Ni jambo jema kwa serikali kung'amua upotevu wa pesa za NHIF. Lakini pia kumekuwa na malalamiko kitambo sasa kuhusu makato mengi ya pesa kwa hospitali za serikali, kutokana na madai kwamba fomu za NHIF hujazwa kwa makosa mengi katika hospitali husika.
Wakati hayo yakitokea, hospitali za binafsi kama Mikocheni Mission Hospital, zimekuwa zikitajwa kutokuwa na makato kabisa. Kwa muda mrefu, habari zimekuwa zikisikika kwamba baadhi ya watumishi wa NHIF makao makuu wasio waaminifu, wako kwenye 'payroll' ya hospitali hizo.
Serikali chunguzeni madaktari wa NHIF wanaopitia fomu za hizi hospitali binafsi, na wale wote wanaopitisha malipo kwa hospitali kama hizo. IKUMBUKWE mara nyingi daktari anayejaza fomu ya madai kwa NHIF katika hospitali ya private ndio huyohuyo yupo hospitali ya serikali, iweje ajaze vibaya serikalini, halafu akiwa private ajaze vizuri, hasa ukizingatia hospitali za serikali hutoa motisha kwa watumishi wake, kwa kila mgonjwa atakayemhudumia ikiwa anatumia kadi ya NHIF?