GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 6,819
- 9,649
Introvert wa JF mpoo! Unafahamu thamani ya uintrovert wako?
Kuwa introvert si ugonjwa. Nibaraka, lakini ukijitambua na kujikubali. Vinginevyo, unaweza ukawa sawa na mtu anayetaka kubadilishana kilo kumi za dhahabu kwa kuku kumi wa mayai! Hasara iliyoje!
Jamii yetu, kwa kutokufahamu, wamekuwa wakiwalaumu introvert kwa kutokuwa extrovert. Kuna wanaofikiria wana viburi,, wengine wanafikiri ni waoga, wengine wanawaona kama ni watu wanaojisikia, n.k. Hawajui kuwa wao ndiyo "wajinga", kwa kushindwa kujua utofauti wa maintrovert an extrovert.
Mungu, kwa nia njema kabisa, kaona vyema watu wawe na "personality" tofauti. Wewe unafikiri ingekuwaje kama dunia nzima ingekuwa ni ya maextrovert pekee? Au unafikiri ingekuwaje kama watu wote wangekuwa ni maintrovert?
Kama ambavyo Mungu kaamua kututofautisha, tuzikubali hizo tofauti na tuzitumie kwa manufaa. Wazazi wenye watoto maintrovert waache kuwalazamisha kuwa extrovert, badala yake wawasaidie kuvuna manufaa ya kuwa introvert.
Kwa wasiofahamu, kuwa introvert si ugonjwa. Ni namna ubongo unavyochakata taarifa zinazotumwa kwake. Kwamba, kiwango cha "dopamine" na muundo wa "dopamine receptors" kwenye ubongo ndiyo humtofautisha Introvert na Extrovert.
Tafiti za Kisayansi zinaonesha kuwa mtu anaweza kubainika kama ni introvert au extrovert akiwa na umri wa kuanzia miezi minne.
Kwa wasiojua, hizi ni baadhi ya tabia za Introverts:
~ Wakiamya
~ Wanapenda mazingira ya kuwa peke yao - hawafurahii mazingira ya mchanganyikeni
~ Wanapenda mazingira ya ukimya
~ Hufikiri kabla ya kuongea
~ Wana kawaida ya kuwa na marafiki wachache
~ Ni wasiri sana, n.k. (wengine wataongezea).
Baadhi ya watu maarufu ambao ni Introverts:
1. Warren Buffett
2. Mark Zuckerberg
3. Bill Gates
4. Steve Wozniak
5. Larry Page
6. Michael Jordan
7. Elon Musk
8. Charles Darwin
9. Mahtma Gandhi
10. Al Gore
11. Sir Isaac Newton
12. Rosa Parks
13. Eleanor Roosevelt
14. Abraham Lincoln
15. Barack Obama
16. Marissa Mayer
17. Guy Kuwasaki
18. Hilary Clinton
19.Michael Jackson
20. Brenda Barnes, e.t.c.
Nafikiri, na hawa Watanzania nao ni introvert: Dr. Mohammed Gharib Bilal, Dr. Ally Mohammed Shein, Dr. Philip Mpango, n.k.
Introvert, umebarikiwa kuwa introvert! Usitamani kuwa extrovert!
Extrovert, hakuna hasara kuwa Extrovert! Usiigize kuwa introvert!
Kila mmoja akae kwenye nafasi yake!!!