milele amina

JF-Expert Member
Aug 16, 2024
2,800
4,114
Ni bora kuruhusu maandamano kuliko hali ilivyo sasa nchini. Maandamano ni njia muhimu ya kuwakilisha hisia na malalamiko ya wananchi. Hata hivyo, kuna hisia kwamba watu sasa hawataki kusikia kuhusu Nyerere, hasa kutokana na masuala ya muungano. Hii inadhihirisha jinsi mabadiliko ya kisiasa na kijamii yanavyoweza kubadilisha mitazamo ya watu.

Katika mazingira ambayo raia wanahisi hawana sauti, kuna hatari ya kutokea machafuko na kukosekana kwa amani. Ni muhimu kwa viongozi wa serikali kukubali kwamba kuna hisia tofauti na kutafuta njia za kuwezesha majadiliano.

Kama serikali inajaribu kupuuza upepo, ni vigumu kudumisha amani bila kukubali ukweli wa hali ilivyo. Kila mtu anapaswa kuwa na nafasi ya kutoa mawazo yake bila hofu. Hali ya sasa inaweza kupelekea kukosekana kwa umoja na ushirikiano katika jamii.

Kwa hivyo, ni vyema kuimarisha haki za raia na kuruhusu maandamano kama njia ya kujenga taifa lenye mshikamano na maelewano.
IMG-20240921-WA0086.jpg
 
Mama Raisi wangu mpendwa Sina cheo chochote serikalini,Sina kipato Cha kuridhisha,kunipa jeuri yoyote mbele ya wenye pesa na jeuri,nikuombe mama Samia,maoni yangu na hisia zangu,yaruhusu maandamano ya wapinzani watoe ya moyoni mwao,baada ya hapo upande unaonyoshewa vidole ukubali kujisahihisha, ikitokea ukazuia maandamano hayo,hasara ni nyingi na image ya nchi itachafuka zaidi
 
Hajali swala la image mwenzako
 
Ni bora kuruhusu maandamano kuliko hali ilivyo sasa nchini. Maandamano ni njia muhimu ya kuwakilisha hisia na malalamiko ya wananchi. Hata hivyo, kuna hisia kwamba watu sasa hawataki kusikia kuhusu Nyerere, hasa kutokana na masuala ya muungano. Hii inadhihirisha jinsi mabadiliko ya kisiasa na kijamii yanavyoweza kubadilisha mitazamo ya watu.

Katika mazingira ambayo raia wanahisi hawana sauti, kuna hatari ya kutokea machafuko na kukosekana kwa amani. Ni muhimu kwa viongozi wa serikali kukubali kwamba kuna hisia tofauti na kutafuta njia za kuwezesha majadiliano.

Kama serikali inajaribu kupuuza upepo, ni vigumu kudumisha amani bila kukubali ukweli wa hali ilivyo. Kila mtu anapaswa kuwa na nafasi ya kutoa mawazo yake bila hofu. Hali ya sasa inaweza kupelekea kukosekana kwa umoja na ushirikiano katika jamii.

Kwa hivyo, ni vyema kuimarisha haki za raia na kuruhusu maandamano kama njia ya kujenga taifa lenye mshikamano na maelewano.View attachment 3102300
Huu ni muendelezo wa ndoto na matamanio ya nafsi zenu. Kimsingi Maandamano yalishazimwa kitambo tu. Tarehe 23 Sept ni sku kama siku nyengine, inategemea na hali ya hewa ya nchi, mawio na machweo. Poleni sana kwa ukweli huo ulio mchungu kwa baadhi yenu.
 
Safi Sana, halina faida,
Leo nimeona polisi wengi Sana wamekaa kihasara hasara maeneo ya Oyster Bay Dar, nikaenda kukaa kwa mama ntilie nipate msosi,nikakuta Afande mmoja yupo bize na simu,
Nikaagiza msosi, Yule Afande akamuita Muhudumu, akamuuliza kwa sauti ndogo, "eti kwa buku tatu, naweza kupata chakula gani,? Pilau, au, ugari na kuku? "
Ile sehemu ni mabanda tu, msosi ni nafuu Sana, hawa askari wa samia, ni, wa kuonea huruma Sana,
Wengi wamekuja Dar Kenya study your,
 
Siyo kuhusu, kuandamana ni haki wala haiombwi inawafahamisha polisi na wao wanajua wajibu wao
 
Huu ni muendelezo wa ndoto na matamanio ya nafsi zenu. Kimsingi Maandamano yalishazimwa kitambo tu. Tarehe 23 Sept ni sku kama siku nyengine, inategemea na hali ya hewa ya nchi, mawio na machweo. Poleni sana kwa ukweli huo ulio mchungu kwa baadhi yenu.
Unaweza ukachukulia haya mambo kawaida sana Ila kiukweli mambo kwa ground ni moto sana na tena walichokosea serikali ni kuruhusu hii boycott ya Maaskari Dar nzima………HiI imewapa CHADEMA umaarufu,ata Kama mtu alikuwa hana Habari na maandamano,anakwenda kuwa na taarifa

Mpaka 2025 CCM watakuwa na hali mbaya sana
 
Ni bora kuruhusu maandamano kuliko hali ilivyo sasa nchini. Maandamano ni njia muhimu ya kuwakilisha hisia na malalamiko ya wananchi. Hata hivyo, kuna hisia kwamba watu sasa hawataki kusikia kuhusu Nyerere, hasa kutokana na masuala ya muungano. Hii inadhihirisha jinsi mabadiliko ya kisiasa na kijamii yanavyoweza kubadilisha mitazamo ya watu.

Katika mazingira ambayo raia wanahisi hawana sauti, kuna hatari ya kutokea machafuko na kukosekana kwa amani. Ni muhimu kwa viongozi wa serikali kukubali kwamba kuna hisia tofauti na kutafuta njia za kuwezesha majadiliano.

Kama serikali inajaribu kupuuza upepo, ni vigumu kudumisha amani bila kukubali ukweli wa hali ilivyo. Kila mtu anapaswa kuwa na nafasi ya kutoa mawazo yake bila hofu. Hali ya sasa inaweza kupelekea kukosekana kwa umoja na ushirikiano katika jamii.

Kwa hivyo, ni vyema kuimarisha haki za raia na kuruhusu maandamano kama njia ya kujenga taifa lenye mshikamano na maelewano.View attachment 3102300
Kabisa!
 
nashauri wawaruhusu tu, wala wasiwazuie. hawataiba, hawatafanya chochote. ila baada ya maandamano atakayeendelea kukaidi huyo anatafuta ugomvi wa peke yake sasa
 
Hakika Mama Samia Rais wetu epusha balaa kwa kuruhusu maandamano na baadae wahusika wa utekaji na mauaji wawakamatwe na watendaji walioshindwa kuzuia mauaji na utekaji wawajibike. Hawa watu wanaomboleza na ikitokea maafa tena au majeruhi itakuharibia zaidi kutokana na uungwana uliouonyesha tangu mwanzo Machi 2021. Polisi wao hawana cha kupoteza maana watadai wanafuata maagizo ya Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa Nchi kwa mujibu wa viapo vyao. Mungu akupe hekima ufanye uamuzi wa kuepusha shari na balaa katika Uongozi wako.
 
Safi Sana, halina faida,
Leo nimeona polisi wengi Sana wamekaa kihasara hasara maeneo ya Oyster Bay Dar, nikaenda kukaa kwa mama ntilie nipate msosi,nikakuta Afande mmoja yupo bize na simu,
Nikaagiza msosi, Yule Afande akamuita Muhudumu, akamuuliza kwa sauti ndogo, "eti kwa buku tatu, naweza kupata chakula gani,? Pilau, au, ugari na kuku? "
Ile sehemu ni mabanda tu, msosi ni nafuu Sana, hawa askari wa samia, ni, wa kuonea huruma Sana,
Wengi wamekuja Dar Kenya study your,
Tusiwalaumu kabisa Polisi hao ni Ndugu zetu, inawezekana mambo mengine hawapendi lakini ndivyo viapo vyao vinavyosema kutii amri. Labda sasa wao nao watumie busara ya kutoumiza watu wasiofanya fujo yoyote. Njaa na shida wanakumbana nayo kama Watanzania wengine na inawezekana wanatamani mabadiliko ili maisha yawe mazuri zaidi.
 
Waliovunja hiyo sanamu ni wahalifu kama wahalifu wengine. Dola itashughulika nao. Imefikia sehemu hata mkigongewa wake zenu mtalaumu serikali. Acheni upuuzi.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Mliruhusuwa kufanya maandamano na mkafanya na mikutano mkafanya.
Tatizo mkageuza maandamano na mikutano kama,forums za kutukana matusi ya nguoni kwa viongozi na,wale wote wasiokubaliana na nyie.
Lugha za,matusi mlionywa mkaendelea kama watoto waliodekezwa na kukosa maadili.
Sasa mnadai haki ukidai haki jua pia kuna wajibu.
Siasa za kistaarabu ndio zitajenga Nchi hii lakini tatizo mmeona ustaarabu ni udhaifu.
Mlifanya hivyo hivyo enzi za Urais wa Kikwete. Mkafyata enzi za Magufuli hata kukimbia Nchi licha ya kuwadanganya wafuasi wenukwamba dhambi kubwa ni uoga.
Andamana ushughulikiwe.
 
Back
Top Bottom