Ngasa na wachezaji wengine wafungiwa mechi tatu na kulipa faini. Kocha wa Yanga apewa onyo kwa matamshi ya ubaguzi wa rangi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,221
115,129
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) katika kikao chake cha Januari 20, 2020 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;

Wachezaji wa Mbeya City (Kelvin John na Majaliwa Shaban) na Yanga Sc (Mrisho Ngasa ,Ramadhani Kabwili na Cleafas Sospeter kila mmoja amefungiwa michezo mitatu(3) na Faini ya kiasi cha Shilingi Laki Tano(500,000/=) kila mmoja kwa kosa la kugoma kuingia vyumbani

Klabu ya Tanzania Prisons na Yanga Sc zimepigwa Faini ya Tsh.500,000/=(Laki Tano) kila mmoja kwa kosa la kutokuwakilisha vikosi vya timu zao kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo katika mechi hiyo iliyochezwa Disemba 29,2019 katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Kocha wa Klabu ya Yanga amepewa Onyo kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi yasiyofaa na Klabu ya Yanga imeelekezwa kumuelimisha kocha wao na kusimamia nidhamu kwa ujumla.

Klabu ya Yanga Sc imetozwa faini ya sh. 500,000 kutokana na Washabiki wa timu yake kurusha chupa za maji kuelekea uwanjani na pia wakati wa mapumziko washabiki hao waliwarushia chupa za maji waamuzi wakati wanaelekea vyumbani katika mechi hiyo iliyofanyika Januari 04,2020

Vile vile katika mchezo huo Klabu ya Yanga Sc imepigwa Faini ya Tsh.200,000/=(Laki Mbili) kwa kutokutumia chumba rasmi kilichoandaliwa kwa kubadilishia nguo.Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo

Mjumbe wa Kamato ya Utendaji wa Klabu ya Coastal Union Bw Salum Perembo amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kutaka kuingia uwanjani kwa lengo la kuwashambulia waamuzi huku akitoa maneno makali katika mechi iliyofanyika Januari 11.2020 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Timu ya Njombe Mji imepoteza mchezo dhidi ya Friends Rangers baada ya kuwa na wachezaji pungufu ya saba(7) katika mechi iliyofanyika Januari 19,2020 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.Hivyo timu pinzani imepewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu.

Klabu ya Mkamba Rangers imepoteza mchezo dhidi ya timu ya Villa Squard baada ya timu hiyo kufanya udanganyifu wa Leseni kwa kubandika picha(sura) za wachezaji wengine katika ;leseni halali zilizotolewa na TFF. Mchezo huo uliyofanyika Disemba 10,2019 katika uwanja wa Jamhuri mjini

Hivyo timu ya Villa Squard imepewa pointi tatu na magoli matatu katika mechi hiyo kwa mujibu wa Kanuni namba 14(36) kuhusu Taratibu za Mchezo

Vile vile viongozi wa Tiimu ya Mkamba Rangers Katibu(Bw.Azizi Mfayeka), Timu Meneja(Kelvin John) na Kocha(Rashid Tuli) wamepelekwa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kitendo cha Udanganyifu wa leseni za wachezaji.

Pia Kamishina wa mchezo huo Bw Laurent Chacha amepelekwa katika Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).

My Take
Huyu kocha amehurumiwa sana,alistahili kufutiwa kibali cha kufanya kazi
 
Huyu jamaa mbona namfananisha kama mfanyakazi wa Meli moja ya Ugiriki
 
mpira wa tanzania kukua ni ndoto, Njombe mji wamepoteza mchezo kwa kuwa na wachezaj pungufu, yaan wametoka njombe mpaka dar na wachezaj chini ya saba, ajabu kabisa,
 
Ligi yetu ni majanga.Ebu tuelekezeni akili kwenye kikosi kikali cha kutufikisha Qatar 2022 kundi letu siyo baya "kihivyo".
 
Kamati ya masaa 72 iwe ni masaa 72 kweli. yaani mnatoa adhabu kwa matukio yaliyofanyika mwezi umeisha ndio mnakuja kutoa maamuzi leo. Au hamjui kwamba hii ndio VAR yetu?
VAR is a modified Kamati ya Masaa 72
Kwahiyo fanyeni haraka.

Halafu jamani mbona mnataka kuwaua hawa yanga?
Yaani hawana hata hela ya kula halafu mnawapiga mafaini kibao au mtayaandika kama madeni?
Wanawaza hela ya kula na mafuta ya basi lao halafu mnawaongezea balaa kubwa zaidi. Kuweni na huruma kama mimi
 
Kamati ya masaa 72 iwe ni masaa 72 kweli. yaani mnatoa adhabu kwa matukio yaliyofanyika mwezi umeisha ndio mnakuja kutoa maamuzi leo. Au hamjui kwamba hii ndio VAR yetu?
VAR is a modified Kamati ya Masaa 72
Kwahiyo fanyeni haraka.

Halafu jamani mbona mnataka kuwaua hawa yanga?
Yaani hawana hata hela ya kula halafu mnawapiga mafaini kibao au mtayaandika kama madeni?
Wanawaza hela ya kula na mafuta ya basi lao halafu mnawaongezea balaa kubwa zaidi. Kuweni na huruma kama mimi
Hawa Yanga wanamatukio ya ajabu ajabu sana,
Msimu uliopita walipigwa faini hadi zilifika M 15, kisa tu Mara hawajaingia uwanjani kupitia mlango maalumu, Mara wameruka ukuta,
Acha wapigwe faini kwa mambo yao ya kitoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa Yanga wanamatukio ya ajabu ajabu sana,
Msimu uliopita walipigwa faini hadi zilifika M 15, kisa tu Mara hawajaingia uwanjani kupitia mlango maalumu, Mara wameruka ukuta,
Acha wapigwe faini kwa mambo yao ya kitoto

Sent using Jamii Forums mobile app
Nasikia Wawa amepongezwa kwa faulo ya makusudi aliyomchezea Ditram Nchimbi eti kwa kuwa alitekeleza maagizo aliyopewa na TIFUA TIFUA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yapo matukio yakuacha ila sio lile la Wawa la kutaka kumdhuru Ditram! Jukumu mojawapo la mwamuzi ni kulinda usalama wa wachezaji uwanjani!

Sent using Jamii Forums mobile app
Eti kwa vile alimsukuma mpaka nje ya uwanja mwamuzi likawa sio jukumu lake lakini mwamuzi huyo huyo anampiga kadi ya njano kocha ambae yupo nje ya pitch ya kuchezea
 
Hawa Yanga wanamatukio ya ajabu ajabu sana,
Msimu uliopita walipigwa faini hadi zilifika M 15, kisa tu Mara hawajaingia uwanjani kupitia mlango maalumu, Mara wameruka ukuta,
Acha wapigwe faini kwa mambo yao ya kitoto

Sent using Jamii Forums mobile app
Ile Yanga ya Zahera ilikuwa na vituko, kila siku wanaibuka na jipya.
 
Back
Top Bottom