Ni afya kwa Serikali kutoa taarifa za mapato na matumizi ya tozo ya miamala mara kwa mara

Aug 15, 2021
30
47
Serikali ilipiga kampeni kali ikielimisha juu ya umuhimu wa tozo ya miamala kuwa ingejenga miundombinu mbalimbali nchini ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Mwanzo wananchi walipiga kelele juu ya utitiri wa kodi au tozo mbalimbali jambo lililofanya serikali kujitokeza na kutolea ufafanuzi juu ya tija itakayopatikana kwenye tozo hizo. Am very open to the idea, sipingi tozo hata kidogo ijapokuwa mwanzoni nilipunguza miamala kupitia simu maana duu inauma bana.

Juzi kati nilituma hela kwa bi mkubwa na kama kawa ikakatwa(tozo) akaniuliza serikali inaonea watu imekata hela nyingi vp kwa wagonjwa wanaotumiwa ili wakatibiwe? Nikamjibu serikali inakusanya hela hizo ili zijenge nchi, akaniuliza mbona hatusikii taarifa za tozo kama ile kampeni?

Ndugu zangu viongozi mliopewa dhamana hasa waziri wa fedha ndg Mwigulu na wasaidizi wako hatuihitaji hadi msimu wa bunge ndio utoe taarifa za tozo bungeni, toeni taarifa za mapato kila mwezi through mass media na tujue zimetumika wapi na wapi hivyo ndio kujenga nchi na Imani kwa wananchi kwa yale mnayoyasema. Tozo zinauma bana but tukijua zimeenda wapi kufanya nini angalau machungu yanapungua.

Je, hili nalo linamwitaji Rais ndio afanye? Wasaidizi wa Rais mpo wapi katika hili? Fedha inaweza ikajenga au ikabomoa uongozi bora.
 
Back
Top Bottom