SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 6,481
- 10,448
Tukiweka ushabiki pembeni, safu ya ulinzi ya Yanga imethibitisha kwa misimu miwili sasa kuwa ni safu ngumu sana kupitika si tu katika mashindano ya ndani ila hata ya kimataifa. Kuna jinsi hawa vijana wanajua kuwajibishana ndani na nje ya uwanja kiasi kwamba kila mmoja wao anahakikisha hazembei na makosa hayatokei mbele yake.
Safu ya kiungo ya Stars bado ina shida kubwa na ushambuliaji ndiyo tatizo ni kubwa zaidi. Shida kubwa ni wale tunaowategemea ni "maji ya jioni" halafu hakuna mbadala kabisa nje, ni kama tulisahau kabisa kwa kipindi cha miaka 5 kuandaa washambuliaji wapya. Hivi Samatta mara ya mwisho kufunga goli kwa Taifa Stars ni lini?
Tunapokwenda kupambana na Morocco hivi leo, tegemeo letu kubwa ni safu ya ulinzi, kule mbele hakuleti matumaini kabisa yaani. Baada ya mechi ya leo, Kocha afikirie kuongeza wachezaji kama Chilunda ili hao kina Samatta wasijione bila wao mambo hayaendi.
Feisal akiwa kwenye ubora wake, anaenda kuwa na gemu nzuri sana.