Ni dhahiri kuwa Binti alikuwa anakutanishwa na Baba mzazi kwa kificho

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
4,023
14,177
Kuna uzi unasema kuwa Baba wa kambo kalea binti mpaka kawa mtu mzima lakini Binti alipotaka kuolewa mahari akasema apewe Baba yake mzazi na sio wa kufikia.

Uzi wenyewe huu hapa Tumsaidie huyu kimawazo

Ngoja niwaambie kitu ambacho hamkijui,

Ukioa Mwanamke mwenye mtoto kuna asilimia 90% kuwa Baba wa kambo unazungukwa/kudanganywa na Single mother.

Wakati wewe unalea na kugharamika nyuma ya pazia Baba mzazi nayeye anatoa pesa na kumgharamia mwanae, chochote unachoambiwa na Single mother ni uongo anakujaza ili uendelee kuwahudumia nayeye aendelee kupokea kote kote,
kwa Baba mzazi na wewe Baba wa kufikia.

Kuna kipindi single mother atakwambia sipokei hata sumni kumbe nyuma ya pazia anapokea hela na anamkutanisha mwanae na Baba yake bila yawewe kujua.

Kwa kisa cha huo uzi nina uhakika kuwa binti alikuwa anakutanishwa na Baba yake na alikuwa anaonyeshwa mapenzi na Baba mzazi wake.

Isingekuwa rahisi binti kusema mahari apatiwe Baba mzazi wakati huyo Baba hakuwapo kwenye maisha yake kabisa.

Ushauri: Kijana pambana utafute Mwanamke fresh ili kuepuka maumivu yanayoweza kuzuilika.
 
Kuna uzi huu hapa Tumsaidie huyu kimawazo

Uzi unasema kuwa, Baba wa kambo kalea binti mpaka kawa mtu mzima lakini Binti alipotaka kuolewa mahari akasema apewe Baba yake mzazi na sio wa kufikia.

Ngoja niwaambie kitu ambacho hamkijui,

Ukioa Mwanamke mwenye mtoto kuna asilimia 90% kuwa Baba wa kambo unazungukwa/kudanganywa na Single mother.

Wakati wewe unalea na kugharamika nyuma ya pazia Baba mzazi nayeye anatoa pesa na kumgharamia mwanae, chochote unachoambiwa na Single mother ni uongo anakujaza ili uendelee kuwahudumia nayeye aendelee kupokea kote kote,
kwa Baba mzazi na wewe Baba wa kufikia.

Kuna kipindi single mother atakwambia sipokei hata sumni kumbe nyuma ya pazia anapokea hela na anamkutanisha mwanae na Baba yake bila yawewe kujua.

Kwa kisa cha huo uzi nina uhakika kuwa binti alikuwa anakutanishwa na Baba yake na alikuwa anaonyeshwa mapenzi na Baba mzazi wake.

Isingekuwa rahisi binti kusema mahari apatiwe Baba mzazi wakati huyo Baba hakuwapo kwenye maisha yake kabisa.

Ushauri: Kijana pambana utafute Mwanamke fresh ili kuepuka maumivu nayoweza kuzuilika.
Ila single moms, labda baba mwenye mtoto awe amekufa.
 
Ila nyie mnaruhusiwa kuwa single baba na muoe wanawake wasio na watoto.

Hata aibu hamuoni..,

Wanaume acheni ubinafsi...
Itokee mwanaume wako unayekutana nae anakuwa amezaa huko nje halafu uletewe hao watoto wa mwanamke mwenzako ambaye amezaa na huyo mwanaume wako uishi nao kama wakwako kama mama yao, uwalipie ada uwalishe, uwavalishe, wakiumwa uwahudumie na kuhangaikia nao kwa kutumia pesa yako ya mshahara wako binafsi, uwatoe out kwa gharama zako, halafu mwisho wa siku huyo baba watoto awe na mawasiliano na mwanamke aliyewazaa nae watoto hao na awe anawaulizia kuwasalimia na muda mwingine anaomba waende kumsalimia na kulala huko huko na baba yao, vipi hiyo utakubaliana nayo kwa moyo mkunjufu?

Kumbuka pesa inayotumika ni ya mshahara wako mwanaume hana kazi wewe ndio unamuweka mjini hakuchangii hata mia kwenye shughuli zote hizo.
 
Mtoto sio wako unataka mahari ya nini! Kwanza mtu atake mahari ya binti yeye ndiyo anaolewa! Mambo mengine ni kukidhalilisha tu.
Unapokaa na mwanamke mwenye mtoto mwisho wa kumsapoti kama mlemavu wa mahusiano ni hadi watoto wanapofika miaka saba baada ya hapo pigia simu huyo mwanaume itisha kikao aje kuchukua mtoto wake au watoto wake akalee huko mwenyewe maana ni damu yake atajua pa kuipeleka.

Mwanamke akileta fyoko mwambie aende na huyo mwanaume huko akalee watoto.
 
Kuna single maza alikua anajfny anakuja kulala kwangu cjui mara afue apike uku akinambia baba watoto alitorokea mwanza na mtot mwngn babayake hamuhudumii, mm nlivopg game nkamsepa ila baadae nkaja kugundua anahudumiwa na wanaume zake wote wawil so guys stay away from single maza
 
Unapokaa na mwanamke mwenye mtoto mwisho wa kumsapoti kama mlemavu wa mahusiano ni hadi watoto wanapofika miaka saba baada ya hapo pigia simu huyo mwanaume itisha kikao aje kuchukua mtoto wake au watoto wake akalee huko mwenyewe maana ni damu yake atajua pa kuipeleka.

Mwanamke akileta fyoko mwambie aende na huyo mwanaume huko akalee watoto.
Unamuoa wann single maza acha ubwege yan ungekua karibu ningekunasa kibao akili ikae sawa
 
Kuna uzi unasema kuwa Baba wa kambo kalea binti mpaka kawa mtu mzima lakini Binti alipotaka kuolewa mahari akasema apewe Baba yake mzazi na sio wa kufikia.

Uzi wenyewe huu hapa Tumsaidie huyu kimawazo

Ngoja niwaambie kitu ambacho hamkijui,

Ukioa Mwanamke mwenye mtoto kuna asilimia 90% kuwa Baba wa kambo unazungukwa/kudanganywa na Single mother.

Wakati wewe unalea na kugharamika nyuma ya pazia Baba mzazi nayeye anatoa pesa na kumgharamia mwanae, chochote unachoambiwa na Single mother ni uongo anakujaza ili uendelee kuwahudumia nayeye aendelee kupokea kote kote,
kwa Baba mzazi na wewe Baba wa kufikia.

Kuna kipindi single mother atakwambia sipokei hata sumni kumbe nyuma ya pazia anapokea hela na anamkutanisha mwanae na Baba yake bila yawewe kujua.

Kwa kisa cha huo uzi nina uhakika kuwa binti alikuwa anakutanishwa na Baba yake na alikuwa anaonyeshwa mapenzi na Baba mzazi wake.

Isingekuwa rahisi binti kusema mahari apatiwe Baba mzazi wakati huyo Baba hakuwapo kwenye maisha yake kabisa.

Ushauri: Kijana pambana utafute Mwanamke fresh ili kuepuka maumivu yanayoweza kuzuilika.
Hayo maneno waweza kuwa umeyapima sawa sawa kabisa.

Lakini bado tu huyo binti ana dosari tena kubwa.

Katika malezi na makuzi, hauwezi kuoneshwa upendo wa kilaghai wa vipipi na vizawadi eti ukasema umeoneshwa upendo halisi na kumuona aliyekutunza na kukusomesha hakukupenda na hakufai kwa lolote!

Mifano ya hivyo ipo na nimeishuhudia, lakini mwisho wa kijana huwa ni mbaya maana ni laana anakuwa kajitafutia, tena kwa kujua kabisa
.
Tukisema kuwa binti huyo ni mwizi wa fadhila tutakuwa tumekosea?
 
Acha uzwazwa, kila mtu natabia zake pia kumbuka watu hubadilika. Kila mwanamke anaupumbavu wake jua hilo ndgu. Kama umekutana na mjinga atabaki na ujinga wake milele na knyume chake ni kweli.

Wendawazimu kibao tunaishi nao bila kujua.
Sasa omba Mungu usiowe mwendawazu utawachukia wanawake wote, na n vyema ukajitambua kama wewe ni mwendawazimu au la.

Pia tambua mzinifu mwanaume ataoa mzinifu mwanamke. Huwezi kua fresh up steres ukaparamia single mother, wengi ni kutokana na matatizo kubwa n maradhi hasa ukimwi. Fatilia utajua hili, wengi walioathirika huponea kwa hawa kwani hujilahisi na hawana cha kupoteza.

Wapo single mothers kibao wameolewa na wanawaheshimu waume zao. Mtoto kumjua au kuwasiliana na baba yake si kosa. Kosa ni ujuha wa wewe kutokujua level ya uwendawazimu wao.

Amini hakuna mtu anaejielewa( si kichaa) anaeweza anzisha mahusiano na mke au mume wa mtu. Jitambue wewe ili uweze kuishi maisha mema katika dunia hii ilojaa vichaa.
 
Mtoto sio wako unataka mahari ya nini! Kwanza mtu atake mahari ya binti yeye ndiyo anaolewa! Mambo mengine ni kujidhalilisha tu.
Thinking Capacity ndio tatizo hapa

Suala hapo sio mahari (Pesa) bali uthamani nyuma ya hio mahari, kusema apple baba mzazi ni kuto kujua umuhimu wa mlezi, hii hata ingekuwa ni karatasi tu tuseme Barua, mwanaume kaleta barua then Binti aside staking mlezi aside bali baba mzazi still mada ingeletwa hapa.
 
Ila nyie mnaruhusiwa kuwa single baba na muoe wanawake wasio na watoto.

Hata aibu hamuoni..,

Wanaume acheni ubinafsi...
Nyie mnaruhusiea kutokuwa na pesa na kuwa na mwanaume mwenye pesa

Hata album hamuoni
 
Itokee mwanaume wako unayekutana nae anakuwa amezaa huko nje halafu uletewe hao watoto wa mwanamke mwenzako ambaye amezaa na huyo mwanaume wako uishi nao kama wakwako kama mama yao, uwalipie ada uwalishe, uwavalishe, wakiumwa uwahudumie na kuhangaikia nao kwa kutumia pesa yako ya mshahara wako binafsi, uwatoe out kwa gharama zako, halafu mwisho wa siku huyo baba watoto awe na mawasiliano na mwanamke aliyewazaa nae watoto hao na awe anawaulizia kuwasalimia na muda mwingine anaomba waende kumsalimia na kulala huko huko na baba yao, vipi hiyo utakubaliana nayo kwa moyo mkunjufu?

Kumbuka pesa inayotumika ni ya mshahara wako mwanaume hana kazi wewe ndio unamuweka mjini hakuchangii hata mia kwenye shughuli zote hizo.
umempa swali zito mno. hakika kwa ukweli wa nafsi yake hawezi kukujibu labda aamue kudanganya tu hapa. ila jibu lake tunalijua.
 
Back
Top Bottom