Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Januari 20, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;
Wachezaji wa Mbeya City (Kelvin John na Majaliwa Shaban) na Yanga Sc (Mrisho Ngasa ,Ramadhani Kabwili na Cleafas Sospeter kila mmoja amefungiwa michezo mitatu(3) na Faini ya kiasi cha Shilingi Laki Tano(500,000/=) kila mmoja kwa kosa la kugoma kuingia vyumbani
Klabu ya Tanzania Prisons na Yanga Sc zimepigwa Faini ya Tsh.500,000/=(Laki Tano) kila mmoja kwa kosa la kutokuwakilisha vikosi vya timu zao kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo katika mechi hiyo iliyochezwa Disemba 29,2019 katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Kocha wa Klabu ya Yanga amepewa Onyo kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi yasiyofaa na Klabu ya Yanga imeelekezwa kumuelimisha kocha wao na kusimamia nidhamu kwa ujumla.
Klabu ya Yanga Sc imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na Washabiki wa timu yake kurusha chupa za maji kuelekea uwanjani na pia wakati wa mapumziko washabiki hao waliwarushia chupa za maji waamuzi wakati wanaelekea vyumbani katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 04,2020
Vile vile katika mchezo huo Klabu ya Yanga Sc imepigwa Faini ya Tsh.200,000/=(Laki Mbili) kwa kutokutumia chumba rasmi kilichoandaliwa kwa kubadilishia nguo.Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo
Mjumbe wa Kamato ya Utendaji wa Klabu ya Coastal Union Bw Salum Perembo amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kutaka kuingia uwanjani kwa lengo la kuwashambulia waamuzi huku akitoa maneno makali katika mechi iliyofanyika Januari 11.2020 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Timu ya Njombe Mji imepoteza mchezo dhidi ya Friends Rangers baada ya kuwa na wachezaji pungufu ya saba(7) katika mechi iliyofanyika Januari 19,2020 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.Hivyo timu pinzani imepewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu.
Klabu ya Mkamba Rangers imepoteza mchezo dhidi ya timu ya Villa Squard baada ya timu hiyo kufanya udanganyifu wa Leseni kwa kubandika picha(sura) za wachezaji wengine katika ;leseni halali zilizotolewa na TFF. Mchezo huo uliyofanyika Disemba 10,2019 katika uwanja wa Jamhuri mjini
Hivyo timu ya Villa Squard imepewa pointi tatu na magoli matatu katika mechi hiyo kwa mujibu wa Kanuni namba 14(36) kuhusu Taratibu za Mchezo
Vile vile viongozi wa Tiimu ya Mkamba Rangers Katibu(Bw.Azizi Mfayeka), Timu Meneja(Kelvin John) na Kocha(Rashid Tuli) wamepelekwa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kitendo cha Udanganyifu wa leseni za wachezaji.
Pia Kamishina wa mchezo huo Bw Laurent Chacha amepelekwa katika Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).
My Take
Huyu kocha amehurumiwa sana,alistahili kufutiwa kibali cha kufanya kazi