Ngorongoro Royal Tour

Shabani Ajaha

Member
Aug 18, 2021
78
60
UVCCM-TAIFA

KARIBUNI WOTE TUKATALII KATIKA VIJANA NGORONGORO ROYAL TOUR

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM) Taifa umeandaa VIJANA ROYAL TOUR itakayoanza Tarehe 03 - 05/06/2022. na Msafara utaongozwa na Katibu Mkuu wa UVCCM Ndugu Kenani L. Kihongosi

Utaratibu uktakuwa kama ifuatavyo:-

Wote wanaotaka kushiriki wanatakiwa kufiika Dodoma na Safari itaanza Rasmi Tarehe 03/06/2022 tutaanza safari kutoka Dodoma kuelekea Karatu Saa 2.00 Kamili Asubuhi Kwa usafiri wa Pamoja, Tutalala Karatu.

Asubuhi saa 12.00 Kamili Tarehe 04/06/2022 tutakuwa na safari kutoka Karatu kutalii ngorongoro siku nzima mpaka Jioni na Tutarudi Karatu.

Tarehe 05/06/2022 tutatoka Karatu kurudi Dodoma

Gharama ya safari ni shilingi elfu sitini (60,000/=)tu.

Lengo la VIJANA NGORONGORO ROYAL TOUR ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuhamasisha utalii nchini, Kazi Kubwa ameifanya na Fursa nyingi za Utalii zimefunguka.

Vijana tunatambua mchango mkubwa wa Sekta ya Utalii katika Kukuza Uchumi wa Taifa Letu pamoja na Kuleta Ajira.

Wote mnakaribishwa.

#AlipoMamaVijanaTupo
#ShirikiUchaguziKwaUadilifu
#2022JiandaeKuhesabiwa
#KaziIendelee

IMG-20220513-WA0065.jpg
 
Back
Top Bottom