BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,804
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa ukusanyaji wa mapato na matumizi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) .
“Imekuwa ikifahamika kwamba mfuko huu umekuwa ukipata nakisi mwaka hadi mwaka 2019/20 walipata nakisi ya bilioni 49, 2020/21 nakisi ya bilioni 109 na mwaka wa fedha ulioisha yaani 2021/22 walipata nakisi ya bilioni 204 na ukiangalia hesabu walizofuga mwezi Juni mwaka huu walipata nakisi ya takriban bilioni 152, na mali za mfuko zimekuwa zikipungua kutoka trilioni 1.2 hadi trilioni 1.1 hadi sasa umefikia trilioni 1.09, Kwa hiyo ukiangalia hata trend ya mfuko wenyewe hata, Mtaji umepungua kutoka trilioni 1 hadi bilioni 700 na kitu Kwa hiyo ukiangalia trend ya mfuko inavyokwenda haileti sura nzuri katika uhai wa mfuko.
“Na nyie wote ni mashahidi ripoti ya Mkaguzi ikitoka mnasikia wapo watu wenye jinsia ya kiume ukienda kwenye mfuko unakuta wamejifungua,wapo watu wanatibiwa na kadi siyo za kwao ,wengine hawajiungi na mfuko mpaka wakiwa wanaumwa ugonjwa mkubwa kwa hiyo mi nadhani trend ya mfuko unavyokwenda hauleti sura nzuri katika uhai wa mfuko,’’.
‘’Sasa sababu zinazotolewa nyingi hazionyeshi ile sura halisi lakini kuna ishu kubwa sana ya umakini katika kusimamia rasilimali fedha na mifumo inayotumika katika usimamizi wa fecha,’’
Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jerry Slaa Agosti 17, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na Watumishi wa Mfuko huo Bungeni jijini Dodoma.
‘’Kwa hiyo ukiangalia trendi ya utendaji wake jukumu walilo nalo kwa sababu sasa hivi wana wanachma milioni 1.35 ambao wameongeza kutoka milioni 1.05 kipindi cha miaka mitatu kutoka 2020 Juni hadi 2022 Juni inaonyesha kwamba ufanisi unazidi kusinzia,’’.