Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 127
- 361
Binafsi sielewi kwanini NHIFTZ na Waziri was Afya @ummymwalimu wameamua kuwa waongo na wazandiki katika hili suala la bima ya afya ya NHIF. Wanachama tumewakosea nini? Mnataka roho zetu?
Swali langu lilihusu dawa namba 21 katika zilizoondolewa, beclomethasone with salbutamol inhaler ikiwa ni mchanganyiko wa dawa mbili ambazo zinatumika kusaidia kutuliza pumu kwa rika zote.
Nikasema kwamba, beclomethasone ni nzuri zaidi ukilinganisha na Salbutamol inhaler ikiwa ni dawa moja tu, kwa wagonjwa wenye pumu sugu (chronic asthma) ametumia dawa nyingi na hazimsaidii.
Dalili za awali kama kukohoa (coughing), kushindwa kupumua (wheezing), na kuhisi kukosa pumzi (feeling breathless). Hizi zinatibiwa na Salbutamol inhaler. Chronic wanapendekeza beclomethasone zaidi.
Salbutamol (albuterol) hupunguza dalili za pumu na ugonjwa sugu wa mapafu unaozuia mapafu (chronic obstructive pulmonary disease - COPD). Dawa hii imetajwa pia kutibu Chronic Asthma in Adults
NHIF mnasema beclomethasone with salbutamol inhaler haipo katika orodha ya dawa muhimu badala yake wameleta budesonide inhaler n fluticasone inhaler. WAONGO. Mmeamua kumtumikia shetani.
Standard Treatment Guidelines& National Essential Medicine List Tanzania Mainland imesaini na UMMY Mwalimu (Waziri wa Afya) na Dr. Mpoki Ulisubisya, beclomethasone ipo ndani ukurasa wa 115 of 464.
Standard Treatment Guideline (STG) imeelekeza vizuri kwamba beclomethasone matibabu ya severe persistent asthma. Au mnataka kusema sisi wanachama wa NHIF hatujui kabisa kusoma STG?
Mnamdanganya Rais @SuluhuSamia mkifahamu hawezi kufuatilia na wasaidizi wapo bizee kumpamba. Waziri wa @wizara_afyatz ndugu UMMY Mwalimu unadanganya kwenye mwezi mtukufu wa Ramadhan?
By Brigedia Mtikila, MMM.