Ngorongoro hatarini kupoteza uhai na umaarufu wake kutokana na kukithiri kwa shughuli za binadamu

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
956
1,038


Mtandao wa DarMpya Media umeripoti makala fupi inayoonyesha hali ya Hatari ya kutoweka kwa hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kutokana na kuingiliana kwa kasi kubwa baina ya binaadamu, mifugo, uhifadhi na wanyama pori.

DSCN7043.JPG

Katika Makala hiyo fupi Dar mpya ambao wamerejea andiko la Gazeti la JAMVILAHABARI wameonyesha mambo mbalimbali ikiwe ujenzi wa nyumba za matofali ambazo haziruhusiwi kisheria hifadhini, Ujenzi wa Nyumba za Ghorofa ambazo haziruhusiwi Hifadhini, Kuongezeka kwa mifugo kutoka chini ya mifugo elfu hamsini hadi zaidi ya mifugo milioni moja hivi sasa, kuongezeka kwa watu kutoka watu 8000 hadi zaidi ya watu laki moja hivi sasa.

Pamoja na yote makala hii inatoa mwanga na mwelekeo chama kwa wadau wa uhifadhi, mazingira na haki za binaadamu za kutafuta suluhu ya pamoja na ya haraka.

Tafadhali fuatilia makala hii fupi kukielimisha kuhusu Ngorongoro

DSCN7080.JPG

HATARI NGORONGORO
- Siku za uhai wa Hifadhi ya Taifa hiyo yenye sifa za kipekee Duniuani zinahesabika

- hali ya muingiliano wa shughuli za binaadamu, mifugo, uhifadhi na utalii yazidi kuwa mbaya

- Makundi ya Mifugo mamia kwa maelfu yatanda kila kona ya hifadhi, magari ya watalii yapishana na Ng’ombe na kondoo barabarani badala ya Wanyama pori

- Matajiri wajenga majumba ya kifahari Hifadhini kinyume cha sheria iliyounda hifadhi hiyo huku wakitumia neno umasikini kama kinga

- Mabilioni ya shilingi yatengwa na asasi kutoka nchi jirani kuhakikisha hifadhi hiyo inapoteza umashuhuli wake

Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ipo hatarini kupotea na kupoteza uhai na umashughuli wake kutokana nna kukithiri kwa shughuli za kibinaadamu ikiwemo ufugaji uliopitiliza kiasi, ujenzi wa nyumba zisizofuata taratibu za kihifadhi na shughuli nyingine za kibiashara

Mwaandishi wa habari hizi ameshuhudia bmakundi makubwa ya mifugo ikiwemo Ng’ombe, mbuzi, kondoo, punda, kuku, na mingineyo ikichukua eneo kubwa kuliko Wanyama wa asili wanaopendwa kufuatiliwa na watalii

Pamoja na kuzingatia ukweli kuwa Ngorongoro ni hifadhi ni hifadhi ya kipekee inayowahusisha Wanyama binaadamu na mifugo kwa pamoja lakini hali ilivyo kwa sasa inatisha kiasi cha kutishia usalama wa hifadhi na wananchi husika wa asili wanaoishi katika eneo hilo.

DSCN7099.JPG

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili imezitafiti ni kuwa mwaka 1959 wakati wakazi walioruhusiwa kuishi katika hifadhi hiyo kwa mchanganyiko wao na Wanyama pori, wakazi hao hawakuzidi watu elfu 9 tofauti na sasa wakazi hao wamefika zaidi ya laki moja na mifugo yao bwanayoimiliki ikikadiriwa kuwa zaidi ya laki6

‘’kwa mujibu wa taarifa wanasema kuna mifugo laki 2 na nusu, nadiriki kusema sio kweli, mifugo hii haipungui haipungui laki saba hadi laki nane…hebu angalia tangu tumeanza kuanza makundi ya ng’ombe, mbuzi na kondoo sasa hivi ni zaidi ya masaa mawili tunazunguka tunawaona tu…hii maana yake kuwa hata kama watu hawa wapo kisheria lakini inahitajika jitihada za makusudi kunusuru tatizo hili…hili ni tatizo kwa kweli’’. Alisema Paul Schenzern Raia wa ujerumani aliyekuwa katika safari za kitalii

Schezern ameongeza kuwa kwao wanavyoifahamu Ngorongoro nin kuwa eneo bora zaidi la kiutalii na kamwe hakuwaza kama angepita barabani akipishana na ng’ombe na mifugo mingine japokuwa alikuwa anaufahamu kuwa Ngorongoro wanaishi binaadamu na Wanyama lakini si kwa kiwango alichokiona

‘’nimetembea hifadhi kadhaa Duniani ambazo Wanyama na binaadamu wanaishi kwa asili, kwa kweli zinavutia n ahata kuishi kwao kunaemndana na uhifadhi wa mazingira, tofauti na hapa Ngorongoro…ntapata shida san akumshawishi mtu atakayeniomba ushauri juu ya kutaka kuja hapa. Nafikiri watetezi wa haki za binaadamu, mifugo, Wanyama na mazingira wanapaswa kupaza sauti ya pamoja kuinusuru hifadhi hii muhimu na bora’’. aliongezq

DSCN7085.JPG

‘’unajua watu wanaweza kulalamika kwamba wanaishi humu na haipaswi kupangwa vizuri, lakini sio sahihi watetezi makini wa binaadamu wanatakiwa watetee kwanza usalama wa mazingira, usalama wa mazingira ya Ngorongoro ndio usalama wa Arusha, usalama wa Arusha ndio usalama wa Tanzania na ndio maana Dunia nzima kunakuwa na sheria kali zinazolinda mazingira.

Kujazana kwa watu na mifugo hifadhini sio haifai tu kwa mifugo bali haifai zaidi kwa binaadamu wanaoishi nhumo kwani kuishi kwao kunategemea zaidi ikolojia nya hifadhi husika’’. Alisema Habibu Mchange, Mratibu wa mtandao wa wanahabari wanarasilimali asilia na taarifa alipoombwa kutoa maoni yake.

DSCN7075.JPG

Mchange alisema kuwa hata yeye alikuwa Ngorongoro mwishoni mwa mwaka jana na ameshuhudia ujenzi uliokithiri na unaovunja kabisa sheria na kanuni za uhifadhi na kuongeza kuwa anaandaa ziara ya wanahabari wanarasilimali asilia na taarifa kwenda kujionea hali ilivyo na kuuhabarisha umma na kuwataka wanaharakati kushirikiana kuokoa kivutio hicho muhimu

‘’hata mimi nilitembbea tembea mwishoni mwa mwaka, niliyoyaona Ngorongoro kwa kweli yanatisha na hayafai kusimuliwa hata kidogo, wadau nwa utalii, uhiofadhi na mazingira tusipochukua hatua na kupaza sauti, Ngorongoro itapotea kama upepo…..kwa kifupi tu nikuambie ndugu mwandishi kuwa NGORONGORO IPO HATARINI KUPOTEA’’. Aliongeza Mratibu Mchange


Taarifa na uchunguzi zaidi kuhusu kuharibika kwa ikolojia Ngorongoro na mitazamo ya wahusika wa pande zote muhimu tutawaletea katika matoleo ya siku zijazo

NOTE:-
Picha zote zilizokuwa attached katika uzi huu ni picha zilizopigwa ndani ya eneo la Hifadhi.

DSCN7080.JPG
 
Watu wanaishi katika eneo walilochagua kuishi zamani sana kabla ya ukoloni. Kabla ya ukoloni hakukuwepo na hifadhi.

Waacheni watu waishi na wanyama kama walivyozoea.

Kama hamtaki kuona kondoo na mbuzi, mkatembee Kisutu, Upanga, Kivukoni na Oysterbay.
 
Baadhi ya Picha za hifadhi ya ngororo zinazoonyesha namna muingiliano baina ya watu, mifugo na shughuli nyingine za kibinaadamu ikiwemo ujenzi zinavyoathiri Ikolojia na uhifadhi. Hatua muhimu na za haraka zinapaswa kuchukuliwa kuikoa hifadhi hii bila kuathiri maisha ya wenyeji wa asili.View attachment 2095940View attachment 2095943View attachment 2095941View attachment 2095942View attachment 2095944View attachment 2095945View attachment 2095946View attachment 2095947
Hizo nyumba za kifahari ziko sehemu gani,mifugo na wamasai walikuepo kabla ya kuwa hifadhi kipindi hicho babu zako wako kirua
 
Watu wanaishi katika eneo walilochagua kuishi zamani sana kabla ya ukoloni. Kabla ya ukoloni hakukuwepo na hifadhi.
Waacheni watu waishi na wanyama kama walivyozoea.
Kama hamtaki kuona kondoo na mbuzi, mkatembee Kisutu, Upanga, Kivukoni na Oysterbay.
Kabla ya ukoloni ni Lini?
 
Pendo lyimo nimeona picha moja lakini kama nakumbuka hapo ni makao ambapo kuna ishi watu na sio crater.

Hifadhi inayo shida nakumbuka 2004-2005 kulikuwa na mkakati wa kupunguza idadi ya magari na watu yanayoingia kwa wakati mmmoja.Eidhaa ingekuwa kwa zamu au kwa siku idadi maalum.Pia mkakati mwingine ikawa wanawatoa staff wanaoishi makao ili wawe wanatoka karatu kwenda ngorongoro kila siku na jioni wanarudi karatu.

Mkakati huo pia ulilenga na wafanyakazi wa mahotelini lakini ikawa ni ngumu kwa sababu wageni wanaolala kwenye mahoteli ndani ya Hifadhi watataka huduma za usafi na chakula kwa hiyo ikawa kuna kipengele.

Hoteli kipindi hicho zilikuwa Serena,CCA Africa (Conscorp)Ngorongoro Crater Lodge)Wildlife Lodge, Baadaye ikaja Rhino.Kwa hiyo hapo kuna wafanyakazi ambao lazima waishi ndani ya Mgodi!

Kwa hiyo Wafanyakazi wa Hifadhi wametolewa nje wengi wanaishi karatu nje ya mji kidogo kuna Maghorofa yao. pale karibu na barabara!Waliona wafanyakazi wa Hotelini italazimu watoke alfajiri kwenda hifadhini na wakahofia ajali za magari pamoja na wanyama kugongwa!Hifadhi kuwa safi ki ecologia ni watu kutoka au kupungua na magari ipangwe idadi kwa siku.
 
Nadhani Rais SSH kwa msaada na nguvu ya ushawishi ya Dr. Edward Lowassa (Dr wa siasa za Tanzania kwa miongo miwili) wanalivutia kasi suluhisho. Iliwezekana wamachinga watoke Dar barabarani na kuchomwa masoko yajengwe kwa upya, hata Ngorongoro wataweza na tunaitia serikali shime ifanye hivyo.

Pengine kabla ya kukabidhi mifugo iwe chakula majeshini au kuweka kambi ya jeshi kuwaondoa watu, pengine pia serikali ije na package kwa wanaotakiwa kuondoka kwenda Morogoro au Kiteto nk mfano kila boma wawe wanalipwa mshahara wa laki 5 maisha yao yote na kusomeshewa watoto mpaka chuo ikiwa watakubali kutoka hapo.

Au / na kutoruhusiwa mtu yoyote katika maeneo flani au ya ukubwa flani kuwa na mifugo zaidi ya idadi flani nk nk. Wakiachwa tatizo litakua na kupanuka beyond reach.

Tufanye sasa vinginevyo watakuja wale marais matapeli na wezi waseme hapa ndio kwenu nyie wanyonge na wapiga kura wangu mtu asiwaguse! Huo ndio ushauri.
 
Nadhani Rais SSH kwa msaada na nguvu ya ushawishi ya Dr. Edward Lowassa (Dr wa siasa za Tanzania kwa miongo miwili) wanalivutia kasi suluhisho. Iliwezekana wamachinga watoke Dar barabarani na kuchomwa masoko yajengwe kwa upya...
Inaonekana hamjui hata chanzo cha umaarufu wa hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro duniani.

Mnakurupuka tu na njaa zenu mnatoa ushauri wa kuipotosha serikali.
 
Kwa akili tu za kawaida iko wazi kua hiyo hifadhi baada ya miaka kadhaa mbele haitakua tena hifadhi.na hilo kosa lilifanywa na serikali yenyewe kuendekeza siasa zaidi badala yakuweka sera na mikakati madhubuti kwaajili ya rasilimali za nchi.

kama serikali haitafanya maamuzi magumu yakunusuru ilo eneo hali itakua mbaya zaidi uko mbele,hili lakutaka kushikilia vyote kwa pamoja nikitu ambacho kamwe hakitawezekana.

Ningekua mimi ndiye rais wa nchi ningefanya maamuzi magumu yafuatayo,(1)Ningetafuta eneo jingine la malisho la hao wananchi waliopo ndani ya hifadhi kwasababu hii nchi bado ni kubwa na bado kuna maeneo mengi sana(2)Ningetenga pesa za fidia kwa wananchi hao(3)

Ningetoa muda wawao kuhamia eneo jipya kwa utaratibu wa serikali baada ya hapo ningepitisha operesheni yakijeshi yakusafisha eneo lote la hifadhi(4)Ningevunja mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro na kuiunganisha na TANAPA na eneo la hifadhi ningeliunganisha na hifadhi ya serengeti nakutengeneza hifadhi moja matata sana duniani.ningehakikisha inakua hifadhi moja yakisasa ambayo dunia nzima ingehamia kuja kuitembelea.Ningehakikisha kwa kipindi cha miaka mitano pesa ambayo ningekusanya hapo ingekua haielezeki.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Binadamu ndio Myama muharibifu kuliko wanyama wote..., na uharibifu huo na kuongezeka kwake exponentially asipobadilika ni suala la muda tu yeye mwenyewe ndio atakuwa chanzo cha extinction yake...
 
Watu wanaishi katika eneo walilochagua kuishi zamani sana kabla ya ukoloni. Kabla ya ukoloni hakukuwepo na hifadhi.
Waacheni watu waishi na wanyama kama walivyozoea.
Kama hamtaki kuona kondoo na mbuzi, mkatembee Kisutu, Upanga, Kivukoni na Oysterbay.
Ata kama uliishi kabla ya dunia kuumbwa serikali inaweza kuamua kupanga wakazi wake upya.kwasababu ni wajibu wa serikali kuhudumia mambo ya msingi ya wananchi wake.

Huduma kama mashule,hospital na miundombinu mbali mbali ni wajibu waserikali na inapobidi kuhamisha wakazi flani kwa ajili ya rasilimali za nchi inaweza kufanya ivyo pia.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom