi ya maeneo kwa lengo lakutaftiwa maeneo mengine.

Swali ninalotaka kujiuliza, hiki kiburi cha hawa viongozi kwenda Zoom kuwajadili machinga wanakitoa wapi?

Kwamba walishindwa kuwatetea Bungeni, kwenye mabaraza ya halmashauri na hata kwenye mikutano ya adhara au kupitia vyombo vya habari hadi waamue kuwashughulikia kupitia Zoom?

Wameenda zoom kukwepa covid, kukwepa gharama au zoom wamekwenda kwa lengo lipi mahsusi?

Yupo mtu anagombanishwa na wananchi bila yeye kujua kwamba anagombanishwa. Mawaziri zoom, viongozi wa bunge zoom?

Basi sawa tuendelee zoom
 
Hapo kungekuwa na posho wala hiyo zoom wasingetumia, mbona mbunge hawataki liendeshwe kwe zoom meeting na wakati wote wana tablets?
 
Nchi ya Marekani imepiga hatua kubwa kimaendeleo lakini mpaka leo changamoto za kimaendeleo bado zipo!
Ni kweli changamoto haziishi ila sio kwa Tanzania. Maendeleo tuliyopaswa kua nayo kwa miaka 60 hii ya uhuru sio haya.

Ni sawa na mtoto ama kijana wa miaka 15 kukuta anafanya mambo sawa na mtoto wa miaka 3 ama 4, huyo anakua hajakua.

Tanzania maendeleo tuliyo nayo sasa tulipaswa kua nayo miaka 20 iliyopita ila kwa sababu ya sera mbovu za ccm, sera zisizoeleweka ndio maana tuko hapa.

CCMs wametawala hii nchi kwa miaka 60, hawana kipya tena cha kuiifanyia hii nchi tena.
 
OK noted

Lazima tuendane na teknolojia, Kwa sasa mikutano mingi inafanyika zoom

Halafu mambo ya CCM hayajadiliwi kwa kutumia nguvu na kufoka foka

Kufoka foka ni kazi ya Serikali ambayo inasimamiwa na ccm

Wale sio machinga, Waliondolewa ni wafanyabiashara wadogo wenye mitaji ndio maana una kuta kuna vibanda vina Bidhaa ya zaidi ya Milioni 200

Wamachinga unafahamu maana yake, Machinga au chinga kazi yao wao ni kuzurula na Bidhaa, Hawakai sehemu moja. Ndio asili ya machinga

Hao Waliondolewa sio machinga bali walijificha ndani ya neno machinga kwa kujenga vibanda

Machinga kama machinga wapo na bado wanazunguka na Bidhaa zao mitaani

Kuna uhusiano gani kati ya CCM na Machinga?

Kuna uhusiano gani kati ya Chadema na Ugaidi?

Kwa ufupi unachanganya sana mambo kwa kuwa na hasira, CCM ipo ilikuwepo na itakuwepo

Kabla ya vyama vingi wote hao unaowaona Chadema, NCCR walikuwa na kadi za ccm, Kwanini walishindwa kudhibiti hao machinga kutoka huko Mtwara na Lindi nakuja kujaa Dar es Salaam Mbagala

Wewe na Mimi wote ni watunga sera, Tuliichagua ccm wenyewe kwa ridhaa yetu na kushangilia ushindi inakuwaje ukinyimwa Teuzi unalialia hapa JF

Sheria zote zinapitishwa bungeni, Mimi na wewe ni wadau wakuu kwani tunapewa fursa za kutoa maoni yetu, Mbona hutoi maoni yako wakati wa mchakato?

Baada ya miezi kadhaa ijayo tutakuona hapa JF unalalamika pesa za uviko 19 toka IMF zimepigwa na watu, Wewe nani amekukataza kupiga hizo Hela wakati una taarifa mzigo umeshaingia mjini inabidi utumike. Itakuwa vituko na vichekesho wewe kushindwa kutumia connection Nasema koneksheni kupata channel za huu mzigo wa IMF. Utakuja hapa oooh ccm wamepiga pesa, oooho madarasa hayana viwango. Wewe unataka watu wale wapi?
 
CCMs hata wakipewa miaka 800 hii nchi maendeleo bado tutaendelea kuyasikia redioni.
Umasikini ni LAANA na TANZANIA ni MASIKINI hivyo ina LAANA hivyo Kupata Maendeleo ni NDOTO za Mchana TANZANIA HAITAKUJA KUENDELEA KAMWE tutaishia kujenga Vyoo Madarasa na zahanati
 
Back
Top Bottom