Ni aina gani nzuri ya Baiskeli kwa Ajili ya Mazoezi ili kuimarisha Afya

Dx and Rx

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,324
3,143
Salamu Wakuu, Habari za weekend.

Nina plan ya kuanza mazoezi kwa ajili ya kuimarisha Afya, huu mwili naona siuelewi, nahitaji kuuweka sawa hasa kuimarisha misuli ya viungo.

Nataka niwe na ka bike cha kimtindo cha kufanyia mazoezi kwa kurid huko barabarani badala ya kufuata bike za gym ambazo mtu unakuwa unaendesha ukiwa husogei.

Naomba kupewa muongozo, ni bike ipi nzuri na imara halafu ni ya bei ya kizalendo ili niweze kuipata na kuweza kutimiza haja yangu ya kuwa nafanya mazoezi kwa kuiendesha.

Wale wapenzi wa kuendesha bike mnaweza kutupia picha za bike mnazozipenda ili niweze kuchagua itakayonifaa.
 
Back
Top Bottom