Nguzo za Zitto Kabwe zimeisha, tumuombee

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,949
4,639
Jana mida ya mchana baada ya kupata tarifa kuwa aliyekuwa mkurugenzi wa NSSF bw Ramadhani Dau kuwa ameondolewa NSSF na kuteuliwa kuwa balozi wa Tanzania katika kituo ambacho hakijapangwa nilijua wazi kuwa vyanzo vya pesa vya Zitto sasa vimeyumba kabisa.

Sote tunajua wazi kuwa wafadhiri wakubwa wa Zitto Kabwe na ACT yake kwanza alikuwa marehemu Deo Filikunjombe aliyekuwa mbunge wa Ludewa mkoani Njombe kabla Mungu hajamchukua.

Mfadhiri mwingine mkubwa wa Zitto ni Ramadhani Dau ambaye alikuwa ndiye mkurugenzi wa NSSF kabla hawajala kichwa,Dau alikuwa ni mtu wa msaada sana kwa Zitto pamoja na ustawi wa chama chake cha ACT alikuwa akimpatia pesa nyingi sana tena pesa zenyewe ni zile za watanzania wala siyo za dau mwenyewe.

Ushirika wa Zitto na Dau ulishamili zaidi Zitto alipokuwa mwenyekiti wa PAC ambayo yeye Zitto akiwa mwenyekiti wa kamati hiyo ambayo ilikuwa ikihusika na ukaguzi wa mashirika ya umma NSSF likiwemo,Zitto alikuwa akimlinda Dau kwa nguvu zote licha ya kuwa na ufujaji mkubwa wa pesa za umma.

Sasa baada ya marehemu Deo Mungu kumchukua Zitto aliyumba sana kifedha hata namna ya kuendesha chama chake,sasa mbaya zaidi kigogo wake bwana Dau naye wamekula kichwa baada ya haya yote tegemeeni kuona Zitto akipagawa pamoja ustawi na ACT ukipukutika kwa kasi kubwa ,mtaona ACT ikidumaa kwa kukosa pesa za kuendeshea kazi zake.
 
Kwani katka kamati ya PAC zitto alikuwa anafanya kazi peke yake hadi iwe rahisi kiivyo kumtetea Dau? Na je hao wajumbe kutoka vyama vingine wangekuwa tayari kuvumilia jambo hili? Ipo haja yakutumia akili yako vizuri kabla hujaandika upuuzi kama huu. Unakera sana watu makini na wenye akili nzuri.
 

ZZK ni is a rare asset kwa Tanzania. Ni mtu anayefikiri kwa mapana, anayetoa arguments ambazo ni researched na si mtu wa Mkumbo. He is simply gifted, and a leader! Anavutua kumsikia, ku- msaport. Hata kama hao mnaofikiri ndiyo walikuwa wanamsaidia hawapo kwenye madaraka sasa atapata partners wengine.
 
Kama hujuwi nafasi na nguvu ya mwenyekiti kwenye kamati yoyote unaweza kuongea haya mfano mzuri ni ndani ya chama chako cha chadema angalia mbowe anavyokichezea chadema mara anabadili gia angani,mara anaita mafisadi kuwa wagombea urais na hakuna wa kumzuia.
 
Sometime namkubali Zitto kwa kuwa huwa anachukiwa na watu mbalimbali wenye tabia moja inayofanana "Chuki" dhidi ya wenye akili.
 
Hivi kumbe 'wamekula kichwa'? Si alishafikia muda wa kustaafu lakini? Naona kama ameongezewa zulia jekundu...
 
Na hapa unatudhihirishia madudu yote yaliyofanyika katika utawala wa awamu ya nne yana mkono wa mwenyekiti wa CCM taifa chini ya kofia mbili.Kwani yeye ndie aliekuwa na mamlaka makubwa serikalini na katika chama chake.
 
Nilichokiona kwa muda mrefu wanachama wengi wa CCM wanapenda sana kutukana,kukashfu na kupandikiza skandol kwa wapinzani,ngoja uwarudi watatotoka huko kama wamemwagiwa maji ya moto
 
Habari nilizozikuta hapa kigoma kuhusu zitto na Simiyu yetu anayo andika nazidi kuamini
Kijana alikua anapiga pesa kwa style yake
 
End of the road(?)
 
Uko tayari kutoa ushahidi mahakamani ili Zitto afungwe kwa kula rushwa toka kwa Dau?
 
Mfadhili wa ACT ni CCM ... rejea mgawo wa 700,000,000/-
 

Tagia lini ulikwa mhasibu wa Zitto?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…