News Tip: Tani 5 za meno ya Tembo zanaswa maeneo ya Kimara, Dar!

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Wakuu,

Inaweza kuchukuliwa kama tip tu kwa sasa lakini ni kuwa mchana wa leo zimenaswa takribani tani 5 za meno ya Tembo maeneo ya Kimara jijini Dar.

Taarifa zaidi naamini zitatolewa na Vyombo vya Dola na naamini si muda mrefu kuanzia sasa.

Mjumbe hauawi
 
Hii habari itapotea kama ilivyopotea ile ya Dodoma Mhindi kukutwa na rundo la noti kwenye beg akiwa hotelini kisha tukaambiwa alikuwa anaenda kununua sijui vitu gani(wanajua wenyewe).
 
Hii habari itapotea kama ilivyopotea ile ya Dodoma Mhindi kukutwa na rundo la noti kwenye beg akiwa hotelini kisha tukaambiwa alikuwa anaenda kununua sijui vitu gani(wanajua wenyewe).

Sasa unajua kwanini imeletwa huku
 
Tuibane china, itunge sheria kali kukutwa na meno ya tembo na pembe za faru iwe kosa sawa sawa na kukutwa na madawa ya kulevya nchini mwao na adhabu ifanane ndio tembo na faru wetu watasalimika.

Ama la sivyo tukicheka nao
 
Halafu wanatudanganya hamna uchakachuaji tena!!!!!
 
Kuna watu wanaendekeza njaa zao na hawaoni shida kama Tanzania itachinjiliwa mbali. Wapewe somo ambalo hawatakaa kulisahau
 
The tusks of the Asiatic elephants are generally smaller than those of the African elephants. The longest tusk of an Africanelephant measured 3.264 meters, the heaviest one weighed102.7 kilograms.
===================================================
Fikiria kilo 100 kwa kila jino la tembo/ndovu. tani 5 X 1000 kg =5000 kg; 5000 kg /100 kg/jino =meno 50 ya tembo; meno 50 / 2 meno/tembo = tembo 25. Kwa hiyo kuna uwezekano zaidi ya tembo 25 wameuwa na majangili.
------------------------------------------------
Hawa watolewe mfano, wajue kuwa sasa uongozi wa sasa siyo lelemama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…